Salamaleko  Ankal,
Nimeibuka tena baada ya kimya kirefu cha kusoma hoja za haja, maombi ya misaada tutani pamoja na maoni ya wadau na waosha vinywa  ambao wote ni anonymous kama kawa. Siju wanaogopaga nini kujitaja… Enewei, ni uhuru wa kujieleza ambao nilimsikia siku moja mkulu JK anasema kwa hapa Bongo saa ingine unapitilizaga – na yeye yuko kimyaaaaa… Ubarikiwe JK kwa hilo. Maana ungekuwa dikteta saa hizi sizani hata kama Libeneke hili lingekuwa linatoa ukumbi kwa akina sie.

Enewei, mie Ankal leo msaada tutani wangu ninaoomba, sitafuti mchumba wala sijisifii nimekula nondozzz ngapi kama unavyoita mwenyewe. Na wala sisemi kuwa ni hensam boi ama naendesha Hama. Mie ni wa kawaida tu, naishi Dar maeneo ya Kisukulu, nna kakibanda kangu ka uani  ka vyumba viwili, choo paspot saizi cha nje. Najivuta nijenge kubwa baadaye ya self container. Umri miaka 38, nna mke na watoto watatu. Kazi mjasiriamali wa kujitegemea, hivyo uchakavu na mazagazaga havisumbui kihiiiiiivyo….fegi napiga kwa jamu na ulabu wa kawaida tu, tena sio vikali ni bierre tu.

Mie Ankal na wadau (ashakhum si matusi, na kunradhi kama ntawakwaza), ni kwamba heshima ndani ya boma langu imepungua sana siku hizi, na sasa naomba msaada wenu mnishauri nifanyeje nirejeshe heshima ya boma hili, hususan kwenye maswala ya chakula ya usiku. Wenyeji wa humu mnanielewa. Wageni naomba mtafute wenyeji wawafahamishe maana ya chakula ya usiku...

Nimefanya utafiti wa kina lakini sijapata tiba endelevu, ama ya moja kwa moja. Kuna walionambia nile Ngogo (nyanya chungu), wengine wamesema nijaribu kubwia pweza mara kwa mara ama mchuzi wake mzito almaarufu kama ‘Mkuyati’ ama mti wake wapi! Heshima bado haijarejea moja kwa moja. Inarejea siku mbili tatu, nikiacha mambo yanarudi pale pale….

Haya kuna wengine wamenitonya nijaribu karanga mbichi ama korosho, wengine wamesema nipige sana plantain (ndizi za kuchoma) na wengine wanasema  uji wa asali (wa nyuki wakali wadogodogo) na tende unasaidia. Yote hayo nimejaribu lakini ngoma bado bila bila.

Wadau naomba msaada wenu. 
Nifanyeje nirejeshe heshima ya boma?
Mdau wa Kisukulu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2012

    Pole mdau. 1. Fanya mazoezi ya kutembea angalau dakika 40 kwa siku. 2. Ongeza mboga na matunda katika mlo wako. (mboga na matunda ni mkuyati asilia). 3. Kula/kunywa asali iliyochanganywa na tangawizi na hiliki kijiko kimoja cha 10mls kila siku. 4. Chemsha gamba la mti mmoja unaoitwa MJAFARI unywe japo kikombe kimoja kwa siku. 5. Masaa sita kabla ya "mechi" mezi kidonge kimoja cha CIALIS. Baada ya hatua hizo, heshima yako inaweza kurejea. Kila la kheri.

    ReplyDelete
  2. Mjomba nakuunga mkono sana kwa kuwa muwazi na tatizo hili ambalo linawakumba wanaume wengi hasa umri ukianza panda..Teknologia ya sasa inaruhusu hasa kwa wewe kupona na ngangari tena..Viagara na Cialis ni mwisho wa mchezo ndugu yangu...kabla ya kwenda kwa doctor na kuomba akuandikie cheti cha kununua hizo dawa unabidi ufanye yafuatayo : pima na fuatilia kwa makini sana blood pressure yako..ni lazima hili liwe na umuhimu wa pekee sana kwani matatizi ya high blood pressure / hyper tension ndio chanzo kikubwa cha jogoo kushindwa kupanda mtungi..angalie mlo walo wako na hasa vyakula vyenye mafuta futa na na kata sana chumvi katika mlo yako....na fanya mazoezi ya kutoka jasho sana....nimesema yote haya lakini bingwa wa yote ni viagara na cialis..sio mchezo babu...all the best...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    Pole kaka, umewahi jaribu kucheki hosp kama una matatizo ya kisukari? mzee wetu alioa mama mmoja ambaye hakuwa mtunza siri za nyumba akawa akitangaza ana njaa, kwenda hosp baba yetu alikutwa na kisukari hatua za mwanzoni. Akaanza matibabu hatukusikia tena aibu ile ya kulalamika kwa mama mdogo. I think mzee alipona

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    Pole ndugu yangu ukishapima afya yako Sema nitakusaidia kukutumia hizo dawa Viagra hapa zipo nyingi sana unanunua over counter

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2012

    Ni tatizo la kawaida kwa wanaume hilo na lisikuondolee raha ya maisha. Kwa vile umeshajaribu option mbali mbali bila ya mafanikio nahisi sasa uonane na daktari. Ukweli pweza, tende, asali, kitunguu saumu, vinaongeza nguvu za kiume kwa kiasi fulani. Pia ufanyaji wa tendo la ndoa kila mara pia linapunguza hamu ya hilo tendo lenyewe. Maradhi kama kisukari na blood pressure vinachangia katika kumfanya mwanaume apungukiwe na nguvu zake. Uchawi pia unaweza kusababisha hilo tatizo. Hivyo ushauri wangu anza kwa daktari baadae muone sangoma!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2012

    GOOD BLESS MICHUZI BLOG, MDAU KWA KWANZA SHUKRAN KWA USHAURI WAKO, NTARUDI BAADA YA SIKU 5 KUKUPA MATOKEO, WAGONJWA TUPO WENGI, SHUKRAN SANA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2012

    Wadau ushauri mzuri sana kweli tatizo linawakuta wengi sana,ningependa kuuliza hizi cialis ni vidonge au?na vinapatikanaje

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2012

    Vidonge ni vingi hasa huku marekani ila cha kufanya mtafute ndugu ama rafiki aliyeko huku mwambie akununulie wala sio bei nadhani kama dola 16 na 20 inategemea na dozi unayotaka sio big deal bwana acha kutishwa na watu na unaweza kuagiza online manake hizi Dawa zinatengenezwa nyingi sana Canada.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2012

    Mtakuwa mnarogwa kwa tabia zenu za kufungulia wanawake zipu zenu hovyo. Wengine wanga; haya mnashidwa hudumia wake zenu; sasa zamu yenu na nyie kusaidiwa!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2012

    e bwana wee, mtaua nyie duh !! hawa jamaa wa USA ndiyo walioshauri Viagara,ndugu yangu wacha kabisa usirogwe kutumia,vinaleta ugonjwa wa moyo ni hatari sana,pia ukinywa ,jogoo linasimama usiku kucha (1) kwanza utachoka ile mbaya, pili huyo mke atakuacha maana hata vumilia joto la jikoni. sasa ,mshikaji utakutwa na mabalaa kibao, kukimbiwa mke ,kuugua moyo. Please ushauri wangu kwako ni huu, si lazima kufanya kitendo cha ndoa kwa kutumia bomba, tumia njia mbadala kama vile vidole ,ulimi N.K, wala hakuna cha asali wala viagra.Asante. wako Zebedayo.

    ReplyDelete
  11. Cialis ni vidonge na vinapatikana katika maduka yote ya madawa baada ya kupata cheti cha daktari. Huku ughaibuni unauziwa cialis vidonge 4 kwa us $ 70. unakula kidonge kimoja unapata lijali la nguvu kwa wiki nzima, na kama ni mdhaifu saaanaaa basi unapata lijali la siku 3 mpaka siku 4. Kigono kinakuwa ngangari ile mbaya..sio mchezo !! ukila cialis nadhani bi mkubwa lazima akufunge pingu usiende katika matembezi yasiyo rasmi...hii ni jibu kwa huyo mdau wa juu aliyetaka kujua kama cialis ni vidonge.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 02, 2012

    Sikiliza brother, utakua either una kisukari ama kichocho chronic nenda cheki hospitalini na kisukari kama kiko stage za chini unaweza ku control na insulin make sure umecheki maana kuna watu walijisahau kikafikia level mbaya kiasi kwamba sasa hivi wakula kwa macho tu hicho chakula cha usiku, zamani nilishawahi umbuka nimeenda kwenye gemu ya usiku nilipofika pale jogoo hakuwika na ilikua game ya kwanza na yule demu duuh basi alinitangaza mpaka noma. Nikaenda kwa wamasai wakanipa dawa ya kutibu mchango/kichocho yaani mpaka leo hii imepita miaka 19 sijawahi piga chini ya bao tatu kila game na hata nikiona mapindo ya underwear ya demu kama kavaa tight skirt kitu lazima ki take off kama air tanzania vile
    U still young n I'm very possive utapona pengine tatizo lako si ugojwa bali ni saikolojia na kutojiamini unapokua kwenye game unachachawa kwa kimombo unakua frightened na hiyo hormone ya kuogofya ama kuogopa inazuia blood flow kwenda bomani as a result ile hormone ya testosterone inayohusika na mpango mzima wa wewe kutwa mwanaume inazidiwa nguvu na kama ujuavyo ule mshipa kule down under hauna mfupa na unasimama kwa nguvu ya damu. Kama hayo yote si matatizo ingia online google kuna herbs fulani za kichina zinaitwa Red Dragon ni noma hapa hamna chemical kama hayo ma viagra hiki kitu ni mzizi na umewekwa kwenye capsule kama rangi mbili vile unakula kwa siku tano tu basi unarudia hali yako ya zamani na zaidi na pia mshipa unakua mrefu zaidi na kunenepa jaribu utaona. Mwisho kabisa kama unavijisenti wacheki kuna jamaa online wanaitwa Boston medical group wewe wa google hawa jamaa hiyo ndo kazi yao na sijui kwa huko bongo utawapataje lakini my guess wewe umesoma so sioni issue sensitive kama hiyo usiishughulikie maana usije ukageuzwa joka la kibisa halafu washikaji wawe wanakugongea mkeo but do whatever it takes to get ur mojo back and perform miraculously in your next game. Goodlucky buddy
    And I'm out n about

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 02, 2012

    Cialis ni vidonge kama Viagra

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2012

    Mimi ni mdau wa jinsia ya kike. Nakushauri usitumie madawa yatakayo kuathiri in long term. Usijaribu kutatua tatizo sasa hivi halafu ukawa na matatizo makubwa zaidi baadae. Umepata ushauri mzuri lakini tafuta printer print all comments halafu upitie moja baada ya nyingine. Nasema hivi kwa sababu wanaume mnakuwaga active kwenye shughuli kwa muda mrefu sana. Unasikia mpaka vikongwe wa miaka 70 bado wako shughulini na wanaoa vibinti huko vijijini. Kwa hiyo ukipata solution ya kufanya kazi kama simba sasa hivi baada ya miaka 10 (when you are in your 40's) bomba linaweza kufa kabisaa kama bomba la maji la DAWASA (linabaki urembo) ndio itakuwa balaa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2012

    I wish ningekuwa msaikolojia nikakushauri kisomi zaidi kuliko shortcuts za vidonge ambavyo ni hatari pia na vina mwisho wake.
    I would feel the same kama mke hajiweki kiujana/kiutoto/sexy kwa mavavi, usafi, usafi wa chumba nk.
    Pia dressing styles zake hasa jioni lazima ziwe na mvuto.
    Labda mazingira ya chumba lazima yaandaliwe kitendo/romantic ikiwamo mambo ya mishomaa, povu bafuni and all that.
    Yote inalenga kuamsha hari ya sex na nikuombe ujibiidishe na vitabu vya mnapenzi na mikanda ya mapenzi ukiinua hamu yako na kujifunza different styles, makaaji na maeneo ikiwemo kufanya jikoni, kwenye sofa, bafuni, kwenye gari, hotelini sometimes nk.
    What i mean is inaweza kuwa ni psychological kutokana na mnavyojiweka kwakuwa sex has a lot than wat we think.
    Mama pia awe mbunifu na mtundu kwani kifo cha mende kila siku ni boring.
    Kwako pia usafi, manukato, mwili wa mazoezi na sio tipwatipwa, kufagilia bustani. Vingi kwakweli vifanyike.
    Walioshauri mazoezi ya diet nawapa pongezi pia lakini hayo madawa yatakumaliza nguvu zote na soon ngoma itakauwa ze end.

    ReplyDelete
  16. Mzee wa mbaliJuly 02, 2012

    NAKUPA USHAURI MFUPI KAMA MTAALAM UKIUZINGATIA UTAFANIKIWA.ACHANA KABISA NA HABARI ZA VIAGRA KAMA ULIVYOSHAURIWA.PUNGUZA AU ACHA MATUMIZI YA SUKARI IKIWA NI PAMOJA NA SODA(SUKARI HUHAFIFISHA UIMARA WA TENDO.FANYA MAZOEZI KILA SIKU JIONI AU ASUBUHI KWA DK 40.PUNGUZA MATUMIZI YA VYAKULA VYA MAFUTA-MAFUTA MF. CHIPS, KUKU WA KUKAANDA NK NABADA YAKE UTUMIE MCHEMSHO.WEKA MATIKITI, ASALI, PILIPILI KATIKA DIET YAKO. TUMIA ALOVERA (WEINGI WANAIFAHAMU),PENDELEA KUTAFUNA MIHOGO, NA JAPO KIPANDE. USHAURI MWINGINE NIKUWA NA KIASI KATIKA TENDO(KIFUKO CHA MBEGU HUJAA BAADA YA SAA 72 -SIKU 3, KABLA YA HAPO UTAKUWA UNALAZIMISHA KUJIKAMUA) NA KUHAKIKISHA KUWA UNAONDOA VIKWAZO VYA KISAIKOLOJIA VILIVYOKO KATIKA MAZINGIRA YAKO.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 02, 2012

    Unaweza kutumia machungwa kwa mpangilio maalum na ukapona. Mimi nimesha tumia na nikaona majibu safi. kula machungwa (unamenya then unakula, usikamue juice). siku ya kwanza 5, ya pili 10, ya tatu 15, ya nne 20, ya tano 25, ya sita 25, ya saba 20, ya nane 15 ya tisa 10, ya kumi 5. ukimaliza kamjaribu mamaa uone balaa kwenye chakula chausiku.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 02, 2012

    Na nini dawa ya kutoa manii haraka yaani kuwahi kufika kileleni maana kuna frend wangu yuko bush yeye hupiga hata 7 per time lakini tatizo zote ni fasta dakika moja tu

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 02, 2012

    Alaykum Salaam,

    Al Ustaadh wetu pole sana na Masahibu hayo mazito yaliyokukuta.

    Kwa kiasi kikibwa nimewahi kusikia watu wazima hasa wazee wakipendekeza zaidi watu wenye tatizo kama hilo kutumia zaidi 'mizizi' ama dawa asilia ambazo zinaongozana na matumizi ya vyakula kadhaa vya ki asili badala ya kutumia madawa ya viwandani ambayo yana madhara ya upande wa pili ama haya ya viwandani yatatumika endapo jitihada za matumizi ya asilia zisipotoa matokeo mazuri.

    IMESISITIZWA KUFANYA HIVI:

    WAZEE WANASEMA 'UWEZO' HUTEGEMEA ZAIDI VITU VIKUBWA VIWILI:

    1.CHAKULA-
    Yaani hivyo vyakula asilia na miti shamba vitu kama mihogo mibichi, mboga za majani na matunda, samaki kama hao pweza,asali, karanga, baadhi ya mizizi kutokana na kila makabila yanavyotumia (hii ktk kila kabila wazee wanajua)

    Pia ktk suala la chakula inasisitizwa tuepuke sana vyakula vya viwandani ambavyo vina kemikali za ziada na pia tunashauriwa kuepiuka sana kula mikaango na rojorojo tupendelee zaid michemsho na kuepuka matumizi ya ziada ya SUKARI, CHUMVI NA MAFUTA YENYE COLESTEROL vyingi.

    2.SAIKOLOJIA-
    Wazee wanashauri tuepuke mikwaruzo na kutokuelewana ndani ya nyumba,kupata muda wa kutosha wa mapumziko baada ya kazi, kwa kuwa unapokuwa hujatulia Kisaikolojia pia uwezo wako wa kimatendo katika kujamiiana unateteraka kwa kiasi kikibwa.

    Tunatakiwa tujenge mapenzi na bashasha na wenza wetu ili tupate utulivu wa Kisaikolojia na kuleta hamu ya tendo.

    KAMA HAPO JUU WAZEE WANATUASA KUWA 'UWEZO' HUTOKANA NA CHAKULA NA SAIKOLOJIA!.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 02, 2012

    Alaykum Salaaam!

    Ustaadh pole sana, hilo ni tatizo kubwa sana kwa maisha yetu ya sasa na linawapata wengi sema tu wengine hawajakuwa wawazi kama wewe ulivyotuletea sisi nduguzo hapa Jamvini.

    Ukweli ni kuwa mficha maradhi kilio humuumbua!

    Pana Jarida Moja la Kimarekani la wana sayansi wa Kimaisha linaitwa ''Reader's Digest''.

    Hili Jarida lina kauli mbiu yake moja inasema 'your well being is how your life style is',,,yaani ''maisha yako ni vile mwenendo wako kimaisha ulivyo''

    LINAAINISHA YA KUWA MAISHA NA HALI YAKO KIAFYA VINAAKISIWA NA MTINDO WAKO WA MAISHA MWENENDO MATENDO UNAVYOKULA NA JINSI UNAVYOENDESHA MAISHA.

    KULINGANA NA MAELEKEZO YAO JARIBU MWENDO HUU HAPA CHINI WA MAISHA:

    1.CHAKULA;
    Jaribu kutumia vyakula vya kawaida
    (asilia) visivyo na virutubisho bandia badala ya vyakula vya viwandani ambavyo vina 'contamination' nyingi, (madhara ya makemikali na mabaki ya madini mfano ktk ushindikaji nivasagwa na mitambo ya vyuma na kuokota mabaki ya haya madini kuchanganyika na vyakula)

    Mfano kwa sisi tulio hapa Tanzania hakuna sababu ya kula vyakula vya makopo badala yake tunaweza kula vyakula vya kutoka Shambani au Sokoni moja kwa moja.

    Epuka sana mambo ya Chips Kuku wa kisasa na mayai ya kisasa, epuka maziwa ya kukorogwa na mashine, epuka Juisi za chupa na didhaa zingine, tumia Juisi asilia za kukamua matunda kwa mikono au mashine ndogondogo.

    Epuka matumizi ya ziada ya mafuta, chumvi na sukari katika vyakula.

    2.MAPUMZIKO YA KUTOSHA;
    Fanya kazi kwa vipimo na kutenga muda wa kutosha wa mapumziko, pia jenga mwenendo wa kuituliza Saikolojia yako na kuacha mifarakano na misuguano ya jamii ktk familia, ndugu na jamaa kwa kuwa inaleta Msongo wa mawazo (stress) na kukubomoa Kisaikolojia.

    3.MWENENDO WA MAISHA;
    Fanya mazoezi mepesi mepesi na kushiriki Michezo kama utapata nafasi.

    Kujamiiana ni sehemu ya maisha lakini usizidishe sana, isiwe kama ibada unatakiwwa ujamiiane kwa mpangilio kwa kuwa ukizidisha hata ile hamu 'appetite' inashuka na kujiona kama nguvu zinakuishia.

    Wanasayansi wanaeleza ya kuwa kupata huduma ya jamii kwa wiki X 2 sio vibaya kwa kuwa ukiwa unajamiiana mara kwa mara uwezo pia unashuka na hata 'mabao' yako yanashuka yakiwa hayana nguvu za kutosha yanakuwa 'too short'.

    4.STAREHE;
    Pata starehe kwa vipimo kwa kuwa nyingi za starehe huchosha sana , mfano kukaa hadi usiku kmubwa ktk kumbi za muziki na matukio mbali mbali kunafanya hata nguvu zako kijamii zinashuka, unatakiwa usizidishe muda wa starehe kwa kuthirisha.

    Kunya pombe kwa viwango, vuta kwa viwango n.k

    Starehe ikizidi inaathiri nguvu za kujamiiana pia.

    5.IBADA NA IMANI;
    Imani pia inajenga sehemu ya maisha, kama unafanya ibada unapata matumaini na kujenga uwezo wako wa kijamii zaidi.

    Hivyo Sheikh ukifuata Mwenendo huo wa maisha ktk vipengele hivyo vitano (5) hapo juu ni wazi utaona mabadiliko ktk uwezo wako Kijinsia na kimaumbile.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 02, 2012

    Acha kutoka nje ya ndoa, umeshalogwa tayari, muombe Mungu, tubu dhami zako. Na nyie wanaume wa Tz acheni kutokatoka ovyo, ss wake zenu tunawamis usku

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 03, 2012

    Ustaadh,

    Pole na matatizo,

    Pana hulka moja ambayo pia inachangia sana wengi kupelekewa kuishiwa na nguvu!

    Hii ni ile hulka na 7-UP au 'bunduki mkononi' kama baadhi ya Wadau hapo juu wamegusia.

    Pana wanawake wengine 'chupi mkononi' ukiacha siku za hatari na dharura kila mara wanataka, muda wote wanataka, !

    Kujamiiana kupo ni sehemu ya maisha, lakini ni jambo la kutia huzuni sana ukakuta wengi wakichukulia kuwa 'tendo la ndoa' ndio mhimili wa mahusiano na kuwa ni kama DOZI mfano,

    1.Kila siku lazima upate.

    2.Wengine wanafikiri kutomwingilia mke kila siku ni udhaifu, kitu ambacho sio kweli.

    3.Wengine hufikia hadi ugomvi kisa wanapotaka lazima wapewe na wasipopewa inakuwa tabu.

    4.Mtu unakuta akitoka kazini anawahi saa mbili usiku tayari yupo kitandani anamshinikiza mwanamke aje ili aanze!,,,ehhh hii sasa hata bata ana nafuu!

    5.Wengine hata Draft au maongezi mtaaani muda hana anawahi kitandani!,,,wengine huku chungu kinachemka jikoni yeye anamshinikiza mkewe amfuate kitandani!

    Kujamiina kupo, ni haki yetu ila kufanywe kwa mpango, sio kama kuku au punda vile!

    Sasa jamani hulka kama hizo 5 hapo juu zinachangia sana kushusha uwezo wa kujamiiana kama zikipitiliza!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 03, 2012

    Mdau wa 22 hapo juu Anonymous wa Tue Jul 03, 12:23:00 PM 2012

    Hahahahah umenichekesha sana,

    Hulka za 7 UP !
    Hulka za 'bunduki mkononi' !
    Hulka za 'chupi mkononi' !

    Pana ile Hulka ya 'zipu mkononi' !

    ReplyDelete
  24. mdau hebu tujuze kama ulifanikiwa tujifunze kwako au tukupe ushauri zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...