Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu tukio la utekaji  na kujeruhi lililompata kiongozi migomo ya Madaktari,Dk. Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinywaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam hapo jana.Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kutokana na swala la kiusalama na kutoharibu upelelezi,kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutokea nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
 Waandishi wa habari wakimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.(Picha na Full Shangwe Blog)
KUNRADHI KWA PICHA HII: Dk. Steven Ulimboka akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana baada ya kutekwa na kupigwa vibaya usiku wa kuamkia leo na kuokotwa huko msitu wa pande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2012

    Pole sana.. I assume mgomo wa madakari unaendelea na huyu dk hatatibiwa... hoja!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2012

    Tanzania kweli nchi ya amani hata wananchi hatujitambui. Ina maana yeye Ulimboka hajijui kuwa anaweza kuwa anawindwa na wasiotaka kuendelea kuona akiongoza migomo? Hainiingii akilini kwake yeye kwenda sehemu za starehe bila ulinzi wake binafsi au wa umoja wa madaktari. Lazima tujitambue.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2012

    Tanzania iko chini ya laana si bure. Nani ataiondoa laana hiyo? tutarudi nyumbani kweli sisi wa ughaibuni kama mambo yenyewe ndo hivi!!! Nimeogopa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2012

    Masikini, pole sana.

    Sasa nani atamtibu wakati madaktari wamegoma? Maana wanasema mganga hajigangi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2012

    Hili sio tukio dogo. Hao watu waliomjeruhi wametumwa na watu wanaomfahamu na wamelipa kisasi. Mungu amsaidie dokta na pia awaangamize waliomjeruhi na walipanga!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2012

    This is bad, really bad, ni mbaya saana, who is behind this cruel act,hopefully things will be sorted out accordingly.
    Dr Gangwe Bitozi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2012

    Nampa pole nyingi Dr. Ulimboka na ninamuombea apone haraka. Pia kwa upande wa pili nadhani Dr. Ulimboka baada ya kupona atakuwa amepata japo chembe ya hisia kuhusu ni kwa kiasi gani wagonjwa wa ajali za barabarani wanavyokuwa katika kipindi kigumu cha kuwania uhai hivyo kuhitaji huduma ya haraka ya madaktari. Kwa bahati mbaya sana madaktari wetu wa Kitanzania hilo huwa hawalitambui, kwao zaidi ni maslahi mbele ingawa hayo maslahi wanayopata wala sio madogo kabisa kulinganisha na vipato vya Watanzania walio wengi.
    Upone haraka Dr.Ulimboka pengine asaa huenda wewe na wenzako mkaingia roho ya huruma kwa bibaadamu wenzenu wanaoteseka kwa maradhi mbali mbali yakiwemo ya majeraha kama uliyoyapata wewe regardless za cause of injury.

    ReplyDelete
  8. Nimejaribu kutafakari kwa kina,lakini naona sipati jibu sahihi juu ya tukio hili la kinyama.Hivi watanzania kweli tumefikia hatua hii....!?Mungu ampe nafuu na apone ndugu yetu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 28, 2012

    Mimi naomba huo mgomo wa madaktari uzidi kuendelea vinginevyo kama huyu Ulimboka Mwakingwe atatibiwa, basi hakutakuwa na lolote zaidi ya unafiki uliokithiri. Let's wait and see the end results!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 28, 2012

    Hiyo serikali ya bongo inaendeshwa kama MAFIA

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 28, 2012

    Niliwaambia na siku nyingine, nchi hiyo yule shetani aliye muua Kombe na mwenzake Kolimba bado anazungukazunguka,"Win their minds don't kill them, they don't understand this". kumteka kiongozi wa mgomo ndo kumaliza mgomo, ndo akili yao au ni nini, kama ndivyo ni akili ya kitoto.
    mimi nasema nipeni mimi nchi hiyo na nitaifanya kuwa paradiso Dunia nzima watakuja kutaka keki hiyo.
    Swaala dogo kama hili serikali inakubali kuingia katika aibu, kwanini?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 28, 2012

    Nivigumu kuelewa madai ya madakitari wa Tanzani , mpaka ufanye kazi katika mazingira ya mahospitali ya hapa kwetu Tanzania.Wananchi ndio tunaoteseka wakati wabunge na madiwani wanapeta.Haya ndio matunda ya serikali yetu ni ubabe ubabe kwa kwenda mbele, kweli mwenyeezi mungu atusaidie!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 28, 2012

    Hao madaktari wana ajenda ya kisiasa. Waziri wa
    Afya kawasihi sana hawasikii hivi wao ni supa Tanzanians? Ulimboka alikuwa na raha gani akitia ulanzi wakati Watanzania wengine wanaathirika na mgomo? Usikute kipigo hicho ni hasira za watu wanaoteseka na migomo ya madaktari. Lakini tunampa pole na tunataka apone halafu tuanze mjadala wa kweli, ni ajenda gani?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 28, 2012

    Binafsi nimefarijika sana na kipigo alichokipata Ulimboka huo ndo mshahara wa dhambi. Yeye amewaongoza wenzake kuacha roho za watu maskini wa nchi hii waliokuwa na uwezo wa kwenda kununua panadol wafe. Madaktari chini ya uratibu wake wameendelea kugoma kwa kudai maslahi yao, wakati wanajua kugoma kwako hawawakomoi Kikwete wa wala Pinda ila wanamkomoa Babu yangu mzaa Mama aliyefikia Bugando Hospitali wakati anasubili kufanyiwa upasuaji wa kibofu cha Mkojo, yeye akawahimiza wenzake wagome.

    Nimefarijika kwamba hawakumuua ila wamemuonesha kwamba, huo ndiyo MSHAHARA WA DHAMBI anazowaongoza wenzake kuzifanya za kuacha roho za wananchi maskini wakiteseka kwa kutaka kuongewezwa fedha.

    kuna namna nyingi za kudai maslahi yao kama ni sahihi lakini siyo kwa kuacha kumtibu Mgonjwa ambaye hana mbele wala nyuma.

    Kwa kweli sina huruma na Madaktari kabisa waliogoma sina huruma na huyu kikaragosi wao Ulimboka na wote waliogoma. Inakuwaje haki za Binadamu anapopigwa Ulimboka lakini hiyo haki ya Binadamu haisemwi pale roho za wasio kuwa na hatia zkitoka kwa UJINGA na UPUMBAVU na TAMAA na KUTOKUWA NA HURUMA kwa Madaktari waliosomeshwa kwa fedha za mlima tumbaku kule Tabora au Korosho kule Mtwara au Pamba kule mwanza n.k ambaye ushuru wa mazao yake ndiyo unaowasomesha Madaktari na wanakuwa na VIBURI vya kuacha kuwahudumia na wanakufa!!!

    Nimefurahi sana na kufarijika sasa acha akae Hospitali apewe huduma kisha avae nafsi ya mtanzania aliyevamiwa na majambazi akapigwa na kuwa kama yeye kisha afike Hospitali na hali aliyokuwa nayo yeye Ulimboka na akute yeye Ulimboka amewaongoza wenzake kugoma. Ndugu zake na yeye mwenyewe wangejisikiaje??

    Huduma zenyewe zinazotolewa na Madkatari wetu ni "MAGUMASHI MATUPU" huduma wanazotoa ni kama wako kwenye MGOMO kila siku.

    Nasema kwa hatua hii ya kupigwa kwa Ulimboka wala Serikali isilaumiwe wajilaumu wao wenyewe. Mimi nimeapa hata aje Daktari wa namna gani hataweza kumuoa Bint yangu au kuolewa na Mtoto wangu. watu gani wauaji hivi wanadhani wao ndiyo muhimu peke yao?

    Kila mtu katika Taifa hili ni muhimu.

    Nasema acha ulimboka apate kichapo ateseke Hospitali lakini asife akitoka hapo atakuwa na mbinu mbadala ya kudai maslahi yao badala ya kugoma na kusababisha roho za wapendwa wetu kutoka kwenye Mikono yao.\

    Nasema hawa jamaa ni wajinga sana, hebu jiulize Wakina Mama wangapi wanakufa kwenye mikono yao kwa kukosa kuwasaidia wakati wa kujifungua? tazama taarifa zao wanazoandika za Uongo kuhusu sababu za kifo, jiulize ni watu wangapi wanakufa kwa kukosa muda wa kumuita Daktari anayeongea na Bwana wake au mwanamke wake kwenye simu?

    Jiulize ni mara ngapi Daktari wanaua ndugu zetu kwa kufanya upasuaji kwa makosa lakini nani aliyeamdamana?

    Kuna mtoto alichomwa sindano akapooza mwili mzima waulize Hao Madaktari wanasemaje, hawajamtaja hata huyo mwenzao aliyefanya hayo kwa makusudi.

    Nasema acha apate kipigo na wengine wapate kipigo tena na tena

    TUMEWACHOKA MADAKTARI WETU UCHWARA

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 28, 2012

    POLE DR. WAFANYAKAZI WA MUHIMBILI TUMEONA UBAGUZI MLIONAO. NA MMJUA JINSI GANI MGONJWA WA KAWAIDA JE HAITAJI HUDUMA YA HARAKA KAMA HIYO TULIYOIONA KWA DR MWENZENU????????? NA KISA CHA KUMSHAMBULIA AFISA UWA USAMA NA JE ANGEPATA MAJERERAHA MNGEMPA HUDUMA???? HUO NI MCHEZO WA KUIGIZA NA ELIMU YENU.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 28, 2012

    Pole sana Dk Uli. Tmmtakie heri apone haraka. Pamoja na yaliyopo kwa muda wa sasa Tuelewe pia Dk pamoja na fani yake na hadhi yake katika jukuiya ya madokto... Bado yeye ni mtu wa kawaida kama siye wengine woote... Je haitawezekana ana vijimambo vyake huko mitaani! na yaliyompta yamempata tu kipindi hiki cha mizengwe ya madokto!! Tuliangalie kwa makini sana hili. Wabunge wanaosafiri kuelekea USA warejeshwe na fedha hiyo ichangie bajeti ya afya!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 28, 2012

    MIMI MTAZAMO WANGU NAONA HAPA SERIKALI HAIHUSIKI WATU WENGI SANA WANASIKITISHWA NA MGOMO WAMADAKITARI WENGINE WAMEPOTEZA NDUGU ZAO,KWA UZEMBE,MTU ANAFIKA NA MGONJWA WAKE HOSPITAL ALAFU WANASHINDWA KUMPOKEA WANAMTIZAMA TU UNAFIKIRI HUYO MTU ATAFURAHI?MBONA DOCTOR'S WENGI WANA HOSPITAL ZAO BINAFSI NA HATUJASIKIA WAMEGOMA?

    ReplyDelete
  18. Haji mnubiJune 28, 2012

    tunategemea dokta nae ataonja adha ya mgomo kama kweli waendesha mgomo wako fair

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 28, 2012

    Sikupenda kuchangia hili kuogopa kuwa mshabiki wa nisilolijua.
    Kwani kutekwa kujeruhiwa kwake kunahusikaje na mgomo wa madaktari!!
    Je wajuaje kama si beef zingine nje ya mgomo!!
    Madhila haya yalitokea baada ya kazi je kwanini yahusishwe na mgomo huo?
    Tumwobee Ndugu yetu huyu apone mambo ya kutibiwa na nani au wapi si kazi yako.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 28, 2012

    Dokta Ulimboka nakupa pole sana na Mungu akuponye mapema uweze kuungana na familia yako hususan na jamii kwa ujumla katika kuweza kuendeleza kudai haki,Kwakuwa ulimboka alikua ni kiungo katika kudai haki hii am,bayo serikali inatumia usalama wa taifa kuwaua au kuwanyamazisha wale wanaoongoza harakati,ninatoa rai kwa wanachi wote waungane na madaktari katika kudai haki yao.Dokta Ulimbopke apewe huduma stahili katika afya yake ili apone.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU MBARIKI DR ULIMBOKA,MUNGU IBARIKI AFRIKA

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 28, 2012

    We wa ughaibuni endelea tu kubeba maboksi,wala hatukuhitaji urudi na visenti vyako uchwara. Ila kumbuka kwenu ni kwenu hata kama pangoni

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 28, 2012

    NAMPA POLE DR. ULIMBOKA, LAKINI KWA UPANDE MWINGINE AC.
    HUKULIE KAMA YEYE NI RAIA WA KAWAIDA ASIYE DR. NA KAKUMBANA NA MASWHIBU HAYO HARAFU ANAFIKA HOSPITALI ANAAMBIWA WAMEGOMA WHAT NEXT
    HILI LIWE FUNDISHO KWA MADACTARI WOTE KWAMBA UHAI KWANZA MASLAHI BAADAYE.

    Hebu chukulia waalimu tanzania nzima wagome naowanawatoto wanasoma ni kitatokea!!

    WADAI HAKI ZAO LAKINI SI KUTUKOMOA TUNAOWALIPA HIYO MISHAHARA WANAYODAI BILA WAALIMU NAO WASINGEFIKA HAPO WALIO LAKINI MWALIMU HALIPWI KAMA WANAVYOLIPWA WAO. WAMENIKATISHA TAMAA MNO MWANZO TULIWAUNGA MKONO SASA IS TOO MUCH. HAYA NI MAONI YANGU JINSI MIMI NILIVYOJISIKIA

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 28, 2012

    Nani aliye nyuma ya jambo hili? Naomba majibu. Dr. ulimboka nakuombea upone haraka uje kutekeleza majukumu yako kadri ya mapenzi ya MUNGU.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 28, 2012

    COMMENT NYINGI ZINAONYESHA NI KWA JINSI GANI WATANZANIA WALIO WENGI HAWAFURAHISHWI NA MGOMO WA MADAKTARI HIVYO HATA HURUMA KWA HUYU DKT. ULIMBOKA INAKOSEKANA KUTOKANA NA KILICHOMSIBU.
    SERIKALI YETU SIO PERFECT KATIKA KUTIMIZA AHADI ZAKE, LAKINI MADAKTARI MKO WRONG KUGOMA KWA SABABU YA HILO. WAKO WENGI WENYE MADAI YA MIAKA MINGI NA BADO HAWAPATA HAKI ZAO,NINIY KWA KUWA MNA DHAMANA YA AFYA YA WATU NDO MJIONE "THE UNTOUCHABLES?". NI ULIMBUKENI USIOVUMILIKA, NA MKIDHANI KUWA HAYA YASEMWAYO HAYANA MAANA, ENDELEENI KUGOMA TU, KWA UBINAFSI WENU NA WATANZANIA WATAENDELEA KUTESEKA. HAKIKA MBELE ZA MUNGU MTAPATA HAKI YENU DUNIANI NA SIKU YA HUKUMU

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 28, 2012

    MADAKTARI ENDELEENI KUGOMA TENA KWA SANA KWA NYINYI MTOHANGAIKA NA WAGONJWA HAMSIKIZWI MBONA WABUNGE WANOLALA TU KWENYE VITI WANAKULA HELA ZA BURE MI NAONA MGOMO NI SAWA TU NA WAKULAUMIWA KWENYE HILI TUKIO NI SERIKALI KWANI NI MPANGO MZIMA WAMEFANYA WAKUMZIMA ULIMBOKA LAKINI MUNGU HAJAPENDA

    ReplyDelete
  26. Kwani hivi ni watanzania wangapi wanavamiwa na vibaka na kupigwa kila siku?
    Huyu Ulimboka si binadamu kama walivyo wengine?

    Ninachoamini Yeye kajichanganya tu na mambo yake mwenyewe wajanja wakamfanyizia wakampa kipondo That's all!
    Siyo eti mambo ya mgomo kwani yeye nani? yeye si msemaji tu wa kundi la hao wahuni kama yeye?

    Hebu jaribuni kufikiri jamani Ooh sijui serikali inahusika Ok prove if that what you are thinking is true! Those are mere assumptions.

    Mpeni pole huyo Ulimboka wenu na tunamwombea apone asije akafa mkampa umaarufu asiostahili bure...

    CHIAO!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 28, 2012

    KWA MFANO DR KAMA USINGETAMBULIKA KAMA NI DR ULIMBOKA UNGEPELEKWA HOSPTALI NYINGINE WAKATI WA MGOMO.NADHANI BAADA YA HAPO UNGEJUA MADHARA YA MGOMO.WATU WENGI WALIPOTEZA MAISHA KWA WEW KUOGOZA MGOMO BILA KIJALI UBINADAMU. KAMA MSOMI NA UNA WITO UNGETOA MAAMUZI MAZURI KUCHAGUA BAADHI YENU MKAONGEE NA SERIKALI NA WENGINE WAKAENDELEA NA NA KAZI. TUMEKOSA IMANI NA HUDUMA ZENU. POLE NA YALIYOKUSIBU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...