Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba akiongea na waandishi wa habari mjini Zanzibar hivi karibuni.
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Rashid Assaa akiongea katika mkutano na viongozi wa mikoa na wilaya mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Joseph Warioba na Mjumbe wa Tume hiyo Dkt. Salim Ahmed Salim.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatarajia kuanza kufanya mikutano na wananchi wa mikoa minane kuanzia siku ya Jumatatu, Julai 2, 2012 hadi Jumatatu, Julai 30, 2012 kwa lengo la kukusanya maoni yao kuhusu Katiba Mpya

Mikoa hiyo ni Dodoma, Kagera, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Pwani, Shinyanga na Tanga. Katika mkoa wa Dodoma, Tume itaanza na Wilaya ya Bahi; Katika mkoa wa Kagera Tume itaanza na wilaya ya Biharamulo; Katika mkoa wa Manyara Tume itaanza na wilaya ya Mbulu na katika mkoa wa Pwani Tume itaanza na wilaya ya Mafia.

Kwa mkoa wa Shinyanga Tume itaanza na wilaya ya Kahama na kwa mkoa wa Tanga, Tume itaanza na Wilaya ya Lushoto. Kwa Zanzibar, Tume itaanza kukusanya maoni katika mkoa wa Kusini Unguja katika wilaya ya Kusini.

Taratibu zote za kuanza kazi zimekamilika zikiwemo kuandaa ratiba na kuisambaza katika mikoa na wilaya husika. Wajumbe wa Tume na watumishi wa Sekretarieti wamejigawa katika makundi saba. Kila kundi litafanya mikutano katika mkoa mmoja isipokuwa kundi moja litakalofanya mikutano katika mikoa miwili ya Kusini Unguja na Kusini pemba.

Tume inawaomba wananchi kuhudhuria mikutano itakayoitishwa na Tume na kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao kwa uwazi, uhuru na utulivu.

Pamoja na kuwasilisha maoni kupitia mikutano itakayoitishwa na Tume, wananchi pia wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz) au kwa njia ya posta kupitia anuani za zifuatazo: 

i. Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Makao Makuu, Mtaa wa Ohio, S.L.P 1681, DAR ES SALAAM, Simu: +255 22 2133425, Nukushi: +255 22 2133442; Au ii. Jengo la Ofisi ya Mfuko wa Barabara, Mtaa wa Kikwajuni Gofu, S.L.P. 2775, Zanzibar, Simu: +255 224 2230768, Nukushi: +255 224 2230769

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2012

    kwa nini zanzibar wakusanye tume kusini mwa unguja kwa nini? wameona kwingineko hawatapata maoni kwa sababu watu tumeshachoka tuacheni TUPUMUWE NA TUNADAI ZANZIBAR YETU MPAKA KIELEWEKE.

    ilikuja tume ya nyalali kukusanya maona sasa imeshafika nusu karne na vikao vimeshafika 80 vimeshakaliwa toka kuundwa tume hizi. wanakula pesa tu kuunda tume kwani unadhani hatulijui hilo kila wakikaa vikao hivi wanalipwa pesa na hakuna cha maana kinachofanyika.

    tumeshaamka babaeeeh hatutaki muungano tunataka nchi yetu ZANZIBAR HURU

    Kila leo kuundwa tume na kero za baa hili la muungano halisuluhishwi tumeshachoka tuacheni tupumuwe.

    tembo kishaingia shimoni mnataka kumvuta mkiaa ili atoke mtaingia wenyewe bora muacheni tembo humo humo shimoni.

    tumechoka Na udanganyifu wenu tuacheni TUPUMUWE.Hatutaki KATIBA MPYA YENYE VIRAKA WALA SERIKALI TATU TUNA TAKA NCHI YETU NA INSHALLAH TUTAIPATA MKITAKA MSITAKE KWA SABABU ALLAH AKBAR (MUNGU MKUBWA )

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2012

    nilijua tu utabania comment yangu lakin ninachosema ni hivi

    longa longo hatutaki jamani tumeshachoka tuacheni TUPUMUWE TUPENI NCHI YETU HATUTAKI KATIBA MPYA YENYE VIRAKA TUNATAKA NCHI YETU FULSTOP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...