Wadau wakigeuza kuhofia kukwama kwenye bonge la shimo na maji machafu karibu na kituo kidogo cha Polisi Mabatini maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam. Barabara hii na nyingine nyingi za pembeni zikifanyiwa ukarabati wa uhakika zitapunguza mno foleni ya magari kwenye barabara kuu. Mh Mbunge Iddi Azan na madiwani wa Kinondoni mpo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2012

    Hicho ni kipande kidogo tu, kwa wakazi wa maeneo haya kazi ipo maana lazima tupite hapo kila siku. Na hapo ni hatua chache tu kutoka kwa Mheshimiwa Spika29

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2012

    JAMANI MTAANI MSISUBIRI SERIKALI KAMATI SHIKAMANENI NAJUWA MNALIWA PESA ZENU WASOMI MTAANI WENGI NA WABUNIFU TENGENEZENI AU KAWASHITAKI WAHUSIKA WA BARABARA MPAKA MAHAKAMANI AU MBUNGE WENU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2012

    Wabonge na wadiwani wakiacha posho za kukaa (sitting allowance) zitatosha kutengeneza na kukarabati barabara zinazitumiwa na wapiga kura wao..... tukatae posho, tupige vita posho! tudai barabara, sisi walipa kodi ndio tunazidi kuumia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2012

    Mnatoa mchango wa harusi laki mbili kwenda juu! Mnashindwa kuchanga kutengeneza barabara mbovu inayoharibu magari yenu? Sisi mtaa wetu tulichanga tukatengeneza barabara yetu. Sasa ni mkeka

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2012

    Hebu acheni utani mtaua magari nendeni mkaibane kamati ya barabara ya s/mtaa hii ndo kazi yao lakini pia hapo pana tatizo la maji kama vile chemichemi chini au kuna bomba limepasuka wasilianeni na DAWASCO haya tumeshawatafunia mezeni.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2012

    Kijitonyama Mabatini!! haujui hata unapopita?

    ReplyDelete
  7. Mbeba BoxJune 11, 2012

    jamani, si mnasema bongo tambarare? Sasa kwa nini msimuwajibishe mwenyekiti wa mtaa? Kaza buti hapo, mnakuwa hamjui wajibu wenu kama walipa kodi, ebo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...