Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud akitoa hotuba katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar kufuatia fujo zilizotokea Zanzibar na kusababisha Kuchomwa moto kwa Kanisa hilo, hapo katika ukumbi wa Kanisa hilo Kariakoo Mjini Zanzibar.hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.Picha na Idara ya Habari Maelezo- Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2012

    Well vizuri waliochoma moto kanisa hawakutendea haki wakristo wala waislam sasa inaonesha kuwa Zanzibar kama kuna chuki za kidini wakati hakuna,kuna sababu tu zilopelekea hayo.

    Ok la pili waziri angetuonesha na Picha ya kubuni vile vile ya Muungano ingekua uzuri zaidi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2012

    Wakristu waislamu wote sisi ni binadamu ni ndugu mungu wetu ni mmoja hamna mungu mwingine, tupendane, tuache chuki sisizokuwa za msingi. Ni wazanzibari wangapi wako wanaishi bara kwa amani na tunaishi nao kama ndugu hata unyanyasaji wa aina yeyote haupo, leo hii huko visiwani mnafanya mambo ya aibu kabisa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2012

    Waafrika wana matatizo sana nafikiri baadhi vichwa vyao si sawa.
    Mnagombania dini kwani nyie ndio MUUMBA???
    Acheni kila mtu aabudu anachotaka. Tumieni muda kujiletea maendeleo kama nchi zilizoendelea, si kukaa chini kujadili na kugombania mambo ya kipuuzi.Usheitwani mtupu!
    Mfano nchi kama UK watu wapo wa dini kibao toka pande zote za dunia, kila mtu na time yake, ninyi mnachomana moto.
    Ole wao wanaohukumu wenzao kwa misingi ya dini, adhabu kali ya Mola iko juu yao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2012

    Zanzibar wanataka hiyo nchi iwe islamic country Muungano ukishavunjika. Hiyo ndo Agenda kubwa uliyokuwa ikitayarishwa na hao UAMSHO. Wameaanza hayo miaka mingi iliyopita kwa maana huo muungano ni moja ya sababu lakini jambo lao kubwa ni Dini yao ili wangie wenye Dini kali waseme na waamrishe wanavyotaka.Yameenza siku nyingi na viongozi wameyaona na wameyadharau wenye akili zao wanajua vizuri.Wapeni nchi yao. nawaonea huruma wakristo maana nchi nyingi za kiislam hazina report nzuri kwa minorities wao e.g. Saudia,Pakistan,Eygpt etc.Zanzibar ya zamani haipo tena Abdallah Mwinyi anakumbuka alivyokuwa anaishi vizuri na marafiki zake wakristo kwa upendo na amani.Sasa ni Dini kali ambayo ina chuki mbaya sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2012

    Hili tukio ni jambo la aibu na la kusikitisha sana!Tumesikia kupitia vyombo vya habari kwamba,kisa cha kuchoma makanisa na hata kutishia au kuwaamuru Wabara warejee makwao,hawahitajiki visiwani Zanzibar,eti kwasababu Wazanzibari hawautaki Muungano,"huu ni uwendawazimu na ukosefu wa akili uliopitiliza".Suala la Muungano na uchomaji makanisa vinahusiana nini?Kwa kitendo hicho cha kihuni,hata wale "sympathisers" watu ambao wangependa kutoa support kwa wazanzibari katika madai yao ya msingi watashindwa kufanya hivyo jamani!Kwanini lakini iwe hivyo?Hivi Bara wanachokipata kutoka visiwani nini hasa cha maana zaidi ya kuimarisha Ulinzi na Usalama wa pande zote mbili kwa manufaa ya Taifa letu la Tanzania?Wazanzibari wanaweza kuachiwa kabisa wafanye watakavyo,lakini lazima watambue kwamba linapokuja suala la Ulinzi na Usalama wa Taifa letu,hakuna mjadala,lazima Jeshi litakuwepo moja kwa pande zote mbili,na Polisi itakuwepo moja kwa pande zote mbili,hakuna namna nyingine!They can do what they want.Hili sio suala la lulichukulia kimzaha mzaha hivi,eti waliotenda makosa hayo ni vijana wadogo wa under 18! This is absolute nonsense!Wakati umefika sasa watu wapuuzi washikishwe adabu!This can not be allowed to continue!We know what is happening there! Tume ya Katiba imeundwa kushughulikia pamoja na masuala hayo ya Muungano.Eti ifanyike Kura ya Maoni kwanza kuhusu Muungano,ndipo Suala la Katiba Mpya lifuate.Huu Ujinga umetoka wapi?Kamwe usipewe nafasi.Tutafute njia bora zaidi ya kuwafanya wazanzibari waendeshe mambo yao wao wenyewe bila ya kuingiliwa lakini wakiwa ndani ya jamhuri ya muungano,no other way!Bara haihitaji chochote kutoka visiwani zaidi ya ulinzi na usalama!sheria ichukue mkondo wake!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    Ni upumbavu ulioje watanzania "waliopotoka na wenye mtazamo finyu"kuendelea kufikiri na kuamini kwamba Muungano uliletwa na watu wawili tu,Nyerere na Karume!Back to colonila times,Bara na Visiwani zilikuwa pamoja na wamoja!Waarabu walipokuja kutoka Oman,hawakuishia Zanzibar tu!Infact,waliweka makao yao makuu Dar es salaam, na kuitawala Pwani yote ya Afrika Mashariki!Walivuka mipaka naa kusafiri ndani zaidi ya Bara hadi Tabora,Kigoma na kupitiliza hadi Kisangani na Bukavu nchini Congo!Kote huko walisomba watu,wake kwa waume,mababu zetu na kuwapeleka Bagamoyo na Zanzibar kuwauza kama Mbuzi utumwani!ushahidi huo upo hadi hii leo!Vizazi vilivyo zaliana kwa kiasi kikubwa na Uzao kutoka Bara,na wachache sana kutoka pwani za mbali na Uarabuni!Sasa leo ukisema Bara na Visiwani sio nchi moja nitakushangaa sana!Walipokuja Wareno,baadaye Wajerumani na kisha Waingereza,ndipo Waarabu wa Oman wakaachiwa visiwa vya Zanzibar "wavimiliki wao" na Bara iendelee kutawaliwa na Wajerumani kisha Waingereza.Wazungu hawakupenda kuhusishwa na biashara ya Utumwa,wakawaachia Waarabu waifanye! Hiyo yote sasa ni HISTORIA!haitamsaidia mtu kurudi nyuma tulikotoka!tunatakiwa sasa tusonge mbele kwa manufaa ya pande zote mbili.Wanaojifanya hawautaki Muungano kwa kisingizio cha kuchoma Makanisa na kutoa kashfa kwa ndugu zao wa Bara,hawa sio wenzetu,Ni Mapandikizi na Wanatumika na Nguvu za Nje kutuharibia amani ya nchi yetu,wasipewe nafasi!Lets not pretend the Influx of Tourists in Zanzibar,"some Bogus,some Real",has had no devastating effect on the Unity of the Two Sides of the Union!Wapo ambao wangependa Muungano huo uvunjike kesho kama Fisi alivyosubiri Mkono wa Binadamu udondoke apate kuula!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2012

    Kuna tatizo gani Zanzibar ikiwa ni nchi ya kiislamu?! Ilhali asilimia kubwa ya wakaazi wake ni waislamu?! Muislamu anapodai haki yake, ndio hapo huitwa gaidi n.k,lakini asiyekuwa muislamu anapodai haki yake ni shujaa! (ref;Sudan Kusini)

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2012

    Haki ni nini wewe annonymous hapo juu? Lazima hao Wanzabibar wanaolete fujo wakalishwe na kufunzwa matokeo ya wanayoyataka maana hizi ni 'external forces' si ajabu hawajui walifanyalo hawa! twaishia kuwalaumu tu yakhe! Kwa nini lakini kusiwe na masikizano??? Sijui kama mwanifahamu hapa!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2012

    Hakuna Tatizo ikiwa ni nchi ya Kiislamu lakini iwe tayari kuweka Amani kwa wale waliokuwa sio waislam kama Magoa,Hindu,Christians na waliokuwa hawana dini.Kwa maana hivyo ndo walivyokuwa wakiishi kabla kuanza kuchomewa makanisa moto, au kwa kuwa hunywi pombe uchome Bar moto,au pia kuwaunguza watu na acid kwa kuwa ni wauza pombe.Kapigwa risasi mumewe na mkewe kamwagiwa acid.Hayo ndo watu wanapingana nayo na yanatokana na chuki mbaya ambazo wanafundishwa kwenye hizo skuli za kigaidi.Hiyo sio zanzibar inayojulika before.Anayetaka kunywa pombe na anywe hapo mtakapobadilisha katiba ya zanzibar na kuifanya islamic country kama saudia ndo muambie watu msinywe pombe unless muweke kepengele waliokuwa sio waislam wanaweza kunywa wakitaka lakini hiyo hamtowaruhusu kwa maana islam haina tolerence nazungumzia islam ya kisasa ambayo ni ya kigaidi inataka tuishi karne za zamani.Waislam wa zanzibar kama wanadai haki sio haki ya dini ni haki ya muungano ubadilishwe sio kuonyesha ukristo ndo adui.Wakristo wa zanzibar eti warudi makwao.Na kama hawana makwao? kisiwa chochote duniani wote ni watu wakuja kutoka sehemu nyengine.Zanzibar msicheze na damu mtajuta watizameni Pakistan au Nigerian wanauwana sio kwa uislam tu bali kwa usuni na ushia hayo ni madogo .Amani itawale Shughuli ya muungano ni vizuri kuishughulikia sio kutia ugaidi wa dini.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2012

    Ovyo maoni yenu !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Zanzibar ikiwa nchi ya kiislamu ndio lazima watu wote wawe waislamu? Egypt, mahali ambapo uislamu uko juu kabisa, bao una wakristo na wasioamini wa kutosha. Wewe una haki gani ya kumlazimisha mtu aamini katika unachamini? Nani amekupa mamlaka ya kuhukumu wengine? Wewe una usafi wa kiasi gani? Tufikirie maendeleo ndugu zangu, tuachane na mambo haya ya udini, kwani hayatatupeleka kokote

    Wasalaam

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...