Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa, NHC, kutoka kwa Ofisa Masoko wa Shirika hilo, Mariam Ndabagenda, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expo, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo, William Genya (wa pili kulia) ni Ofisa Mauzo mwandamizi wa Shirika hilo, Emmanuel Lyimo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utengenezaji wa Viage vya ujenzi wa Nyumba kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kampuni ya Insignia Ltd, Obed Machoka, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expo, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba 220 zinazojengwa eneo la Jangwani Beach, jijini Dar es Salaam, zinazotarajia kutumia jumla ya dola milioni 208, kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Global Land Solutions Ltd, Murtaza Adamjee, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expo, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu matumizi ya Nyaya za Africab kutoka kwa Ofisa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Khuzema Janowalla, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-OMR 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2012

    Siamini kwamba nyumba 220 zinaweza kujengwa kwa jumla ya shilingi milioni 280!! Kuna kosa limetokea mahala?
    Merinyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2012

    Ni kweli Merinyo, labda ni dola Milioni 208 na siyo shilingi kama inavyosomeka. Michuzi na timu yako rekebisha hilo kosa.
    Robert.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2012

    Nadhani mdau wa pili (Robert)umetumia diplomasia ya kutokuulalamikia ujinga wa huyo mdau wa mwanzo ambae kaona SHILINGI MILIONI 280 badala dola 208 zilizoonekana na kila mmoja aliyesoma habari hii.Ni vizuri tunaposoma habari TUZIZINGATIE kabla hatujatoa comments

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...