Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameitumia  familia ya Mzee Bob N. Makani  (pichani) salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mzee huyo kilichotokea usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Aga Khan ya Dar es Salaam.
Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amesema kuwa amehuzunishwa na kusikitishwa na habari za kifo cha Mzee Makani ambaye alilitumikia taifa la Tanzania kwa uadilifu na uzalendo katika nafasi mbali mbali alizozishikilia katika maisha yake ikiwamo ile ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
“Nimepokea kwa huzuni na masikitiko habari za kifo cha Mzee Makani ambaye nimejulishwa kuwa aliaga dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Aga Khan mjini Dar es Salaam. Nilimfahamu Mzee Makani vizuri wakati wa uhai wake. Alikuwa Mzalendo na mtumishi mwadilifu wa umma, sifa ambazo alizithibitisha katika nafasi zote alizozishikilia katika utumishi wa umma ama kwenye siasa.”
“Nawatumieni salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu, nikiwajulisheni kuwa niko nanyi katika msiba huu mkubwa ambao umewaondolea mpendwa wenu, baba yenu, babu yenu na mhimili wa familia yenu. Napenda mjue kuwa msiba wenu ni msiba wangu. Naelewa machungu yenu katika kipindi hiki, lakini nawaombeeni subira na uvumilivu kwa sababu yote ni mapenzi ya Mungu. Naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze pema peponi roho ya Marehemu Makani. Amen.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2012

    Kebby, Mohamed na Ally poleni sana kwa msiba wa Baba yenu. Mjaliwe nguvu za kuweza kumlaza pema. Nilimjua kwa uungwana wake. Roho ya marehemu ipumzike kwa amani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...