JESHI la polisi Tanzania limetoa ajira 1,446 kwa Vijana wa kidato cha nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na vijana walioko kambi za JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani.

Kati ya hao 951 ni walio hitimu kidato cha nne na sita mwaka 2011/2012 na 495 kwa Vijana waliokuwa katika Kambi za JKT za JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani.

Maelekezo Muhimu:-
1. Vijana wa kidato cha nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na vijana walioko JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi baada ya mchakato wa usaili uliokamilika hivi karibuni wanatakiwa kuripoti Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi kati ya tarehe 06/10/2011 na 07/10/2012 kwa ajili ya zoezi la usajili litakaloanza chuoni hapo tarehe 8.10.2012.

2. Vijana hao wanatakiwa kuripoti tarehe 05/10/2012 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kwa ajili ya kuwaandalia usafiri wa kuwapeleka Chuoni.

3. Vijana wanaotoka katika makambi ya JKT yaliyotajwa hapo juu wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa mikoa iliyo karibu nao.

Vijana wa kidato cha nne na sita wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa waliojiandikisha wakati wa zoezi la usaili lililoendeshwa mwezi Julai, 2012.

4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Chuo cha Polisi Moshi

5. Vijana hawa wanatakiwa kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

a) Vyeti vyao vyote vya masomo(Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

b) Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c) Chandarua
d) Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e) Pasi ya Mkaa
f) Ndoo moja.1
g) Pesa kidogo ya kujikimu.

6. Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya mkononi, atakayepatikana na simu atafukuzwa chuoni hapo. Chuo kitaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.

7. Hakikisha jina lako liko kwenye orodha hii. Jeshi la Polisi
halitahusika na gharama zozote kwa atakaye kiuka maagizo haya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Jamani pasi ya mkaa. Give us a break. Polisi wanaishi karne ya 21. Kikwete waamshe hawa akina Said Mwema.

    ReplyDelete
  2. Wakimaliza wanakuwa majambazi!!

    ReplyDelete
  3. Naam, Duh pasi ya mkaa na hakuna simu ya mkononi balaa, afu ndoo ya moja inaonyesha wazi hapo maji ni utata hayatoshi, waboresheeni walinzi wetu wa usalama.

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  4. Yaani Tanzania baaaado ipo nyuma sana! sasa pasi ya mkaa na ndoo za nini jamani?au mashuka na uniform pia ni za nini?yaani serikali inashindwa kuwahudumia hawa watu na kuwanunulia hivyo vifaa jamani?wakati wabunge na mawaziri wanaiba tu pesa za kuchota!magari na majumba yao ya kifahari na huduma zote wanazipata buru!iweje washindwe kuwanunulia vitu vidogo kama pasi za umeme,ndoo na mashuka?Yaani nchi yetu inatia aibu sana,na inanuka rushwa na mafisadi!

    ReplyDelete
  5. Kwani ajabu mtu kwenda na vitu vyake mwenyewe? Hata ulaya wanafunzi/wanachuo kuna baadhi ya nchi unakabidhiwa chumba tu, hakina kitanda wala nini? Ni kuta, sakafu na makabati, ofcourse na choo na bafu, kisha wewe mwenyewe ndo unawajibika kuweka vitu unavyovihitaji. Sasa chuo kinunue mashuka kwa askari wanafunzi, kisha baada ya masomo ambayo huwa ni takribani miezi tisa wayatupe? Hapa ni busara kila mtu aende na vitu vyake. Nakubaliana na huu utaratibu. Kuhusu pasi ya mkaa na ndoo unaweza kukuta na nyenzo ya kujifunzia! Kwani mnajua syllabus ya huko polisi?

    ReplyDelete
  6. Asante sana mtoa maoni wa mwisho , wewe dume lenye mishipa , wacha hao vijidume soft wa UK kazi zao kuponda, eti pasi ya mkaa !! so what ?? pasi hizo zinatafutwa sana Ulaya na bei yake ni kubwa sana (antique) halafu kingine , bongo tunataka kuhifadhi hali ya hewa duniani .to prevent polution, kwa kutumia mali zetu za asili-siyo umeme,unaotokana na kuchoma mafuta na kuharibu dunia yetu. Hivyo jamani badala ya kushangilia utamduni huu wa gharama ndogo !!! mnalalama. Hovyooooo. Ndugu hapo juu wa august 22 saa 11:54.I wish i know your name, yaani wewe bomba hata huyo Mashaka anayesifiwa ,hakufikii kwa mawazo makali na ya kina, Bongo sasa hivi, viongozi tunao na nyie wazee ondokeni sasa madarakani.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  7. SIJAPENDA HUU UTARATIBU MPYA WA INTERVIEW YA SHORTLIST KATIKA MAJESHI YETU...INA ATTRACT KUPENDELEANA...NAKUMBUKA KIPINDI NINAJIUNGA NA JESHI LA POLISI(KWA SASA SIO ASKARI TENA)...KATIKA MKOA WANGU WA KAGERA TULIKUA TUNAKUSANYIKA VIJANA WOTE WENYE SIFA NA VYETI SAHIHI...BAADA YA KUKAGULIWA VYETI NA INTERVIEW YA MASWALI YA PAPO HAPO PAMOJA NA KUPIMWA AFYA NYOTE,THEN MNAKIMBIA MARATHON KUTOKA BUKOBA MJINI MPAKA KEMONDO WATU WOTE MLIOHUDHURIA THEN WALE MIA MOJA WA KWANZA KUVUKA KAMBA PALE KEMONDO NDIO WANAOCHUKULIWA NA KWENDA CCP...HAPO HAKUNA ANAELALAMIKA KWANI UNAJIENGUA HUKU UKIWASIFIA WENZAKO NA KUJIRUDIA NYUMBANI KUJIPANGA UPYA....SASA HAYA MAMBO YA SHORTLIST UNADHANI TANZANIA HII TUNA FORM FOUR LEAVER WANGAPI NA WOTE WANA SIFA HIZO...JE NI VIGEZO VIPI MMETUMIA KUWACHUJA WANAOFAA NA WASIOFAA?...HAPA TUNAJENGA JESHI LA KIJOMBA,KISHANGAZI NA KISHEMEJISHEMEJI...RUDIENI UTARATIBU WA ZAMANI BWANA..HAO SIO WAFANYAKAZI WA BENKI...By Mzalendo halisi.

    ReplyDelete
  8. safi sana...hii ni sawa na kwenda JANDONI.......wakirudi wote wamezubaaa.....safi sana.....walao tuna uhakika wa kupata watu safi................simu haziwasaidii....tafadhali wazazi tuunge mkonono jeshi la polisi.....haya mambo ya kuonyesha huruma sizizokuwa na maana kwa hawa watoto zimetutokea puani......HAYA FASTA WAHINI ENEO LA TUKIO.......nimefurahi sana SINA BUDGET.....habari ndiyo hiyo walao mmeshikwa pabaya!....BIG UP JESHI LA POLISI.

    ReplyDelete
  9. Jamani ebu msaidieni huyo zebebayo... eti kuprevent pollution?? wewe umesoma mpka langapi?? hujasoma athari za kukata miti na kutumia mkaa?? unajua athari za kutumia pasi ya Mkaa?? waulize waliosoma shuri tanga watakwambia.. yaani wewe ndo msahmba wa mwisho kabisaa

    ReplyDelete
  10. Maelekezo ya Muhimu:

    Kipengele No. 5 (e) Pasi ya mkaa,

    Sasa hili shariti ni 'Tambiko kwa Polisi kutumia pasi ya mkaa wakiwa mafunzoni' au mazoea au ndio Utaratibu?

    Kama ndio utaratibu kwa kigezo kipi ktk karne hii ya 21 sasa?

    ReplyDelete
  11. ANGALIZO:

    Pasi ya mkaa katika mafunzo ya u-Polisi:

    Asiyetumia pasi hiyo hataiva kwa mafunzo ya Kipolisi sawa sawa akipewa majukumu pindi akiwa kazini!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...