Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi kupitia kwa wahariri wa vyombo vya habari leo Ikulu jijini Dar es salaam
Sehemu ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
wakimsikiliza Rais Kikwete leo
Ndugu Wananchi;
Naomba nianze kwa kuomba radhi kwa kutoa hotuba ya mwisho wa mwezi wa saba, leo tarehe 01 Agosti, 2012 badala ya jana tarehe 31 Julai, 2012.  
Hii ni kwa sababu ya msiba uliotukuta katika familia na mimi kwenda Lindi kushiriki maziko ya marehemu wetu.  
Tofauti na miezi iliyopita leo, pamoja na hotuba ya kawaida ya mwisho wa mwezi nimetoa fursa kwa Wahariri wa vyombo vya habari nchini kuniuliza maswali nami kujibu.  Kwa upande wangu nina mambo matatu ambayo nitayazungumzia leo.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Rais Wangu nina ushauri mmoja utakaomaliza tabu zako kwenye uongozi na kukupa fursa ya kulala usingizi kama wengine. Utamaduni wa kuchunguza na michakato isiyoisha lazima ukome.Kamwe hatutapiga hatua madhubuti kama sisi tutaendele ku plan tu wakati wenzetu wanasonga mbele. Huku majuu wanafanya hivi, wanatengeneza project phases na wanapanga tarehe ya kuanza. Hata kama una shilingi moja mfukoni tarehe ya kuanza ikifika unaanza tu. Mfano huo ujenzi wa mabomba ya gesi ukisema kwa mwezi tutajenga km 5 tu ndio uwezo wetu baada ya mwaka una km 60, miaka mitano una ka 300. Mpaka kufika miaka 5, wilaya nyingi zitakuwa zimefikiwa na wanaweza ku tap kwenye bomba kuu na kuanza kuuzia wananchi gesi na viwanda vya mtwara, lindi na sehemu zote njiani mwa mtwara na dar. Goal isiwe bomba kujengwa kwa mwaka mmoja na gesi kufika dar tu. Hujui wafanyabiashara wangapi watahamia wilaya za kusini kama gesi ikianza kutumika. Kuwa na short term goals ndani ya longterm goals. Inawezekana kabisa mh Rais na vijana wasomi wa kusimamia hizo shughuli tupo. Toa ajira uone tutakavyo miminika. Anza sasa hata kama hazina wana milioni moja tu, anza nayo achana ngoja ngoja, oh wahisani, oh bajeti ijayo, oh TRA hawana pesa za mapato. we anza tu!!!!! KM 5 kwa mwezi lets go. Na barabara hivyo hivyo, na airport mpya hivyo hivyo mifuko miwili ya smenti ipo kazi ianze.

    ReplyDelete
  2. Very true mdau wa hapo juu..... Haitawahi kufikia siku ambayo nchi hii itakuwa na pesa za kutekeleza majukumu yake Na mipango yake kibao AT A GO! Please Honorable Mr. President, huo ushauri wa bomba la gesi ni vema ukasikiliza ushauri wa kujenga kwa awamu. Wewe umeshatembelea nchi ya Trinidad and Tobago ambayo ina gesi nyingi sana na ingawa ni nchi ndogo tu yenye watu wasiozidi milioni 2, wamefanya maajabu kwa kutumia hiyo nishati ya gesi ambayo hata Rais Obama alipowatembelea alishangazwa sana. By the way, Trinidad and Tobago wanauza gesi yao nje ikiwa ni pamoja na USA.

    Nafahamu pia kuwa tunayo draft Master Plan ya Gesi, lakini bado tunasua sua kujipanga, wakati tunao marafiki wazuri toka Trinidad and Tobago ambao wako tayari kuisaidia Tanzania kusonga mbele kwenye sekta hii mpya ya gesi, bila kusubiria misaada ya nchi za magharibi.

    Mhe. Rais, kwa hili la gesi, tafadhali sana wape TPDC uwezo na uhuru wa kutekeleza mipango yao mizuri kutokana na uzoefu waliokwishapata toka nchi walizotembelea ikiwamo Trinidad and Tobago. Bila kusahau taasisi nyingine muhimu kwenye sekta hiyo na kuziwezesha. Mfano tu ni suala la Vipimo vinavyotumika kwenye sekta hiyo ya gesi..... Hivi nani anahakiki kiasi cha gesi inayonunuliwa Na TANESCO??? Tukisubiri watu wa Vipimo (Wakala wa Vipimo) wadundulize pesa za kununulia vifaa vya kuhakiki mita zinazotumika kununulia gesi, nchi itaendelea kupata hasara hadi kiama. Hao Vipimo wenyewe wanahangaika wenyewe, hata masuala madogo tu ya kudhibiti wizi kwenye mizani ya mabucha ni mtihani mkubwa, sembuse mita zinazopima gesi.

    Huo ni mfano tu Mhe. Rais lakini ipo mingi kwenye sekta ya gesi ambayo tusipochangamka sasa, yataishia kuwa kama Nigeria ambao wana mafuta kibao lakini hawafaidi hiyo neema kwa kuwa walianza na "A WRONG FOOT".... Mungu ibariki Tanzania na Rais wetu mpendwa.

    ReplyDelete
  3. Mheshimiwa Raisi, hivi ni kweli ulitia saini ya kutekeleza sheria ya kuzuia mafao?? kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa, lakini kwa hili CCM itapata adhabu kali hapo panapomajaliwa uchaguzi! hii ni dhambi ambayo kesho ahera utahukumiwa!!sisi wafanyakazi ambao tunategemea mafao yetu tuwasomeshe wenutu, tumalizie vijumba vyetu???

    ReplyDelete
  4. naomba Mungu Mh.JK ayapate maoni yenu wadau hapo juu. Ankal JK anaisoma blog yako?

    ReplyDelete
  5. wadau mliotoa mawazo hapo, sijui kama mmesoma hotuba ya mheshimiwa..mfano wa Trinidad na Toabgo kesha utoe, tumewaliliana na matafia na mashirika yaliyo na ujuzi wa kutumia kipato cha rasilima hii ili tufanye hivyo na sisi, akimaanisha wananchi na serikali wafaidi ili gesi siwe laana kama NIgeria na Angola. Ila ukiangfalai Equatorial Guinea, mafuta yameboresha maisha na nchi..na nadhani MH. JK anasema hivyo. Na amesisitiza mikakati ianze kuawa na sovereign funds sasa ili hapo baadae mafisadi wasikwamishe jitihada hizo kwani watao zinakwamisha makulaji yao.
    halafu hili nalipeleak sambamba na malalamiko wa wadau wengine kuhsu TRA, jamamni Mh Mkapa alipoanza kuiwezesha TRA kukusanya kodi na kulipa deni letu la njea, watu walilalamika kuwa sio vizuri. Leo hii deni la nje tumesamehewa baada ya kuona nia ya kulipa na kuheshimu madai yapo. tunapeta. Kuhusu TRA, taarifa ya IMF mwaka(iko kwenye website) ni kwamba TRA is outperforming expectations ukulinganisha na wakati wa Mzee Ruksa alipowasamehe matajiri kodi, watoa misaada wanaboreka kwani pesa wanayotumia kutupa misaada imetokana na kodi..taifa lolote lazima likusanye kodi, na hapo Bongo kwa serikali hiina Mkapa wamefanya vizuri, wanasifiwa..angalia hata CIA fact book. Kwa hiyo sulala watu wanalalama kisahihi ni kuwa haya makusanyo ni ya haki na yanatumika kuleta maendeleo ya nchi na wananchi wake? nadhani jibu ni kwamba sio..na hapo seriklai kuongea tu kodi ya mtoto bila kuonyesha gharama za kuzima moto wa magari( vijijini, mjini, barabarani nk) sio haki. wenzetu huku kama kodi umelipa ikazidi gharma inarudishwa..kwetu kiendecho kwa mganga..
    sasa kuna rafiki yangu mfanya biashara aliyelalama wakati wa awamu ya Mkapa kwamba "serikali imebana sana siku hizi faida za asilimia 300 hakuna tena!" sio mafisadi hao? nadhani serikali hii na itakayofuata wakiendelea hivi mambo yatakuwa mswano kodi lazima, mapata ya gesi yadhibitiwe iwe kwa faida ya taifa badala ya mafisadi nk..Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  6. Kaka Said naomba kujibu kwa nyongeza kwamba utamaduni wa serikali yetu kila wizara utakayoenda kuna mipango mizuri na minono ambayo haina tarehe ya kuanza. Hili ndilo suala la msingi tunaliongelea hapo juu. Ukiingia bungeni utasikia kila kiongozi lazima aseme" Mh Spika tathimini ya mradi huu imeanza chini ya usimamizi wa ofisi yangu hivi sasa tunasubiri fedha na wahisani" hutawahi kusikia kazi imeanza tarehe fulani na hivi sasa mafundi wako nachingwea kwenye stage fulani na mwisho wa wiki watamaliza daraja au bomba au nguzo au jengo. Why??????? kwa nini sisi tu tunashindwa kuanza? ukweli ni huu bwana said; Rais hawezi kuwepo nkila mahalikusimamia hivi vitu ndio maana ana wasaidizi. Hawa wasaidizi hawabanwi ili watekeleze majukumu yao. Nenda ofisi za serikali ndio utajua. utakuta watu wamekaa na makaratasi lundo mezani ya kutia sahihi. ukiuliza nini utaambiwa maombi ya likizo, uhamisho, ripoti magari na vifaa vya ofisi. sasa Mh Rais lazima awape hawa watu muda wa kudeliver kazi akishindwa basi abadilishwe awekwe mwingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...