Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (katikati), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 53, Naibu  Makamu Mkuu wa Chuo cha St. Augustine (SAUT) Mwanza, Taaluma, Padri Thadeus Mkamwa (kulia) katika hafla iliyofanyika chuoni hapo hivi karibuni. Anayeshuhudia kushoto ni Naibu  Makamu Mkuu wa chuo hicho Utawala na Fedha, Padri Peter Mwanjonde. Msaada huo ni kwa ajili ya mradi wa maji chuoni hapo  pamoja na kilimo cha umwagiliaji.  
  Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT, Mwanza, kabla ya kukabidhi mfano wa hundi yenye themani ya shilingi milioni 53 fedha ambazo zimetolewa ili kutekeleza mradi wa maji kwa matumizi ya wanachuo na kilimo cha umwagiliaji. 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St. Augustine ( SAUT) Taaluma, Padri Thadeus Mkamwa, (mwenye koti jeusi) akizungumza na wanafunzi na walimu wa chuo hicho muda mfupi kabla ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 53 kwa ajili ya mradi wa maji na kilimo cha umwagiliaji. Hundi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tannzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kutoka kulia) jijini Mwanza hivi karibuni.  Mwenye miwani ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho , Utawala na Fedha, Padri Peter Mwanjonde .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...