Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihada zetu tumefanikiwa kumsafirisha marehemu ASHA HASSAN KALLENGA (pichani) akazikwe nyumbani.Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Dar es salaam kesho Juni 18, 2012 kwa ndege ya Turkish airlines (TK0603)
Pamoja na hali ngumu inayoendelea kutukabili watanzania tunaoishi Ugiriki ugumu huo haukuweza kutuzuwia kutekeleza ada na mazowea ya kumsafirisha mtanzania yeyote anaefariki hapa.
Jumuiya ya watanzania Ugiriki, inawashukuru wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kumsafirisha mwenzetu.
Tunamuomba Allah amlaze Marehemu mahala pema peponi.
(Amin)
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN
Kayu Ligopora
Katibu Mkuu
Jumuiya ya watanzania ugiriki
InnaLLaha Waina Illaihirajiuna.
ReplyDeleteMungu amsamehe marehemu dhambi zake zote na amjaalie mahali pema kwa mapumziko ya milele. Shukrani zisizo kifani kwa Watanzania waishio Ugiriki jitahada na utamaduni mliojenga wa kurudisha ndugu zenu nyumbani ni mfano wa kuigwa kwa wengine waishio njee ya nchi. Kwakweli nyinyi ni wazalendo, mola akuzidishieni umoja wenu
Mungu awabariki na tunaiombea ugiriki itoke kwenye financial crisis kwa faida ya dunia mzima.
ReplyDeleteYaani mie ndio nawapendea hapo watu wa ugiriki, yao wanayamaliza wenyewe. Lakini sio sie wa bibi wala wa baba likitokea tu basi tunawakamua hadi waliopo nyumbani! Mungu awazidishie ukarimu na moyo wa kujali.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awajalie moyo wa subira wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mola amlaze mahala pema peponi na nyie wote wa ugiriki mliojitahidi kuchanga bila kuomba msaada tutani Mola atawazidishieni Amin
ReplyDeleteUkiwacha yote,Huyu Marehemu alikua ni mtu mmoja mwenye roho nzuri sana tena sana,na ni mtu mwenye Bidii sana katika community ya Watanzania,Alikua akipigania kwa nguvu zote kama mtu ambae analipwa na alikua akijitolea kusafiri kushuhulikia matatizo mfano ya Passport na mengine.Mungu amlaze mahala pema Peponi.Ameen
ReplyDeleteMwenyezi Mungu aipokee na kuilaza roho ya marehemu Asha.H.Kallenga mahali pema peponi,nimestushwa sana na kifo chake marehemu alikua mwanafunzi mwenzangu Bunge Primary School mid 70's pamoja na mdogo wake Said.H.Kallenga ambae tulikua darasa moja kwa miaka mingi tulipoteana mpaka hivi nilipoliona tangazo hili la masikitiko.Shukurani nyingi kwa watanzania wenzetu waishio Greece kwa ushirikiano mkubwa mliokua nao kwa kuwezesha mwili wa dada Asha kurudi nyumbani kwa mazishi,nawapa pole wafiwa mwenyezi Mungu awape nguvu na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteG.Mwaluli
Milton Keynes
Pongezi sana Watanzania mliopo Ugiriki kwa moyo wenu pamoja na maisha kuwa magumu lakini bado mnaendelea na upendo wenu Mungu awazidishie na wengine waige mfano wa wenzetu wanaoishi Ugiriki,ni mfano wa kuigwa na kwa kweli wanastahili sifa
ReplyDeletePoleni sana wafiwa. Mola amlaze mahala pema peponi. Amin.
ReplyDelete