Diwani kata ya MWIMBI wilaya MPYA ya KALAMBO Mkoa wa Rukwa Leonard Shalamwana (wa tatu kulia)akimuonesha Mkuu wa wilaya Moshi Mussa Chang'a(wa tatu kushoto) chanzo cha Mradi wa maji utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 158.3 na kunufaisha takribani wakazi 8,000. Mradi huo unadhaminiwa na benki ya dunia, wananchi pamoja na mfuko wa maendeleo wa jimbo la Kalambo. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Miradi ya TASAF wilaya John Kiondo na Kaimu Mkurugenzi wilaya Sumbawanga Crispin Luanda.
Afisa Mtendaji wa Kata ya MWIMBI iliyopo wilaya Mpya ya Kalambo Mkoani Rukwa Mosses Nkinda akisoma Taarifa ya Maendeleo ya Kata hiyo mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo Moshi Mussa Chang'a (hayupo pichani) wakati wa ziara ya mkuu huyo wa wilaya kujitambulisha katika wilaya yake mpya jana. Mkuu huyo wa wilaya anatembelea kata zote 17 za wilaya hiyo iliyotokana na kugawanywa kwa wilaya ya Sumbawnga. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA SUMBAWANGA.

WAKAZI wapatao 8,000 wa vijiji viwili vya Majengo na Mwimbi katika Kata ya Mwimbi wilaya mpya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi unatekelezwa katika kata hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 158.3.

Mradi huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia iliyotoa zaidi ya shilingi milioni 154.4, wakazi wa kata hiyo wamechangia shilingi 2,709,000 na mfuko wa jimbo la Kalambo umetoa shilingi 1,200,000 ili kufanikisha mradi huo.

Akielezea mradi huo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Mussa Chang’a, diwani wa Kata ya Mwimbi Leonard Shalamwana alisema kwa sasa mradi huo uko katika hatua ya nne ambayo ni usambazaji wa maji katika vituo vikuu.

Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Mosses Nkinda alisema mradi huo utaongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi hao na kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza hali ya kiuchumi mara utakapokamilika.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo Moshi Mussa Chang’a alipongeza utekelezaji wa mradi huo na kuwataka viongozi wa kata hiyo kuhakikisha kuwa unakamilika haraka ili wakazi hao waanze kunufaika nao kama ilivyokusudiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...