·        Watu wazima kulipa 2500/- kwa siku na watoto 500/-
·        Tiketi za kupaki magari madogo kwa siku ni 4000/- ma maroli ni 40000/-
Dar es salaam 26 juni 2012, Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayoanza tarehe 28 ya mwezi Juni hadi tarehe 8 mwezi ujao.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mdhamini rasmi wa mawasiliano wa maonyesho hayo Vodacom Tanzania, Tantrade imetangaza malipo ya Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000. 

Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine.

Malipo ya ada binafsi.

1.      Kwa siku - watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-
2.      Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-
3.      Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-
4.      kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-
5.      malipo kwa kipindi chote cha maonyesho - Beji kwa wahusika wa maonyesho   - 20,000/-
6.      Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/-

Tiketi za uegeshaji magari.

1.      Kwa siku (magari madogo)  - 4,000/-
2.      kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-
3.      Malipo kwa pamoja – 200,000/-
4.      Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
5.      Maroli na magari makubwa – 500,000/-
6.      Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-
Maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonyesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko Tanzania, maonyesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na wanaohudhuria kupata nafasi ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2012

    Ahsanteni TANTRADE:

    Si walisema Laki si pesa?,,,ingawa ni hivyo lakini Tshs.5,000/= haikuwa ndogo!!!

    Maana ile Kiingilio cha 5,000/= kwa siku kilikuwa ni kiwango cha kuweza kumudu Mafisadi pekee na familia zako!

    Sisi akina 'Embalasasa Mjusi Shemboza' hatukuwa tunaweza kuimudu, mara zote tulikuwa tunatumia kuingia kwa kuruka ukuta!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2012

    Ahhh afadhali!

    Maana Kiingilio cha BUKU TANO wengi tulikuwa tunatumia kuingia Uwanjani kwa kujichanganya na kujifanya Ma-Stafu wa Uwanja ama Makampuni,

    Na kama tukishindwa ilikuwa tunasubiri Malori yanayoingia tuna benjuka nyuma kwenye bodi na kupita nayo hadi ndani.

    Bongo ndio kama tulivyoizoea!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2012

    Mnhhh

    Nafuu imepungua sasa, nakumbuka kwa Kiingilio kile cha (5) niliwahi kuzama uvunguni mwa lori la Soda ili niingie ndani Jamaa wasimamizi wakaniona wakanichomoa!

    Nikajaribu mara ingine nikazama katika buti ya taxi, tokea asubuhi nikihangaika ndio nikapia lakini ilikuwa ni jioni giza linaanza kuingia!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2012

    Angalau na sisi tutaweza kuingia,
    sio mchezo ile 'elfu tano' ilikuwa ni 'laki moja kwetu' !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...