Bwana Michuzi
Kwa wale waliopitia Tosamaganga wape hii link waweze kukumbuka ya enzi hizo.
http://www.stats.ox.ac.uk/~marchini/vsopics2.html
Naambatanisha picha ya mkusanyiko siku ya ijumaa asubuhi na nyengine ya pita pita. 
 Picha kwa hisani ya mdau Jonathan Marchini aliefundisha Tosa enzi hizo
Mdau Anthony L.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2012

    Mdau asante sana kwa kunikumbusha shule niliyoipenda hadi leo nawaomba waliosoma hapo kuanzia miaka ya 1980-84 wapokee salaam zangu za heri na baraka. Wale wote waliocheza ile ngoma ya kimanda kutoka Ludewa wakiwa Mkonyi ambaye sasa ni daktari nawasalimia sana akina Linus na wengine popote mlipo.

    Nimetamani kama ningekuwa narudi nyuma ningerudia shule nisome tena Tosa,hahahahahaaa siku zimeenda ni over 28 years now,nimezeeka sasa hahahaaaaaaa ila pawepo na reunion jamani ni muhimu tena tukutane palepale shuleni.

    ReplyDelete
  2. Imenikumbusha mwaka 1999-2001 nikiwa tosa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2012

    Dah, my camp Tosamaganga,..........hakika nilikupenda sana wewe shule na ndio maana nikapita hapo......Msalilwa, mkangwa mazege, fyudo, mlelwa, kibiki, nyaganilo, aaaagh nearby lyalamo.....Live long my school.

    Mdau Mbije, Andendekisye(1995-1998)

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2012

    Yaani nimekumbuka mbali sana, mimi ni Hamisi Saidi walikuwa wananiita kwa nickname ya KINGDOM. Nilimaliza pale mwaka 2000 form 6 nilikuwa PCM3. Ile ilikuwa bonge la shule na kipindi hicho Mkuu wetu wa Shule alikuwa Mr. Mkangwa, he was gentleman yule bwana utadhani alikuwa na dawa hata kama mkiwa na nia ya kugoma kuingia madarasani mkimpa nafasi ya kuongea nae mmekwisha wote lazima mtalainika na kurudi madarasani.

    Nakumbuka mwaka ule shule ilitoa wanafunzi wengi walioingia UDSM na vyuo vingine vingi. Baadhi tu niliokuja kusoma nao Mining Engineering ni Mtimbange, Ndomba, Nesphory Paul na wengine wengi katika kozi nyingine walikuwepo Frank Mlwale, Michael John, Gadiel Benjamin (huyu nilianza nae tangu O'level kule Lyamungo - Moshi), Mashaka Harison (Osborne), Tito Sifael, Ramadhani Mfaume, Ramadhani Hashim, John Sausi na wengineo wengi.

    Naungana na mdau alitangulia kama inawezekana tungekutana wote pale pale shuleni. Ingekuwa nzuri sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2012

    Excellent stuff. I was there between 1999 and 2001 A-Level and it was exciting environment. It is amazing how years pass by; since our time we are already counting over 10years and most of us are professionals in different fields. I'm sure if we united to look back, Tosamaganga would be a much better school. My last visit there was 2008 and I saw evidence rapid deterioration of buildings and the environment at large. We need to do something.
    Wish to remember great volunteer teachers during our time Allison Kind (UK), Dale Larson (USA) and Jake Ashcraft (USA). They did a great job and they are great people. Thanks guys where ever you are and whatever you do, God make you successful. In addition we remember local teachers who were there during our time the great Mkwangwa and the rest. For those who passed away former students and teachers R.I.P

    Clarence

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2012

    Ni enzi za headmaster Mpogole au ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...