Kwako Ankal,

Habari za ujenzi wa taifa?

Naomba uniweke kwenye blogu yetu ya jamii nikigusia kidogo swala la lugha ya Kiingereza kwa Watanzania. Nilifuatilia maoni kwenye mchango wa ndugu yetu fulani kutoka Chuo na baadhi ya wachangiaji walionyesha kutokujali kwamba Kiingereza kilichoandikwa kilikuwa na mushkeli, walisema kwao message ikitumwa ndio muhimu zaidi.

Naelewa mijadala ya lugha imefanyika kabla kwenye blog hii na nyinginezo, ila ningependa nitilie mkazo hili kwa nia njema tu ya kumkomboa msomi wa Tanzania wa leo.

Ndugu zanguni Kiingereza ni muhimu (kama sio Lazima) kwa yeyote anayejiita msomi. English na Kiswahili ni lugha zinazotumika Tanzania, kwenye sheria, mahakamani, kwenye forms mbalimbali, kwa hiyo hili halikwepeki. 

Wengi wanadai eti unaweza kuwa msomi na utumie lugha ya Kiswahili peke yake, swali langu ni Je Chuo kikuu ulisomaje? Maana kozi  nyingi tu za chuo lugha ya kufundishia ni English, sasa wewe mwenzetu ulisoma vipi bila kuwa na uwezo wa kutosha wa kuongea, kuelewa na kuandika Kiingereza?
Kuna wale wanaosema kazi zao hazihitaji Kiingereza, kwa mfano ukiwa Daktari unatibu Watanzania Kiingereza cha nini? 

Kumbuka ukitaka kujiendeleza kielimu, kuhudhuruia semina na makongamano ya madaktari kutoka nchi mbalimbali, ukitaka kuandika academic paper/report ya fani yako ikasomwa na watu nje ya Tanzania basi utafanya hivyo kwa lugha ya Kiingereza, bila hivyo itabidi utafsiri 'medical terms ' kwa Kiswahili na ni kazi hasa.

Jamani tusidanganywe na wachache wanaotaka tubaki nyuma ili wao waimege nchi yetu na kuiuza vipande vipande. Wengi wanaosema hatuhitaji Kiingereza wala lugha zingine za wakoloni wenyewe wamesoma tayari, lugha hizo wanazijua vizuri ndio maana wanaweza kuzitumia kwa manufaa yao.Watoto wao wanawasomesha aidha English Medium humu nchini au nje. 

Nia yao wengi tubaki nyuma ili wawapendelee watoto wao na ndugu zao. Wasomi waleo vijana msikubali kurudishwa nyuma jifunzeni Kiingereza,Kifaransa,Kiarabu na Kiswahili fasaha. Lugha siku zote ni ya manufaa, ukiijua inakuongezea ushindani,kielimu, kikazi na kibiashara. Hii ni dunia ya utandawazi, hakuna kizazi cha action bila lugha.

 Ukitaka kusoma nje wanakwambia ufanye mitihani ya lugha ni kwanini? Tusijilinganishe na wageni eti mbona Wachina hawaongei Kiingereza? Watanzania sio Wachina. Hatuwezi kujilinganisha kiuchumi na nafasi inayoshikiliwa na China duniani. Tutajidanganya.

Ukitaka kufanikiwa katika maisha, jitahidi kujifunza lugha. Kuongea maneno machache ya kiingereza ukichanganya na Kiswahili sio Kiingereza wala sio Kiswahili. Jifunzeni lugha moja ikamilike halafu unajifunza nyingine.  Huu ndugu zangu ni ushauri wa bure. 

Tutabaki nyuma, tutabaguliwa kwenye Umoja wa Afrika Mashariki, kama tutabaki nyuma katika lugha rasmi ya jumuiya. Ni kweli asili ya English ni Ukoloni wa Waingereza, lakini mbona WaMarekani wanatumia lugha hiyo kwa mafanikio tu? Je asili ya Kiswahili ni Afrika? Tuchangamkie tenda wajameni wakati ni sasa.

Asante Ankal

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Mimi nakuunga mkono wewe ulieandika hii maada. Kwakweli niaibu... hata huku ugabuni wakenya wanajitahidi kushinda hata watanzania... utamuona mtanzania katulia kimya kwenye mijadala, madarasani na sehemu mbalimbali.... shida ikiwa nikiingereza. Akikutana na wabongo au wakenya yeye mstari wa mbele kuchangia maana... kwavile nikishwahili kinatumika. Kweli nanchi ingalie nijinsi gani inaweza kuhamasisha lugha hii ya kiingereza. Bongo kunawatu wenye uwezo mkubwa sana lakini lugha inawakwamisha. Hata kwenye maolimpikis hawawezi kuhudhuria kutokana na lugha. Asante sana!!

    ReplyDelete
  2. Mwambieni genius wenu Jonhi mashaka naye ajifunze kiswahili. atakuwaje msomi tena kiongozi mtarajiwa humu nchini bila kufahamu kiswahili. akija kuwa rais alafu aende huko bukoba ataongea lugha ghani na wapiga kura wake?

    ReplyDelete
  3. Tatizo kubwa ni kuwa idadi kubwa ya walimu wanaofundisha kiingereza hawajui kingereza. Yaani kama ni mpira wa miguu tungesema Refa kipofu, laizimeni kiziwi. Kuna ambao wanasema mbona Japan hawaongei kingereza na wameendelea? Kijapani kinatumika katika sehemu kubwa ya elimu yao. Kwahiyo tukitaka kujifananisha na wajapani au wajerumani, basi tutafsiri sheria na vitabu vyetu vya kufundishia kutoka kingereza kwenda kiswahili. Hapo ndipo tutakapoanza kuchekesha kwa mifano ifuatayo:
    Organization = oganaizesheni
    analog = analogia
    number = nambari
    marching guy = machinga
    spark = sipaki
    Ipo mifano mingine mingi kama baiologia, fizikia,teknolojia na kemia ambayo inatudhihirishia kuwa kiswahili kina maneno machache ukilinganisha na kingereza au kijapani. Kwahiyo badala ya kutafsiri, tunaanza kuchekesha. Ukienda kwenye sheria, tafsiri ya aina hiyo inaweza kuwatia hatianai watu ambao hawana hatia. Kwavile tunakaribisha wawekezaji kutoka mataifa ya magharibi, tutaendelea kuwa outcompited na majirani zetu kama hatukupata bahati ya kusoma nje. Tukitaka maendeleo ya kweli lazima tufamu kingereza na kiswahili.

    ReplyDelete
  4. Wabongo wengi tunamatatizo na lugha ya kiingereza, it is the language of our former masters, na ukiipigia debe jamaa wasema...ni ugumu wa kukata minyororo ya utumwa.This language now is universal na sijui kama waweza kwenda mbali kimataifa kama hujui hii lugha, ni lugha ya computer na internet, air travel,international trade,banking,tourism na kadhalika.Miye naona ingekuwa compulsory kufundishwa kwenye shule zote bongo mwanzo sana wa elimu ya vijana.Wenzetu wafanya sana bidii kujifunza hii lugha.Nilikaa hoteli moja hapa ukerewe na karibu waiters wote walikuwa ni college students from eastern europe walioletwa hapa kujifunza lugha.SISI chelewachewa kama kawaida.

    ReplyDelete
  5. KAENI MKIJUA YA KUWA:

    KUJUA AU KUTUMIA KIINGEREZA SIO KIGEZO CHA KUELIMIKA!

    Naongelea suala hili nikisema sawa Kiingereza ni muhimu ili kuitwa Msomi kimataifa ni vile ni Lugha inayozungumzwa na wengi zaidi Duniani kuliko lugha ingine yeyote, UMUHIMU WAKE UNABAKIA KWA DHANA HIYO TU.

    NAKATAA KUWA KUJUA KIINGEREZA SIO KIGEZO CHA KUWA NDIO UMEELIMIKA ZAIDI AU KUWA NDIO UNA UELEWA ZAIDI AU NDIO AKILI ZAIDI KWA SABABU:

    1.NCHI ZILIZOENDELEA ZOTE SIO ZINAZOTUMIA KIINGEREZA KAMA LUGHA KUU MFANO:
    -JAPAN
    -UJERUMANI
    -CHINA
    -UFARANSA
    -URUSI
    -ITALIA
    -UHOLANZI
    -ISRAEL
    -IRAN
    NA NYINGINEZO,

    Kwanza kwa Mjerumani au Mjapan alivyokuwa jeuri na kiburi ukimsemesha kwa Kiingereza yeye anakujibu kwa lugha yake !

    Akikufahamisha ya kuwa anakuelewa lakini anakueleza kuwa lugha yake ni mihumu zaidi pia.

    2.WAPO WENGI TU WASIOTUMIA LUGHA YA KIINGEREZA WALA KUKIFAHAMU LAKINI WAKAWA NA FIKRA NZURI NA ZENYE FAIDA NA AKILI YA HALI YA JUU.

    3.KUHUSU LUGHA YA KIINGEREZA:
    ILI UITWE UNAFAHAMU LUGHA YA KIINGEREZA AU LUGHA YEYOTE NI LAZIMA UWE NA VIGEZO HIVI:

    YOU MUST BE ABLE TO DEMOSTRATE THE FOLLOWING:

    (i)WRITING SKILLS AND READING
    (ii)SPEAKING AND INTERPRETING
    (iii)LISTENING AND COMPREHENSION

    SASA WALE WALIOSHINDWA KUMUEELEWA MSOMI WA CHUO KIKUU PAMOJA NA KUWA LUGHA YAKE ILIKUWA MBOVU NDIO WALIO DEMSOSTRATE UDHAIFU WA KUILEWA LUGHA KWA SABABU MUELEWA WA LUGHA YA KIINGEREZA ANATAKIWA AWE NA UWEZO WA KUMUELEWA HATA ANAEONGEA BROCKEN ENGLISH.

    NA HIYO NDIO KAZI AMBAYO HATA WAKALIMANI WA KIMATAIFA WANAIFANYA KWA LUGHA TOFAUTI ACHILIA MBALI HIYO ENGLISH !!!

    ZINGATIENI HAYO MATATU (3)HAPO JUU:

    Mimi Mdau,

    E-mail:mohamedtzn@AOL.COM

    ReplyDelete
  6. BABA WA TAIFA LETU MWALIIMU J.K. NYERERE ALIKUWA NI MSOMI. ALIONGEA KIINGEREZA VIZURI NA KISWAHILI NA LUGHA NYINGINE.ALIWACHUKIA WAKOLONI NA KUWAFUKUZA NCHINI ILA LUGHA YAO ALIJIFUNZA KWA UFASAHA. KWANINI TUSIIGE MFANO WAKE? TUKIKAZANIA KISWAHILI PEKEE TUTAONGEA VIPI NA WAGENI WANAOKUJA KUPATA UZOEFU NCHINI? JE KAMA UNAUWEZO MKUBWA KITAALUMA, UTAUELEZA VIPI DUNIANI?
    BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LINAENDESHWA KWA LUGHA MBILI ENGLISH NA KISWAHILI, MAGAZETI YA TANZANIA NI LUGHA MBILI. WAKENYA AKIMALIZA FORM FOUR ANAONGEA KIINGEREZA VIZURI. SISI CHUO BADO TUNABAHATISHA

    ReplyDelete
  7. kiingereza muhimu. Waalimu wa Bongo wanalalamika hawapati kazi kwenye shule za English medium pamoja na kuwa na degree zao, waalimu toka Kenya wanaajiriwa, kisa ni lugha tu.
    Mbona Benki transaction zote ni Kiingereza na hatulalamiki? nani aliwahi kupewa mkopo benki wenye maelezo ya Kiswahili? Unafikiri mikataba ya Richmond iliandikwa Kiswahili? Tukizubaa itakula kwetu. Mimi naanza English Kozi Jumatatu

    ReplyDelete
  8. Watanzania wabishi sana.
    Hamna nchi inayolazimisha mtu kutumia kiingereza au lugha fulani kujielezea.
    Kuna wakalimani kibao siku hizi tena Wazungu wamegunduwa wakihitaji ujuzi wa mtu wanamtafutia na mkalimani wao tena mzungu siyo mswahili.
    Heshimuni mawazo ya watu.
    Hamna haja ya kukosowa wasomi wetu kwamba hawajuwi Kiingereza.
    Mtanzania anayejuwa Tanzania haitaji Kiingereza nchi nyingi tu wasomi wake hawajuwi kiingereza na wanatushinda kwenye kuwasilisha mambo yao na yakaeleweka.
    Unahiaki ya kutoa hoja ila firikiria huu si wakati wa kudanganya watu.

    Tusiwadharau waswahili alafu tunawatumia kwenye kujipatia shibe na kuwadanganya tunawaheshimu.

    Kuna Waingereza kibao wanajuwa kiingereza na ni mambumbumbu wako mtaani wanaumia.

    ReplyDelete
  9. Kiingereza ni muhimu duniani kwa sasa.Tena na Kifaransa ambacho sisi tunakidharau.Kwa ufupi kama alivyosema mkubwa mmoja hapo juu...LUGHA.Kufahamu lugha tofauti ni kitu muhimu sana.Ni hayo tu

    David V

    ReplyDelete
  10. MDAU HAPO JUU ACHA KUTETEA UTUMBO AU NDIO KIBONDWE MWENYEWE? KIINGEREZA KILICHOANDIKWA KILIKUWA KIBOVU,FULL STOP. UMEWAHI KUANGALIA TV PALE WANAPOONGEA KIINGEREZA KIBOVU CHENYE ACCENT WANAWEKA SUB-TITLES? KIBONDWE ALIHITAJI SUB_TITLES ILI AELEWEKE. UBISHI UTATUUA BANDUGU

    (i)WRITING SKILLS AND READING
    (ii)SPEAKING AND INTERPRETING
    (iii)LISTENING AND COMPREHENSION

    SASA WALE WALIOSHINDWA KUMUEELEWA MSOMI WA CHUO KIKUU PAMOJA NA KUWA LUGHA YAKE ILIKUWA MBOVU NDIO WALIO DEMSOSTRATE UDHAIFU WA KUILEWA LUGHA KWA SABABU MUELEWA WA LUGHA YA KIINGEREZA ANATAKIWA AWE NA UWEZO WA KUMUELEWA HATA ANAEONGEA BROCKEN ENGLISH.

    ReplyDelete



  11. NDUGU WADAU.
    NAPENDA KUUNGA MKONO KUWA KUONGEA KINGEREZA NI MUHIMU SAAANA KATIKA KUELIMIKA NA MAENDELEO...FACT. UKIJUA ZAIDI YA KIINGEREZA NI FAIDA YA ZIADA. PILI NAPENDA KUMREKEBISHA ANONYMOUS WA E-mail:mohamedtzn@AOL.COM KUWA SIO KWELI KUWA KINGEREZA NDIO KINAONGEWA NA WATU WENGI DUNIANI..WRONG WRONG WALA SIO CHA PILI...TAFADHALI USITOE TAARIFA AMBAYO HUNA UHAKIKA NAYO. LUGHA INAYOONGEWA NA WATU WENGI KULIKO WOTE DUNIANI NI KISPANIOLA.

    TATU HUYO HUYO MDAU ANAFANYA ANALYSIS NUSU. NCHI ALIZOZITAJA KUWA KIINGEREZA SIO LUGHA NAMBA MOJA NI KWELI LAKINI HAKUWAAMBIA WATU KUWA KUANZIA PRIMARY MPAKA UNIVERSITY KARIBU ZOTE ZA NCHI HIZO ZINAFUNDISHA KIINGEREZA KWA HALI YA JUU SANA. NDIO MAANA HATA WATAALAMU WANATOKA NCHI HIZO WANAONGEA KIINGEREZA KIZURI.

    MIMI KWA MAONI YANGU NI KUWA ..KUWA MSOMI NI PAMOJA NA KUFANYA VITU KWA USAHIHI. KAMA UNAFUNDISHWA KINGEREZA AU KISWAHILI HADI CHUO KIKUU ALAFU HUONGEI VIZURI KAMA YULE MTOA MADA...SASA USOMI WAKO UKO WAPI?? UTAJIELEZAJE MBELE YA MATAIFA MENGINE????
    NI HAYO KWA SASA

    NI MIMI MDAU WA ARDHI

    ReplyDelete
  12. nafikiri tusilaumu watu wazima wasio jua kiingereza. tujadili ni namna gani kizazi kijacho kitabadilika, katika umri tulionao wengi tumeshachemsha. tatizo ni walimu na mifumo ya elimu. sasa tuanzie hapo basi. pia mdau uliejaribu kutoa tafsiri mbalimbali ya maneno ya kiingereza kwenye kiswahili jua kuwa "machinga" sio "marching guy". umejitungia mwenyewe hiyo tafsiri. tafiti kwanza kabla ya kujianika

    ReplyDelete
  13. Asanteni Kwa maoni yote katika hoja hii. Ninakubaliana na mdau hapo juu wa 11:40:00AM. Tunahitaji suluhisho kwa sasa ilikuwakomboa hao walioko mashuleni leo na wasomi wa baadae. Hatua ya kwanza ni kukubali kwamba Tunahitaji Kiingereza na Kiswahili fasaha kwa kuanzia; pili kujiuliza tatizo lipo wapi kwenye mfumo wa elimu ya TZ kuanzia vyuo vya ualimu wanakosomea waalimu wetu hadi mashuleni msingi- sekondari. Je Waalimu wanaofundisha kiigereza wenyewe lugha hiyo wanaiongea? uwezo wao ukoja? Je Mwanafunzi anapewa changamoto kuelewa na kuongea lugha hiyo? au anakatishwa tamaa na kutishiwa kwa viboko anapokosea? Je kuna english debate club za kutosha? je vitabu vya kujisomea wanafunzi vipo? Wanapofika nyumbani je wazazi wanatoa support gani - hata kama mzazi haongei kiingereza amruhusu mwanafunzi agalau asikilize BBC World in English - ili ajiendeleze nyumbani; kama mzazi unaongea lugha basi weka nusu saa ya kumchangamsha mwanao kwa kiingereza. ongea nae kitu chochote kuhusu mapishi, michezo, chochote ambacho mnachagua wenyewe ili tu umpe moyo na kumsahihisha kupima maendeleo yake.
    Akifika Chuo Kikuu tena ningependekeza compulsory English course kwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza. Ikiwezekana waalimu waandaliwe kwenye nchi zinazoongea Kiingereza kama UK, Australi, New Zealand etc ili waielewe lugha vizuri na kama haiwezekani basi chuo kitafute volunteers kutoka nchi hizo. Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akipasi English aweze kuongea vizuri na kuandika na kusoma basi apewe cheti cha language certification kuonyesha kwamba amefaulu mtihani wa Kiingereza uliofundishwa na certified Teacher. Namna hii basi itasaidia kujiandaa kufanya mitihani mingine ya Kiingereza na pia kujiunga na vyuo vya nje.
    Naishia hapa kwa sasa ila kwa ushauri zaidi nipo tayari kuchangia ili kuboresha ma graduates wa Tanzania.
    Asanteni

    ReplyDelete
  14. FANYENI UBISHI WENU LAKINI MUELEWE YA KUWA KUTUMIA ENGLISH AU KUJUA ENGLISH SIO KIGEZO CHA KUELIMIKA!

    <<<<>>>>

    PANA ILE KABILA MOJA YA KANDA YA ZIWA AMBAYO HATA KAMA KIINGEREZA CHAKO NI BROCKEN ILI MRADI KILA BAADA YA NENO MOJA UNAINGIZA NENO LA KIINGEREZA HATA LISILO STAHILI, LAKINI KWAO UNAONEKANA NDIO UMEELIMIKA!

    SIO SAHIHI KUWA UNAPOTOA MAONI KWA KIINGEREZA NDIO WEWE NI MTAALAMU SANA AMA FIKRA ZAKO NI SAHIHI KWA KIWANGO CHA JUU CHA USOMI.

    PANA WATU WANAOTUMIA LUGHA ZINGINE KAMA MDAU ALIYETAJA JUU WA NCHI ZINGINE LAKINI WAMETOA MCHANGO MKUBWA SANA DUNIANI.

    TUNACHOWEZA KUKUBALI NI KUWA MKOLONI MWINGEREZA ALIPIGANIA SANA MTAALA WA MAFUNZO NA TAALUMA UWE KTK LUGHA YAKE NA NDIO MAANA MACHAPISHO MENGI YA KIMASOMO DUNIANI NI YA KIINGEREZA HILO NDIO WALIWEZA KUWAHI NA NDIO MAANA HATA NINYI WASOMI WA TANZANIA-BONGO TAMBARALE MMEWEKA DHANA KUWA KUTUMIA AMA KUJUA ENGLISH NDIO KIGEZO CHA KUELIMIKA...SIO KWELI!!!

    HATA HAO MNAOSEMA WA NCHI ZINGINE NDIO WANAJIFUNZA KIINGERZA NA WANAONGEA KIINGEREZA KIZURI LAKINI NI KWA MALENGO (YA KUWEZA KUWAFIKIA NA KUBADILISHANA MAWAZO NA WENGINE DUNAINI KWA UFANISI) HUKU UMUHIMU MKUBWA UKIWA NI LUGHA YAO YA KWANZA.

    KWA MSINGI HUO HATA SISI TANZANIA TUNAWEZA KUPITIA 'DIRISHA DOGO' KUINGIA KUKUBALIKA DUNIANI KAMA TUTATUMIA KISWAHILI CHETU KIKAENEA KWA KUTIMILIKA DUNIANI.

    HIVYO LUGHA ZA KIGENI (ENGLISH) NI MUHIMU LAKINI LUGHA YA KWANZA NI MUHIMU PIA!!!

    ReplyDelete
  15. Kiingereza kwa sana sio kigezo cha kuelimika !

    Kiingereza kwa sana sio kigezo cha kuwa na akili nyingi !

    Kiingereza kwa sana sio kuwa ndio kigezo cha kuwa na fikra za maana!

    PANA WALE NDUGU ZETU WAMEKUWA NA DHANA KUWA KUWASOMESHA WATOTO NCHI JIRANI KENYA, UGANDA KWENYE KIWANGO CHA JUU CHA KIINGEREZA NDIO KUELEIMIKA.

    YOTE HAYA NI MAWAZO KAMA YA WADAU WENGI HUMU WANAOTETEA KIINGEREZA KUWA NI SAWA NA WAZAZI WANAOSOMSHA WATOTO WAO NCHI JIRANI HUKO KWENYE KIINGEREZA WAKIFIKIRI KUTUMIA KIINGEREZA MASOMINI NDIO KUELIMIKA ZAIDI!

    HIO SIYO KWA SABABU IMEONYESHA UBOVU MKUBWA WA MTAALA KWA NCHI HIZO JIRANI NA KUWA MTOTO ANAHITIMU KTK UONGEAJI WA KIINGEREZA TU WAKATI TAALUMA AKIWA SIFURI!!!

    ReplyDelete
  16. Mfanye msisitizo zaidi kwenye lugha yenu ya Kiswahili kwanza,,,halafu ndio mkurupukie lugha ya Mkoloni wenu ambayo kwa sasa sio yenu ni ya wenzenu!

    Inakuwaje mnasisitiza zaidi Kiingereza cha wenzenu wakati Kiswahili Fasaha hamjui?

    ReplyDelete
  17. Wasomi wa Kibongo,

    KIBONDEZZZ MSOMI WA UDOM AMEWATOA KAMASI NA ENGLISH YAKE BOMU, JE MTAMWELEWA MNYAMWEZI WA NEW YORK ANAYEMWAGA SLYING ENGLISH???

    English mnaitilia mkazo sana, je vipi lugha zenu za Makabila mmefanya jitihada gani ziwe juu?

    JINGINE ACHENI UPUMBAVU KABISA KUJUA KIINGEREZA AMA KUTUMIA KIINGEREZA SIO KIGEZO CHA KUELIMIKA!

    ACHENI UBWEGE NA UBISHI WENU!

    MTU MWELEWA WA KIINGEREZA ANATAKIWA AWE NA UWEZO WA KUMWELEWA ANAYEINGEA BROCKEN ENGLISH,,,SIO NINYI WENYE KIINGEREZA CHA KUKREMU NDIO MAANA MSOMI KIBONDEZZZ NA ENGLISH YAKE MBOVU AMEWATOA KAMASI HAMKUMPATA KABISA AMEWAACHA HEWANI.

    JIFUNZENI NINYI KIINGEREZA ZAIDI ILI MUWEZE KUWAELEWA WASISEMA KIINGEREZA FASAHA!

    MPO HAPO?

    ReplyDelete
  18. Wewe Msomi wa Manzese English ya Mnyalukolo ya kuunganisha unganisha umeshindwa kumuelewa Mnyalu mwenzio,

    Je, English ya Muitaliano ya kupapasa mtaiweza?

    Je, English ya Mnyamwezi wa New Jersey ya kuuma maneno mtaiweza?

    Wasomi wa Kibongo English ninyi wenyewe hamna kabisa, ndio maana wengi mkienda ktk Mikutano mingi wawakilishi wetu mnatoka sifuri juu ya kilichozungumzwa huko.

    Ndio maana ktk Mikataba mara zote tinapigwa kwa kuwa ninyi Wasomi English ni tatizo pia kwenu msimcheke Msomi Denti wa UDOM,,,!!!

    ReplyDelete
  19. MDAU WA ARDHI ANONYMOUS WA Sun Sep 30, 10:49:00 AM 2012

    ...LUGHA INAYOONGEWA NA WENGI DUNIANI NI KISPANIOLA...(HIYO NI MUWONGO NA WEWE NDIO UNAPOTOSHA WATU UKWELI)...

    NATAKA TWENDE KWA TAKWIMU:

    MASWALI:

    1.JE NI MKOLONI GANI AMETAWALA SANA NCHI NYINGI ZA DUNIA KATI YA MUINGEREZA NA MSPANIOLA?

    TUCHUKULIE AFRIKA YETU KWANZA

    Mwingereza:
    -TANZANIA
    -KENYA
    -MALAWI
    -UGANDA
    -ZIMBWABWE
    -NIGERIA
    -GHANA
    -SIERRA LEONE
    -MISRI

    NA ZINGINE:

    Mfaransa
    -CONGO DRC
    -RWANDA
    -BURUNDI
    -DJIBOUT
    -SENEGAL
    -GUINEA
    -CENTRAL AFRICA

    NA zingine,

    Spainiola:
    Ni nchi zipi alitawala ktk Africa?...JIBU UTUPE WEWE !

    2.JE MSPANIOLA ANA KITU KAMA ALIYONAYO MWINGEREZA ''COMMONWEALTH''?

    3.JE KAMA KISPANIOLA NI LUGHA INAYOZUNGUMZWA NA WENGI ZAIDI WAKATI WAKIWA HAWANA MAMLAKA YA KIKOLONI KAMA ALIYONAYO MWINGEREZA YA COMMONWEALTH ,,VIPI MFARANSA MWENYE FRANCOPHONE UMEMWEKA WAPI?

    KWA TAARIFA HIYO FUPI NI DHAHIRI MWINGEREZA ANA MAKOLONI MENGI ZAIDI NA AMEACHA ATHARI YA LUGHA YAKE SEHEMU ZOTE ALIZOTAWALA , HIVYO ENGLISH NDIO LUGHA INAYOZUNGUMZWA SEHEMU KUBWA DUNIANI.

    WEWE NDIO UNAPOTOSHA KWA KUTOA TAARIFA ZIZISO NA UHAKIKA:

    ReplyDelete
  20. Sun Sep 30, 10:49:00 AM 2012

    MDAU WA ARDHI NA KIBONDEZZZ WA UDOM MPO SAWASAWA WOTE VILAZA!

    WEWE UNASOMA ARDHI UNIVERSITY INA MAANA UMESOMA JIOGRAFIA, UNATAKA KUDANGANYA WATU HAPA KUWA ...SPANIOLA NDIO LUGHA INAYOONGEWA NA WENGI DUNIANI?

    TOA TAKWIMU: TAJA NCHI DUNIA NZIMA NA IDADI YA WATU BAINA YA ENGLISH NA SPANISH TUONE !

    AMA KWELI KAMA JAMAA WA UDOM NI KIBONDEZZZ NA WEWE WA ARDHI UNIVERSITY NI KILAZAZZZ !!!

    ReplyDelete
  21. WASIOELEWA KIINGEREZA UTAWAJUA TU. MTABAKI UBISHI TU FORMS MJAZIWE NA WENZENU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...