Ankal habari ya Swaumu..
Naomba usinibanie hoja yangu hii ambayo nahisi wengi itakuwa inawakera ila hawajui wasemee wapi. Ila kwa kuwa Blog yetu ya Jamii ni kama chombo mama cha habari za mitandaoni najua meseji itakuwa sent nikipitia humu.

Ankal kuna hili tangazo la Coca Cola ambalo linasema sijui wakati wakinanani sijui wanafanya nini, waafrika wanafanya hivi; halafa mwishoni kabisa ndio kulikonifanya nilete hoja hii hapa ijadiliwe. Pale mwishoni kuna maneno yanasikika "WAKATI DUNIA INAFIKIRIA YA MBELENI , WAAFRIKA WANAKUNYWA NA KUFURAHIA COCA COLA..."

Kunradhi, naweza kuwa nakosea ama njimekosea kunakili lakini hoja yangu hapa ni HIVI NI KWELI WAAFRIKA KAZI YETU NI KUBWIA TU SODA BADALA YA KUFIKIRIA YA MBELENI?

Kwanza kabisa naomba Coca Cola watutake radhi kwa hili.  Kisha naomba ufafanuzi toka kwa wahusika, maana huenda lugha hapo ni gongana. La, wabadili kipengele hicho cha mwisho maana kinatudhalilisha wamatumbi.

Mdau Kilwa Masoko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2012

    Waafrika siku zote tumeonekana kuwa ni watu tusio na maana wala uwezo wa kujiendeshea mambo yetu. Hili tangazo ni kielelezo kidogo tu cha mtizamo huo. Yafaa hatua zichukuliwe kwa kweli, kwa mfano kuwaagiza cocacola walirekebishe hilo tangazo. Vinginevyo tuache kunywa hizo soda zao...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2012

    Wala isikupe shida inategemea wanasema ya mbele yapi,kama ni mambo ya kidunia wala siyo issue waache waendelee sisi waafrika tujitahidi na tujifunze kwa bidii kuutafuta uso wa Mungu wakati wao wanatafuta mambo ya hapa duniani ambayo hayana maana, ukizingatia hapa duniani sio kwetu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2012

    yaani mdau kula tano, hili tangazo limekuwa linanikera kila nikilisikia, Sijui maana kila mtu ana uelewa wake lakin mim binafsi linanichefua kwa kweli.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2012

    ukweli unauma!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2012

    Nakuunga mkono

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2012

    kinawadhalilisha wapi hamtaki kuambiwa ukweli kama Africa mmelala,wenzenu wanaendelea

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2012

    kinawadhalilisha wapi hamtaki kuambiwa ukweli kama Africa mmelala,wenzenu wanaendelea

    ReplyDelete
  8. Pole sana kwa kuguswa na hilo Tangazo. Kiuzalendo upo sahihi, lakini kiuhalisia Watowa tangazo hawajakosea sana kwani kula na kunywa ndio fikra za wanatuongoza, na sio kwenda mbele. Any way message sent.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2012

    Kumbuka hiyo si taarifa au tamko rasmi bali hilo ni tangazo tu mdau kwani sifa ya tangazo la kazi ni kulifanya la muhimu kuliko vitu vyote. Kwahiyo kama tangazo la mitandao likisema ni MTANDAO BORA KULIKO YOTE ina maana mingine sio mitandao? biashara ni kuremba

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 24, 2012

    Coca cola Tanzania jibu hoja ya mzee wa Kilwa Masoko.Hapa hatusutani...tunaelimishana tu!.

    David V

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2012

    Pamoja na kwamba kwa waafrika maneno haya yanafedhehesha lakini ndio ukweli. Si unaona yanayoendelea ktk bara la Afrika na viongozi wake? Ni ubinafsi na kujaza matumbo yao (kujaza COCA COLA) Kwa watengezezaji wa COCA COLA inawezekana tafsiri hii isiwafurahishe lakini nadhani bila kukusudia wametangaza ukweli.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 24, 2012

    Kitu gani ambacho sio kweli katika huo msemo wao? Angalia hapo kwenye picha, duniani sasa watu hawabebi mizogo namna hiyo. Wanatumia vitruck kazi rahisi. Sasa ingekuwa Waafrika tunafikiria mbele basi huyo angevaa nguo zinazoendana na wakati huu. Kubali ukweli hata kama unauma ili ubadilike na kupata maendeleo. Kubali kuwa Wazungu wametuzidi sasa ili tuendelee lazima tufate frameworks zilizowafanya waendelee kwa kurekebisha kwa mazingira yetu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 24, 2012

    kwa kuwa Tz na waafrika wanaongoza kwa kunywa kinywaji chao cha coca cola kuliko kufanya kazi na kuwekeza kwa maisha yajayo,so hawa jamaa wanajaribu kutukumbusha tufikilie dunia inayokuja na siyo kukalia kunywa kinywaji chao tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 24, 2012

    Hivi afrika haipo duniani? Dunia inafikiria ya mbeleni YES afrika inclusive...kizuri ni kwamba we have added advantage ya kubwia COCA COLA. mtazamo tu...!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 24, 2012

    huo ni udhalilishaji coca cola wala la kujibu kuhusu hili na ni ubaguzi wa rangi na si waafrika wote hatuwazi ya mbele.... ila kingine kinachonishangaza ni kubaguliwa alaf ukaiona ni sawa tuu waafrika tunakwenda wapi?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 24, 2012

    Tangazo la picha lina toa ujumbe kuliko maandishi na maneno.Kama picha ndo inavyo onyesha then wakaongezea maneno basi huo ni udhalilishaji,huwezi tumia weaknes ya mtu kumdhalilisha,hata hao wazungu wanamapungufu yao(negative)ila hatuwezi kuwazalilisha kupitia mapungufu yao.Hope vyombo usika vitachukulia hatua matangazo yanayo dhalilisha utu wa mtu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 24, 2012

    Nakupongeza sana mdau kuleta hoja hii hapa jamvini. Kwanza mimi sinywi soda ya coca kwa kipindi kirefu sasa,ni zaidi ya miaka 10. zingine natumia. ukiniuliza ni kwanini nitakujibu kiufupi tu kuwa sizipendi.
    Nawakumbusha kidogo: Wakati wanatoa tangazo nia yao ilikuwa siyo kutupasha waafrika ukweli, bali ni kutuvutia ili wale ambao walikuwa hawatumii soda hiyo waanze kutumia. Kiukweli kuna watu wametafsiri kuwa ukinywa coca ndo unakuwa huna plani za mbele. Hapa mipango ya mbele sio lazima iwe mikubwa bali ya kawaida kukuwezesha kuendelea. "we proceed at different speed". sasa kutokana na hivyo kibiashara tunahesabu kama hasara kwakuwa hujaongeza wateja kutokana na hiyo advertisement. Wameboa kwakweli na hakuna mwafrica aliyevutiwa kutumia hiyo soda kutokana na hyo tangazo.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 24, 2012

    nadhani na tuache kunywa hizo Coca cola, maana waliotengeneza hilo wameliona hilo kwamba zinanyweka hasa huku Afrika (tunaacha kunywa Juice za matunda yetu halisi)na uchumi tunajenga wa kwao kwa kunywa hizo Coca cola.
    tunashindwa kukausha matunda yetu na kuungaza, tunaacha yanaharibika. nchi zingine wanakausha au kusindika. mambo yetu tunayaharibu wenyewe, hivi kuna mtu ambaye anatoa maamuzi anasoma hizi comments? maana mawazo mazuri yaanaishia kwenye hizi blog zetu. na pia tunapochangia tuwe tunajaribu kuangalia hoja na sio nani amesema ame-comment nini. Tuwe-Constructive

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 24, 2012

    nilipata kuona hii post kwenye
    http://hermespower.blogspot.com/2012/07/coca-coca-advert-is-it-fare-for-african.html

    Hakika namuunga mkono uyu jamaa kweli ni good marketing

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 24, 2012

    Hasira ya nini,stop drinking coca cola,fanya tangazo ya ku support their rival [pepsi cola]moyo utatulia,pole sana

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 24, 2012

    hayanimamboyanayozidikutudhalilishawaafrika

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 24, 2012

    the problem with us Africans is cowardness, some races or religions would have protested against this and at times even claim compensation for publicly undermining our race. But this is the same attitude we had a while ago which led to our colonisation and even now the same attitude is used by other Africans to collabo with white people to undermine their fellow black Africans (its a shame).
    We need to wake up and speak against anything that undermines us, these people have the courage even to make movies talking nasty about Black people (indirectly), and when we black watch these movies we think its funny/comedy, and just laugh.
    We need a new black generation which are confident enough to say NO to such behaviours.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 24, 2012

    Ukweli maoni alivyo sema kwani Africa haipo duniani?

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 24, 2012

    Coca Cola ni Kampuni ya Wazungu (watu weupe) Haya Makampuni mengi pia ni ya kwao hivyo kwa msingi huo Maafisa Wanaopitisha Uakisi wa Maneno ya hao matangazo yao pia ni wale wale!

    Hebu angalia mfano katika haya Makabila yetu ya Jadi inapotokea mtani wako wa jadi kikabila akikuzungumza mbele za watu atakuvika nguo?

    Ni wazi kuwa mtani wako atakusasambua uchi wa mnyama!

    Hivyo mtu mweupe daima amejenga dhana ya kumbeza mtu mweusi!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 24, 2012

    Acheni kunywa coca cola mimi niko UK nimekuja Hulu nimeyaona madhara ya coca cola sio nzuri inanenepesha wanawauzia maji ya sukari na rangi. Acheni kunywa inamadhara makubwa. Kunyweni maji na jusi za matunda

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 24, 2012

    hahahaha mtakunywa sanaa coca lol....

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 24, 2012

    Kama kweli tangazo linatukera suluhisho si kumwadabisha Cocacola bali kuonyesha kama waafrika hatuko kama tangazo linavyosema. Ni sisi waafrika ambao tunazungumzia matatizo ya kale hadi sasa mf malaria, kipindupindu, njaa, nk wakati wengine wanafikiria nishati mbadala nk.

    Waafrika tumezoea kushikia bango fedheha kuliko vitu vinavyotusaidia kila siku. Sauper alitengeneza filamu ya mapanki na kila mtu akamlaumu kwama anatudhalilisha ilhali tunakula mapanki kila siku.

    Tubadilike, tufikirie namna ya kutatua matatizo yetu ili tuonekane kweli tuna akili na tunaitumia kufikiri.

    Ignorant,

    Mbeba box

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 25, 2012

    Tangu zamani sinywi coca na kila ninaemuona akinywa namsihi asinywe, ina sumu ya kuua baada ya muda mrefu. Hivi unaweza kuamini kwamba wakati inaanza kutengenezwa bwana mmoja alibwia sana lile donge la coce na akafariki? ina cafein ambayo kwa kuzidi ile concentration ilimuua. Ukweli soda zote sio nzuri kunyweni natural juices watabaki na tangazo lao sisi tutaongeza afya na kusonga mbele.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 25, 2012

    Ukweli ni ukweli tuu, nyie pigeni kelele lakini najua wengi wenu mwaishia kunywa Coca cola.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 25, 2012

    Nimepitia maelezo ya wana blog,lakini sehemu kubwa ya arguments ni upotishaji tu.Coca-cola licha ya kwamba original yake ni USA bado ni kampuni yetu kwani inatoa ajira na kuchangia uchumi wa Bongo kwa kiasi kikubwa.Tangazo la Coca-cola halidhalilishi waafrika wala watanzania ila linaonyesha mazuri ambayoAfrika au Tanzania hatujayapa priority na kujivunia kwahiyo ni wakati wetu kuona kwamba hata hapa Afrika kuna mambo mazuri sio ulaya.Tusilalamike tu bali tuchukua action kwa kuwa proud na utanzania wetu au Uafrika wetu.Mara ngapi watanzania wenyewe kwa wenywe hatusifiani kazi kulaumiana tu na kutakia wengine mabaya.Ni wakatiwa kuamka tuache kulala vipaji tunavyo tuwe creative,innovative na tuwe na malengo ya maisha ya baadae sio kulalalimia na kupiga majungu kwa kupotosha umma kwa kutumia udhaifu wetu.Hongereni Kampuni ya Coca-Cola kwa mchango wetu katika michezo na burudani kwa ujumla.Cheers..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...