Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika Ukumbi wa mkutano, wakati walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano, wakati alipofika kuiwakilisha nchi katikaMkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Francis Malambugi.
 Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa. wakiwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992
Balozi Liberata Mulamula, akifurahia jambo baada ya kukutana na Wabunge wa Tanzania, (kushoto) ni Mbunge wa (wa pili kushoto) ni Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli, (wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, (katikati) ni Mkurugenzi wa mazingira, Ofisi ya Makamu wa rais, Dkt.Julius Ningu, katika Viwanja vya Kumbi za mikutano ya Rio+20, wakati walipofika kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2012

    Waheshimiwa wa Msafara wa Serikali ya Tanzania, huko mlipo ni 'Shamba kubwa' wapo ndugu zetu wengi tu hadi Vijijini huko msije mkakubali kupewa mafurushi na Wabongo wenzenu huko ya kuleta nyumbani Tanzania!

    Viwanja vingi vya ndege Duniani kuna Computer za ukaguzi !!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2012

    Siyo "" mkutano wa Mazingira Endelevu"". Ni Mkutano wa ""MAENDELEO ENDELEVU""....nINYI WATU WA vpo MNAWAZA MAZINGIRA KILA SIKU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2012

    Hehehehe

    Waheshimiwa msije mkadanganyika kukabihdiwa mizigo na mafurushi ya kuleta nyumbani Tanzania na wanaotokea sehemu za mashambani huko Brazil !!!

    Sio mtu anakuletea furushi amelizungushia 'rubber bands' na tape za kumwaga huku lina makaratasi ya jaribosi !

    Wanajua ninyi mnapitia VIP hakuna ukaguzi !

    Mwambie atumie DHL au FEDEX kuutuma Tanzania kwa kuwa utapitia Ulaya kwa Semina ya miezi miwili (2) ndio urejee Bongo hivyo mzigo utachelewa sana kufika!

    Je hapo si mnaona mtakuwa mmewaacha kwenye mataa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...