Maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Saba saba  yameanza Juni 28, 2012 katika viwanja vya Maonesho vya  JK Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania wanashiriki maonesho hayo makubwa Tanzania, huku serikali na taasisi zake nyingi zikiwa moja ya washiri katika maonesho hayo yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzanaia.

Pia taasisi za Kimataifa na mashirika makubwa duniani yanashiriki maonesho hayo, miongoni mwa mashirika hayo ni Umoja wa Mataifa ambao upon a taasisi zake zote zaidi ya 21.

UN Tanzania wapo katika Banda la Ali Hassan Mwinyi na elimu mbalimbali juu ya Umoja huo wa Mataifa ambao Tanzania ni mwanachama wake unapatikana.   
 Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi walio telea Banda hilo leo.
 Afisa habari wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Austin Makani akiwa na Afisa Habari wa Umoja wa Umoja wa Mataifa (UN) Hoyce Temu.
 Mjasiriamali, Bi Magreth Msuya kutoka Kikundi cha MATA Woman Group cha Tabata jijini Dar es salaam ni moja ya watu wanaofaidika na UN, na hapa anashiriki maonesayo ndani ya Banda la UN. Kulia ni mteja anaeangalia bidhaa zake na kto ni Afisa Habari wa UN Tanzania, Hoyce Temu.
 Wageni katika banda la UN
  Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa wananchi walio telea Banda hilo leo.
Banda la umoja wa Mataifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...