Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa siku 3 kwa walimu wa nchi za Afrika unaojadili kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wawakilishi wa walimu kutoka Kenya waliohudhuria mkutano wa saba wa ACP unaojadili kuhusu kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi saba za Afrika mathalani zile zinazotumia lugha ya Kiingereza umefunguliwa leo na Makamu wa Rais katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga walimu kutoka nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa 7 wa ACP,unaojadili kuhusu maboresho ya Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo na Mheshimiwa Makamu wa Rais na unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika hususani zile zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji.Picha na OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...