Hayati Mwalimu James Irenge enzi za uhai wake. Picha hii ilipigwa Novemba, 2011 katika Shule ya Msingi Mwisenge wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda mkoani Mara. 

Mwalimu James Irenge, ambaye ni mwalimu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana.

Habari zilizopatikana jana zilisema Mwalimu Irenge, alifariki dunia nyumbani kwake Mwisenge, Musoma mkoani Mara.

Mzee Irenge aliyekuwa na umuri wa miaka zaidi ya 120, alimfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge, kati ya mwaka 1934-1936.

Hadi mauti yanamfika, licha ya umri wake mkubwa, bado alikuwa na uwezo wa kusoma na kuandika mwenyewe bila kutumia miwani.

Wiki kadhaa zilizopita aliandika barua yake ya mwisho kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wiki iliyopita akimshuru kwa kumwezesha kumlipa fedha za dawa na chakula; mambo yaliyokuwa kilio chake cha siku nyingi.

Mwalimu Irenge mara kadhaa alikuwa akilalamika kwamba tangu alipostaafu ualimu miaka ya 1970 hakupata kulipwa mafao yake, na kiinua mgongo.

Kifo chake kinahitimisha uhai wa walimu wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu mwingine, Daniel Kirigini, alifariki dunia mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Mazishi ya Mwalimu Irenge yanatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii katika kijiji alichozaliwa cha Busegwe- Nyanza wilayani Butiama. Ameacha mjane, watoto 12, wajukuu 30 na vitukuu 15.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    poleni sana wafiwa.

    Mwandishi,naomba hapo juu urekebishe kidogo,
    nadhani tarehe ya picha sio Novemba 2012.

    Wazee kama hawa ingekuwa ni "national treasure" serikali ilitakiwa kuwahudumia kila hali na mali.

    Poleni sana wafiwa.

    Ni hayo tu.

    Mtoto wa Mkulima

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    Mungu akulaze pema babu. vitu kama hivi hata hatuvijui inasikitisha sana ingewekwa orodha na picha za hawa watu watoto wetu pia wajue. poleni wafiwa Mungu awape faraja

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2012

    Historia ya nchi yetu imepotea. Can you imagine Mzee kama huyu watu wangekaa nae chini na kuandika biography yake?

    R.I.P

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2012

    Wow! Hawa ni watu wenye maisha marefu, natafuta kumwoa mjukuu wake najua atakuwa na ka-gene ka maisha marefu ili watoto wangu waishi zaidi, ingawa najua mimi ka-gene kangu kata disturble kidogo lakini siyo mbaya sana wataisha angalau, badala ya kufa katika miaka ya ujana kama ilivyo kwa wengi.

    ReplyDelete
  5. Anon. wa kwanza kabisa, nakubaliana na wewe. Ila tatizo la huyu Michuzi, akikosolewa anarekebisha kosa lake mbio mbio au kisirisiri, halafu bado wewe uliyetowa 'comment' ya kumkosowa ataibandika 'comment' yako hapa hapa, ilhali kosa lake kaliona na kalirekebisha upesi upesi, matokeo yake wale wanakaokuja kuisoma khabari hiyo kwa baadae, wanaanza kujiuliza mbona hakuna kosa lolote? Kisha wewe uliyejaribu kumkosowa wakati kweli kosa lilikuwepo wazi na baadhi ya wasomaji waliowahi kuisoma khabari hiyo mapema wameliona, unaonekana mjinga. Inaudhi sana tabia hiyo.

    Hakuna mkamilifu, ila tu unapokosolewa ukarekebisha kosa lako, basi haina haja tena ya kuendelea kuiweka 'comment' ya mkosowaji hapa, wakati kakuzinduwa na ukaweza kulirekebisha kosa hilo. Ni mara nyingi sana kunakuwa na makosa madogo madogo kimaandishi, huenda ikawa ni 'poor editing' .

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2012

    Mimi nauliza jamani, pale UDSM watu wanasoma historia na wengine fasihi (literature), hadi wanapata shahada za uzamivu (PhD). Lakini historia ya nchi yetu inapotea au kupotoshwa hivi hivi tukishuhudia.Tafiti zao wanafanya wapi? Kwa nini hakuna vitabu ambavyo vina historia za watu kama huyu mzee na mambo waliyopitia? Hii leo hakuna historia zilizoandikwa kwa ufasaha za watu kama Nyerere, Sykes, Jumbe,Karume, Mwinyi,Thabit Kombo, Kawawa,Mkapa, Sokoine na wengineo wengi ambao matendo yao yameathiri maisha ya waTanzania wote kwa namna moja au nyingine. Wanakufa,wanatoweka,tunabaki kubahatisha tu kuwakumbuka. Wasomi wetu kwa kweli wanaliangusha sana taifa hili.

    Mdau, Dar es salaam

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2012

    yaani hata mwl Nyerere hakuhakikisha aliyekuwa mwl wake na mwl mwenzake analipwa mafao yake mpaka anakufa? kumbe utamaduni huu wa kutodhaminiana watanzania umeanza zamani!!

    ReplyDelete
  8. Kanindo-Arusha.July 23, 2012

    Tumepoteza nguzo ya muhimu katika historia ya nchi yetu.Huyu ndiye alimjuaMwl Nyerere siyo Maria au mwingine yeyote.Nimesoma habari watu waliovunja rekodi za umri mrefu duniani wengi ni wanawake. Kwa wanaume naona huyu kavunja rekodi kabisa.Kama kuna mtu mwenye ushahidi wa kumzidi basi wasiliane na mimi kwenye forum hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...