Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Anna Mkapa(kulia)  na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi  Sinare-Majaar(kulia kwa Mama Mkapa)  wakiangalia aina ya vipodozi vilivyotengenezwa kutokana na mimea ya asili jana jijini Dar es salaam wakati Balozi huyo alipotembelea banda la EOTF . Kushoto  ni Meneja wa Masoko na Mauzo kutoka Equator Natural Comestics ya Jijini Dar es salaam Anna Mnaya.

EOTF imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza wajasiriamali kinamama kwa mafunzo ya mbinu za kisasa ya kutengeneza, kupakia na kuuza bidhaa wanazotengeneza wenyewe ambapo mamia ya kinamama wamenufaika sana na taasisi hiyo. Kwa takriban miaka 10 sasa EOTF imekuwa ikiandaa mabanda maalumu ya kinamama wajasiriamali katika maonesho hayo ya SABASABA kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...