Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar
Wanahabari wakihangaika kupata picha ya Dk. Steven Ulimboka alieinginzwa kwenye gari hiyo tayari kwa kupelekwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiisukuma gari iliyokuwa imempaki Dk. Stevan Ulimboka.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2012

    Jamani bado nchi hii ina mambo haya hadi leo?
    Na hao waliotumwa wamuadhibu wako wapi, watuambia hao vigogo waliowatuma na waliwalipa kiasi gani?
    Demokrasia ipo wapi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2012

    Michuzi hebu tueleze uzuri habari hii kwa sie ambao ndio kwanza tunasoma habari hii hapa. Unasema amepatwa na mkasa huu kwenye msitu wa mabwepande usiku wa kuamkia leo. Hukusema kuwa alikuwa anafanya nini katika msitu huu tena usiku hata kufika kutekwa nyara huko? Hivyo ndivyo ilivyokuwa au umekosea kiuandishi kidogo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2012

    sasa ndio tungependa tuone huo mgomo ndio maana tuna sema madaktali ni wa baguzi wala hamna lolote inaleta hisia kuwa mnashinikizwa kisiasa rungu la serikali lipo litawagonga tu
    mdau wa tanzania

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2012

    MNATUAMBIA TURUDI NYUMBANI TUJE KULETA MAENDELEO..TUTAKUJA KUSEMA MBOVU MTUTIE RISASI BUREEE

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2012

    hawa madaktari bora wakasomee FPA maana mchezo wao wa kuigiza umepasi. Wanacheza na maisha ya mtu namna hii,

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2012

    Haya wewe mdau kalia huo uchumi ulionao huko huko ughaibuni na ufie huko huko!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 28, 2012

    MI nadhani si mda wa kuwakandia madaktari kiasi chote hiki, suala kwa nini wagome? kiko kilowagomesha nadhani! madaktari,walimu,viongozi, ni watu muhimu katika jamii yoyote duniani lakini labda wanahisi wanadharauliwa au mishahara yao haitoshelezi ndo mana yanatokea yote hayo, au nyinyi mnahisi kuwa wanalalamika bure awo madaktari? kaeni nao chini wahusika muwasikilize vilio vyao, ayo ni mawazo tu msinijengee chuki,

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 28, 2012

    Jamani huyu mtu katekwa nyara Kinondoni alikuwa anakunywa labda Malta ,watu watano wakaja wakamkamata -labda kiujanja ujanja na kutokomea naye Mabwebande,huko sasa ndo huo mkongoto , mimi katika kuona kwangu, hawa watu wote wanajuana,ni madakitali wenzake au ma VIP fulani-hii jamani siyo bure bure tu, wamemfuatilia kwa muda mrefu. Lazima ,anakitu anakijua. halafu wewe unayesema kunya -kama hutaki kurudi si ubaki tu huko-kwani lazima ??? wewe fanya tu safari za western union, tuma hizo $ 50 kila unapojiweza basi, ila kumbuka ukitimiza miaka 55 mgongo tena haunyanyui mabox inavyotakiwa , usitulilie .

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 28, 2012

    Hawa madaktari walisomeshwa kwa kodi ya wananchi, kugoma si suluhisho,Watu wengi wanapoteza maisha kwasababu ya tamaa ya fedha. kwa upande mwingine naona sawa kwa Ulimboka kupata kichapo...Enzi za mwalimu Watu Hawa ilikuwa in kifungo cha maisha...mkuki kwa nguruwe... Kama madaktari wangegoma kumtibu Ulimboka nafikiri Angetia akili

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 28, 2012

    Huyo mdau aliezungumzia maswala ya kurudi bongo yahausiana vipi na hii ajali? Mbona bichwa kuubwa ubongo wa mende?? Yawezekana ulipelekwa na serikali hii hii huko ukasome, leo hii unaona kila ulichokiacha nyuma ushenzi...na kama hukulelewa na Tanzania kusoma nk ungefika huko? Acha zarau bwanaaa!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 28, 2012

    Binafsi nimefarijika sana na kipigo alichokipata Ulimboka huo ndo mshahara wa dhambi. Yeye amewaongoza wenzake kuacha roho za watu maskini wa nchi hii waliokuwa na uwezo wa kwenda kununua panadol wafe. Madaktari chini ya uratibu wake wameendelea kugoma kwa kudai maslahi yao, wakati wanajua kugoma kwako hawawakomoi Kikwete wa wala Pinda ila wanamkomoa Babu yangu mzaa Mama aliyefikia Bugando Hospitali wakati anasubili kufanyiwa upasuaji wa kibofu cha Mkojo, yeye akawahimiza wenzake wagome.

    Nimefarijika kwamba hawakumuua ila wamemuonesha kwamba, huo ndiyo MSHAHARA WA DHAMBI anazowaongoza wenzake kuzifanya za kuacha roho za wananchi maskini wakiteseka kwa kutaka kuongewezwa fedha.

    kuna namna nyingi za kudai maslahi yao kama ni sahihi lakini siyo kwa kuacha kumtibu Mgonjwa ambaye hana mbele wala nyuma.

    Kwa kweli sina huruma na Madaktari kabisa waliogoma sina huruma na huyu kikaragosi wao Ulimboka na wote waliogoma. Inakuwaje haki za Binadamu anapopigwa Ulimboka lakini hiyo haki ya Binadamu haisemwi pale roho za wasio kuwa na hatia zkitoka kwa UJINGA na UPUMBAVU na TAMAA na KUTOKUWA NA HURUMA kwa Madaktari waliosomeshwa kwa fedha za mlima tumbaku kule Tabora au Korosho kule Mtwara au Pamba kule mwanza n.k ambaye ushuru wa mazao yake ndiyo unaowasomesha Madaktari na wanakuwa na VIBURI vya kuacha kuwahudumia na wanakufa!!!

    Nimefurahi sana na kufarijika sasa acha akae Hospitali apewe huduma kisha avae nafsi ya mtanzania aliyevamiwa na majambazi akapigwa na kuwa kama yeye kisha afike Hospitali na hali aliyokuwa nayo yeye Ulimboka na akute yeye Ulimboka amewaongoza wenzake kugoma. Ndugu zake na yeye mwenyewe wangejisikiaje??

    Huduma zenyewe zinazotolewa na Madkatari wetu ni "MAGUMASHI MATUPU" huduma wanazotoa ni kama wako kwenye MGOMO kila siku.

    Nasema kwa hatua hii ya kupigwa kwa Ulimboka wala Serikali isilaumiwe wajilaumu wao wenyewe. Mimi nimeapa hata aje Daktari wa namna gani hataweza kumuoa Bint yangu au kuolewa na Mtoto wangu. watu gani wauaji hivi wanadhani wao ndiyo muhimu peke yao?

    Kila mtu katika Taifa hili ni muhimu.

    Nasema acha ulimboka apate kichapo ateseke Hospitali lakini asife akitoka hapo atakuwa na mbinu mbadala ya kudai maslahi yao badala ya kugoma na kusababisha roho za wapendwa wetu kutoka kwenye Mikono yao.\

    Nasema hawa jamaa ni wajinga sana, hebu jiulize Wakina Mama wangapi wanakufa kwenye mikono yao kwa kukosa kuwasaidia wakati wa kujifungua? tazama taarifa zao wanazoandika za Uongo kuhusu sababu za kifo, jiulize ni watu wangapi wanakufa kwa kukosa muda wa kumuita Daktari anayeongea na Bwana wake au mwanamke wake kwenye simu?

    Jiulize ni mara ngapi Daktari wanaua ndugu zetu kwa kufanya upasuaji kwa makosa lakini nani aliyeamdamana?

    Kuna mtoto alichomwa sindano akapooza mwili mzima waulize Hao Madaktari wanasemaje, hawajamtaja hata huyo mwenzao aliyefanya hayo kwa makusudi.

    Nasema acha apate kipigo na wengine wapate kipigo tena na tena

    TUMEWACHOKA MADAKTARI WETU UCHWARA

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 28, 2012

    haya sasa tuone huo mgomo ni kwa wananchi wa kawaida ama ni pia kwa daktari mwenzao? Naomba waendeleze mgomo na daktari mwenzao wasimtibu.....mgomo mgomo kote kote....Mimi sifurahii kujeruhiwa kwa huyu daktari isipokuwa hawa madaktari wanacheza sana na maisha ya watu hata kama ni kudai haki zenu basi hata huruma hamna? siamini kwamba huu mgomo wa madakatari hauna chembe chembe za kisiasa nahisi kuna shinikizo tu ila ni nani ama ni kundi gani haijulikani....

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 28, 2012

    Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu! Mgomo uko kwa wale wasio madaktari lakini kwa daktari mwenzenu hapana, ubaguzi huo! Sina maana kwamba nafurahia kitendo cha kupigwa Dkt Ulimboka, hapana, kinachonisikitisha ni huo mgomo wenyewe ulivyo. Nadhani asingekuwa daktari mwenzenu (raia wa kawaida)asingepata matibabu kama hayo!! Mwenyezi Mungu amuafu Ulimboka.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 28, 2012

    Pole kwa Dr Ulimboka nami nasema kama madaktari wako kwenye mgomo je Ulimboka naye si mgonjwa? sasa kwa nini wamhudumie ili hali wagonjwa wengine mnakataa kuwahudumia? simamieni msimamo wenu ila mjue mnawaumiza hata wasiohusika katika madai yenu

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 28, 2012

    Ukweli utajulikana tu, mungu amsaidie Daktari apone
    Kama kwa kudai haki mtu anapaswa kuadhiwa hivi tutakuja ona
    ili tujue na tuhakiki kuwa serikali haijahusika na hili, kama wanavyoweza kuwatafuta watuhumiwa wa makosa mengine, kwa jitahada nzuri, basi jitihada hizo zitumike katika kuwatafuta waliohusika na hili
    mgogo wa madaktari hauhitaji mbwembe za kisiasa wala Mabavu, inahitaki hekima na busara, madai yao ni ya msingi sana, sasa hivi sio tena mgogoro wa serikali na madaktari, bali hata sisi walala hoi tunahusika. mkitaka kujua idara ya afya tanzania badi ina changamoto kubwa mno, njooni vijijini msikae tu huko kwenye magorofa, njooni, vitendea kazi hakuna, mtu anakufa unamuaangalia kwa kukosa huduma bora, na inaudhi zaidi kwamba wanaotaabika na haya yote ni walala hoi, viongozi wetu wakiumwa safari India, kwa nini fedha hizi zisiboreshe hospitali zetu? hili halihitaji kwenye chuo kikuu kulifahamu, Tumechoka jamani

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 28, 2012

    Safari bado ni ndefu sana....Kwa mwendo huu aaahhh sijui. Mwendo wa punda mpaka lini?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 28, 2012

    MADAKTARI NAWAULIZA SWALI KWA KILE TULICHOKIONA JANA INA MAANA UHAI WA DOKTA ULIMBOKA NI MUHIMU KULIKO WATANZANIA WENGINE WALIO MAHUTUTI HAPO MOI NA MUHIMBILI.!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 28, 2012

    Dk Uli Pole sana Ila utuambie ukweli Janga hili linamahusiano gani na mgomo wenu! Else tujue tu ni ajali binafsi kwa maswala binafsi na kamwe wenzio wasilihusishe na mgogoro wenu na serikali kwa gharama ya afya na uhai wetu..! Waweza hebu wajibika pls!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 28, 2012

    Those who receive this privilege therefore, have a duty to repay the sacrifice which others have made. They are like the man who has been given all the food available in a starving village in order that he might have strength to bring supplies back from a distant place. If he takes this food and does not bring help to his brothers, he is a traitor. Similarly, if any of the young men and women who are given an education by the people of this republic adopt attitudes of superiority, or fail to use their knowledge to help the development of this country, then they are betraying our union. NANI ANIAMBIE HAYA MANENO ALISEMA NANI? NA YANA REFLECT VIPI SITUATION YA SASA

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 28, 2012

    Hainiingii akilini naposikia wengine wakisema serikali inahusika kwenye mkasa huu kwa kuwa ndiye kiongozi wa mgomo. je? wale wenye wagonjwa wao muhimbili ambao hawana uwezo wa kuwapeleka wagonjwa wao private, na wanaona huyo jamaa anashinikiza ndugu zao wasipatiwe matibabu jee?, Hapa waTZ mnatakiwa kuliangalia hili swala kwa kina kabla ya kuyatolea maamuzi ya haraka haraka bila kuingiza akilini.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 28, 2012

    Yaani mtu unategemea madaktari wagome kumhudumia daktari mwenzao? Hayo ni mawazo ya kitoto kabisa na hayasaidii lolote. Halafu watu tunawashambulia madaktari wee kwa nini hatuibani serikali ikatekeleza yale ambayo walikubaliana? Leo ni kwa madaktari kesho itakuwa kwako. Serikali gani duniani haioni umuhimu wa kutimiza makubaliano? Je utaiamini vipi kwa mengine pia? Tunahitaji serikali inayowajibika,si kwa madaktari tu bali kwa watu wote:walimu,wakulima,polisi nk.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 28, 2012

    Kwa kweli maendeleo Tz yatachelewa sana. Watu wanadai haki iloibwa tangu uhuru na wenye mamlaka ninyi wengine mnawaona kama hawana akili. Ni nani asiyejua kuna pesa bilioni 300 zilizofichwa nje ya nchi na wajanja hawa? Nani asiyejua kuna trilioni 3.1 kule SA za mjanja mmoja? Serikali ingekuwa inasimamia vizuri rasilimali zake kungekuwa na foleni Dar? Kungekuwa na huduma mbovu mahospitalini? Kungekuwa na huduma mbovu katika elimu?

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 28, 2012

    Madakrari wabaguzi sana. Je wananchi wote tusomeeee udakrari au????
    watalindwa na nani, yaani ana roho ngumu kama paka hadi mchana yuko hai tuuuuu naona alikunywa sana dawa. nao hao walikosea Paka ni kumpiga kichwa tuuuuuuuu.

    Yaani nimepata faraja angalau hao walofanya hivyo naona na wao waliwapoteza watu mhhimu kwao sana inauma mana jamaa zangu wengi wamepotea mgomo wa kwanza na huu jamani duuuuu

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 28, 2012

    huruma, ila nimeipenda sana hii ya kupigwa huyu bwana, hapo inabidi Ulimboka avae viatu vya wale ambao hawana pesa za kutibiwa private, umpata ajili then unafika hosp kama yeye hivyo alivyofikishwa then unakuta hakuna huduma, what next? ni kifo....

    By the way,am very much convinced kuwa this is a set up, na imefanywa na madaktari wenzake,na Ulimboka analifahamu hili,ila sina hakika kama ataja sema ukweli..

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 28, 2012

    ukijaribu kuyatazama mawazo ya wachangiaji hpo juu utajua kua taifa hili la tanzania linatatizo kubwa la kufukiria..kma hvi ndvyo wananchi wanaojiita wasomi wanafikiri hvii basii nchii hii itakua maskini miaka miatatu ijayooo.......matatzo ya madkatari na sector nyngne za utumishi wa umma inadhihilisha UZAIFU WA SERIKALI YTU aliyosema Mh mnyika...

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 28, 2012

    mnyika nae si boya tu ambae hana akili hata kiduchu....fanya kazi dai chako sio kugoma goma tu kila siku... we mkeo akiwa hakupi mchezo utagoma?? hizi ni akili na tabia za kiboya ambazo zinaturudisha nyuma kila siku.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...