Maisha yana majaribu.Kila siku ina changamoto yake.Labda hivyo ndivyo tunavyoweza kusema kwa kusoma,kusikia na kuona yale ambayo Vicent 'Ray' Kigosi amepitia kwa mwaka huu tu wa 2012.Bila shaka ni mengi.Na mengi zaidi.Wiki iliyopita,Jumatatu ile,ndiye aliyeketi na Salama Jabir katika Mkasi na kusema yaliyo moyoni mwake.
Haya hapa mahojiano kamili ambayo kama yalivyo mengine,yote huanzia pale Amaya Beauty Salon & Spa,katikakati ya jiji la Dar-es-salaam(ndani ya kampaundi ya Air Tanzania Corporation-ATC) katika makutano ya mitaa ya Garden na Ohio.Hebu usijivunge,wapigie( 0753 26 29 24, 078426 29 24 and 0716 60 44 95),watembelee na wewe upendeze kama wenzako wajanja wa mjini.WORD!



Read more: BongoCelebrity

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2012

    Ray nimependa sana ulivyozungumza kuhusu maisha yako na umefafanua vizuri kuhusu uvumi wa ugomvi wako wewe na marehemu Kanumba.Una kipaji kaka angu
    Ray nimekuonea huruma sana wakati ukizungumza huwo ugomvi wenu,,umekuwa muwazi,,na mtu yeyote mwenye akili atakubaliana na wewe kuwa kweli nyie mlikuwa marafiki wa kweli.Na ugomvi kwa marafiki kama nyie mlivyokuwa ni kitu cha kawaida.Bila kugombana urafiki haunogi.
    Kuhusu watu kukuandama na kifo cha Kanumba,ukumbuke kwamba hata wewe ungekuwa ndo umetangulia nae Kanumba angeambiwa umemuuwa Ray...Hata hivyo kazi ya Mungu haina makosa,,na nyie wote mmepita katika vitimbi kwa kusemwa semwa,,na yeye pia marehemu alisakamwa sana na watu eti hajui kizungu pia.Huwezi kuwazuia walimwangu kukusema especially watu kama nyie mnaojulikana,kwani kuna mengi mabaya wanafanya watu wasiofamous lakini hayatangazwi na mengine hayasikiki.Ukisikiliza maneno ya watu hutofanya lolote.Pia ulitakiwa mtu wa kukuencourage kwa kipindi hicho ili kipite uanze kuganga mengine
    Kuhusu ulivyoizungumzia serikali kujali mtu pale anapokufa,ni kweli.Maana hiyo michango uliyotolewa kwa Kanumba kama angepewa katika uhai wake na wasanii wengine pia,basi nyie wasanii wa Bongo mngekuwa mbali,,Mtu unashangaa watu wanavyokusanyika kwa ajili ya kifo cha mtu,utafikiri kinamtokea yeye tu wao laa hasha hakitawatokea.
    Kuhusu ulivyoweka picha za marehemu katika blog yako,,mimi nilijuwa ulikuwa na uchungu wa namna gani nakutaka kujaribu kumuenzi rafiki yako kwa njia hivyo.Lakini watu wakakuelewa vibaya masikini,,mpaka ukashindwa wewe mwanyewe kujuwa msimamo wako..POLE SANA RAY!
    Salama napenda kweli unavyoulizaga maswali,,Ila sasa naona kidogo unaanza kuvuka kiwango.Wewe mambo ya umesexy mara ngapi inahusu nini hapo..kimaadili ya kitanzania,,kiafrika na hata dini haipo,,Kumbuka kipindi chako kinaangaliwa na wengi hata watoto.Chunga sana maswali yako
    Hata hivyo nakupongeza kwa kazi nzuri sana.

    Ahlam,,,,London

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2012

    hawa vijana wawili wanaoingilia interview kwani wanafanya kazi na Salama? wanakera sana sana sana! wanatakiwa wafunge midomo wamuache Salama afanye kazi yake..hebu salama waambie hao wanaodakiadakia...

    ReplyDelete
  3. Kipindi kwa jumla ni kizuri sana, ila hayo maswali wanayouliza kuna baadhi yanakuwa ya msingi na ya maana, ila kuna mengine sometimes wanayachomowa tu mradi yamewajia tu vinywani mwao, ingependeza zaidi kama interview yao ikawa 'formal' kuliko ilivyo sasa, maana ukiangalia hao vijana wawili nao, mara huyu kachupia hapa huyu pale, kidogo inakuwa haipendezi. Actually, hawakatazwi kuuliza na wao, ila ingependeza zaidi kama wangejaribu kupangilia maswali yao na utaratibu wa kumtupia huyo muulizwaji. Zaidi ya hayo, hongera sana kwa waandaaji, waongozaji na khususan hao wahusika watatu tuwaonao hapo kila mara kinapokuwa hewani kipindi hicho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...