Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) chini ya mpango wake wa WESTADI linatoa tamko kwamba litagharimia safari za kusafirisha mwili wa Ndg Domitian Rutahimirwa aliyefariki tarehe 18 katika Hospitali ya George Washington University, USA.

Kwa kuwa Marehemu alishajiandikisha katika Mpango wa WESTADI hivyo ni jukumu la Shirika chini ya mpango wake wa WESTADI kusafirisha mwili na kulipia gharama ya tiketi ya kwenda na kurudi kwa mwanafamilia mmoja atayesindikiza mwili.

Tayari Uongozi wa WESTADI umeshafanya mawasiliano na Familia ya marehemu na utaratibu wa kulipia gharama hizo unaendelea.

Menejementi ya NSSF inatoa salam za rambirambi kwa wafiwa, ndugu na jamaa.

WESTADI NDIO TEGEMEO LA WANADIASPORA, JIUNGE SASA..

Kujiunga na maelezo zaidi ingia hapa www.nssf.or.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...