Kaka michuzi nashukuru kwa juhudi zako kufikisha huu ujumbe.niligundua watu wameuliza picha na wengine wanaona habari nusu nusu,sasa kama utaziweka tena labda itasaidia ili kuweza kupata ndugu wa marehemu,

kwa ufupi alifariki mwaka jana kwa ugonjwa wa sarakani ya tumbo,kama nikivyosema mwanzo ndugu hawakujulikana hivyo alifanyiwa mazishi ya kiserikali,jina kamiki ni Rehema kiyenga,nafanya uchunguzi wa hospitali na kazi kujua kama nitapata information zozote ambazo zitasaidia.

mawasiliano yangu ni abdulhabimana@hotmail.com na simu ni 6233993100.

shukrani kwa msaada tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2012

    Asante ndugu Abdu kwa moyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2012

    Bwana Abdul una uhakika na hizi habari ulizoandika? nashauri kwanza pata taarifa kamili kabla hujatuma tangazo hii taarifa sensitive sana, kama hauna uhakika na kilichotokea tafuta uhakika kwanza, lingine nalokushauri ni kufikisha habari hizi ubalozi wa Tanzania wanautaalamu wa kudeal na habari kama hizi, simu yao ni (202)939-6125 au (202)884-1080 sasa nimeelewa kwa nini dada yetu alikaa mbali na wabongo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2012

    Haya ndio matatizo yanayoweza kuwatokea watu wanaojokata wakiwa Majuu!

    Unakuta mtu anakaa nje hana mawasiliano na ndugu hata mmoja nyumbani akiogopa kuombwa misaada, angalia sasa inatokea mtu huyo Majuu anafariki hata ndugu hawana taarifa na matokeo yake anazikwa na Serikali ya Ughaibuni.

    Ndio mambo ambayo yanapelekea tunaynimwa sana visa na Balozi za nje sambamba na kuwekewa Sheria ngumu za Uhamiaji huko Majuu kwa kuwa mara zote tunawapa sana gharama ktk nchi zao.

    Kweli tutasma wakitunyima visa Sheria na kuweka Swao ni wabaya?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2012

    marehemu lazima atakuwa na simu i hope mnaweza kutrace number za kitanzania, ni mtazamo tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2012

    mungu aipumzishe pema roho yake peponi.
    Tuko wengi ambao tuko mbali na nyumbani (bongo), inatuuma kusikia au kuona mwenzetu anakufa ugenini, lakini yote ni mola anaepanga.

    Pumzika dada salama, sikukufahamu ila imeniuma. pole kwa ngudu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2012

    sasa toka mwanzo mbona hamkusema kama alishazikwa. all this time watu wanadhani mwili bado uko mochwari tuandae michango.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 28, 2012

    huyo dada alijilipua huko ati mkimbizi ndio maana akawa ana wakimbia watanzania wenzake ili wasimjue sana wangeweza kumchoma kwenye vyombo husika kaka ilivyokuwa kawaida ya watanzania huko ughaibuni. halafu kuna sampuli nyingi za watu kama hawa wao hujifanya wazungu sana zaidi ya wazungu wenyewe, ndio maana mambo kama hayo yanawakuta na hakuna mtanznia hata mmoja ana habari nao katika society zetu , anyway huo ni umauti utamfika kila mmoja wetu mungu amuweke peponi, kwa amani na usalama, AMEEN

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 28, 2012

    wabongo tunaongea sana ndo maana sometimes ni vizuri tu kujichimbia kwani kufa si kila mtu atakufa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...