Mhe. Dr. Limbu (kiongozi wa ujumbe wa Tanzania,kushoto), akiwa na Waziri wa Nishati wa Trinidad & Tobago, wakati ujumbe huo wa Tanzania ulipoitembelea Wizara ya Nishati kujifunza sera zinazohusu masuala ya gesi nchini Trinidad & Tobago.Ujumbe huo wa Tanzania wenye Waheshimiwa Wabunge na maafisa wa Serikali na TPDC, wapo katika ziara ya mafunzo nchini Trinidad & Tobago, kujifunza na kupata uzoefu wa nchi hiyo kuhusu masuala ya nishati ya gesi
Mhe. Dr. Limbu akimkabidhi zawadi, mmojawapo wa wenyeji wa ujumbe wa Tanzania katika ziara ya mafunzo nchini Trinidad & Tobago.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na Maafisa wa Serikali, katika picha ya pamoja kabla hawajaanza ziara katika maeneo muhimu yanayohusu gesi nchini Trinidad & Tobago.
Ujumbe wa Tanzania pamoja ujumbe wa Trinidad & Tobago katika picha ya pamoja. Wa tatu kulia ni Mhe. Dr. Limbu, ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe wa Tanzania.
Mitambo maalum ya gesi nchini Trinidad & Tobago.
Oooh no, wot are they learning there? Study tour hizo ni waste of public funds.
ReplyDeletekweli mdau hapo juu kwa nini wasiende sudan au nigeria na nchi nyingi tu afrika zinamafuta na bei rahisi ya gharama kuliko kutumia hela za maskini kutembea nchi za watu
ReplyDelete