Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihada zetu tumefanikiwa kumsafirisha marehemu ASHA HASSAN KALLENGA  (pichani) akazikwe nyumbani.Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili   Dar es salaam kesho Juni 18, 2012 kwa ndege ya Turkish airlines (TK0603)

  Pamoja na hali ngumu inayoendelea kutukabili watanzania tunaoishi Ugiriki ugumu huo haukuweza kutuzuwia kutekeleza ada na mazowea ya kumsafirisha mtanzania yeyote anaefariki hapa.

Jumuiya ya watanzania Ugiriki, inawashukuru wale wote walioshiriki kwa hali na mali katika kumsafirisha mwenzetu.
  
Tunamuomba  Allah amlaze Marehemu mahala pema peponi.
(Amin)
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu Ligopora
Katibu Mkuu 
Jumuiya ya watanzania ugiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. InnaLLaha Waina Illaihirajiuna.
    Mungu amsamehe marehemu dhambi zake zote na amjaalie mahali pema kwa mapumziko ya milele. Shukrani zisizo kifani kwa Watanzania waishio Ugiriki jitahada na utamaduni mliojenga wa kurudisha ndugu zenu nyumbani ni mfano wa kuigwa kwa wengine waishio njee ya nchi. Kwakweli nyinyi ni wazalendo, mola akuzidishieni umoja wenu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2012

    Mungu awabariki na tunaiombea ugiriki itoke kwenye financial crisis kwa faida ya dunia mzima.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2012

    Yaani mie ndio nawapendea hapo watu wa ugiriki, yao wanayamaliza wenyewe. Lakini sio sie wa bibi wala wa baba likitokea tu basi tunawakamua hadi waliopo nyumbani! Mungu awazidishie ukarimu na moyo wa kujali.
    Mwenyezi Mungu awajalie moyo wa subira wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2012

    Mola amlaze mahala pema peponi na nyie wote wa ugiriki mliojitahidi kuchanga bila kuomba msaada tutani Mola atawazidishieni Amin

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2012

    Ukiwacha yote,Huyu Marehemu alikua ni mtu mmoja mwenye roho nzuri sana tena sana,na ni mtu mwenye Bidii sana katika community ya Watanzania,Alikua akipigania kwa nguvu zote kama mtu ambae analipwa na alikua akijitolea kusafiri kushuhulikia matatizo mfano ya Passport na mengine.Mungu amlaze mahala pema Peponi.Ameen

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2012

    Mwenyezi Mungu aipokee na kuilaza roho ya marehemu Asha.H.Kallenga mahali pema peponi,nimestushwa sana na kifo chake marehemu alikua mwanafunzi mwenzangu Bunge Primary School mid 70's pamoja na mdogo wake Said.H.Kallenga ambae tulikua darasa moja kwa miaka mingi tulipoteana mpaka hivi nilipoliona tangazo hili la masikitiko.Shukurani nyingi kwa watanzania wenzetu waishio Greece kwa ushirikiano mkubwa mliokua nao kwa kuwezesha mwili wa dada Asha kurudi nyumbani kwa mazishi,nawapa pole wafiwa mwenyezi Mungu awape nguvu na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu.
    G.Mwaluli
    Milton Keynes

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2012

    Pongezi sana Watanzania mliopo Ugiriki kwa moyo wenu pamoja na maisha kuwa magumu lakini bado mnaendelea na upendo wenu Mungu awazidishie na wengine waige mfano wa wenzetu wanaoishi Ugiriki,ni mfano wa kuigwa na kwa kweli wanastahili sifa

    ReplyDelete
  8. Poleni sana wafiwa. Mola amlaze mahala pema peponi. Amin.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...