Mtambo wa kuchimbia madini ambao Raia wa China walikamatwa wakiutumia katika pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkansi kinyume cha sheria.Raia huyu wa china amehukumiwa kulipa faini na kuamriwa kuondoa mtambo huo katika pori hilo.
Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.(Picha/ Tabu Ndziku).

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .


Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya, mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.


Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.


Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.


Taarifa hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba. Aidha Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.


Chaoxian Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai 25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa huru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Mungu wangu! shamba la BIBI TZ.! yaani mgeni aje, aweke machine na achimbe pori la akiba kisha alipe faini ya Tumilioni tumoja? kweli wabongo tunajidharaulisha saaaana!
    Sie tunaweza kufanya hivyo kwao?

    AIBU kwa HAKIMU, POLISI na woote waliohusika!

    ReplyDelete
  2. MalcolmX

    Habari Ankal Michuzi!

    Kama kuna kitu ambacho kinasikitisha ni jinsi tulivyopumpazika katika kusimamia rasilimali zetu! Yaani mtu anakuja nchini, anaingiza mitambo, anavamia pori la akiba, anaweka miundombinu na kuanza kuchimba madini halafu mnapomshtukia kwa kupewa taarifa na good samaritan wa nchi hii! mnampeleka mahakamani halafu mnamtoza faini ya Shilingi Milioni Moja na Ushee za kitanzania! Ewe Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Neema, Mwenye kuneemesha neema ndogondogo na kubwakubwa! Naomba utupatie viongozi wenye busara na uchungu na nchi hii ili angalau vizazi vyetu vipate kubakiwa na urithi wa maliasili na rasilimali lukuki zilizopo nchi hii! Kwa taarifa yako tu ni kwamba Tanganyika ni nchi ya tatu kwa kuwa na rasilimali na maliasili za kutosha kuondoa umaskini wa aina yeyote uujuaye wewe msomaji! Ikianza na Congo (DRC); South Africa halafu sisi Tanganyika! Lakini tunashindwa na vijinchi visivyo hata na rasilimali moja ambayo sisi tunayo!! Kulikoni? Lazima tujiulize na tuchukue hatua madhubuti za kulinda rasilimali zetu dhidi ya waporaji hawa wanaojifanya ni ndugu zetu kumbe kikulacho ki nguoni mwako! |Amen

    Shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  3. SI KOSA LA HAKIMU WALA POLISI NI LA SHERIA,at least sheria ingesema jela au faini ya milioni mia moja(100),lakini hako kamilioni 1 ni utani tu,kila mgeni atakuja atachimba akikakamatwa analipa mambo kwisha, anaenda kwao kula bata miaka kibao anampisha mwenzake, naye vile vile atalipa maisha yanaenda,TUNABAKI HOHE HAHE TU .

    ReplyDelete
  4. HII ni kazi ya kijinga leo unaweza kuchimba madini china bila kibali then unafikiri utalipa fine tu,huyu kwanza kibali chake cha kuishi nchini kilitakiwa kufutwa,then jela miaka kumi kwa kuvamia eneo la hifadhi,hakimu lazima kalamba millioni tano kwa kosa ili na serikali imepata hiyo fine ya kijinga,tokalini mtu anaweka mitambo na kuanza kuchimba na kuna kamati ya ulinzi kila mkoa na wilaya hao watu wamelala?kama mdau alivyosema kweli bongo shamba la bibi,mchina ametoka hapo atakwenda sehemu nyingine anachimba madini ya million 50 na fine ya two million ndio atadaiwa atafanya tu mradi huo.

    ReplyDelete
  5. mitambo kwa nini isitaifishwe kama meli ya samaki wa Maghufuli ili itumiwe na halmashauri ya Nkasi kuchimba madini ktk eneo linaloruhusiwa kisheria?

    Mdau
    arumeru

    ReplyDelete
  6. Rushwa at work. Aliingia kama muuza maua sasa amegeuka mchimba madini.

    Na utashangaa anaendelea kudunda mitaa ya keko akitafuta biashara nyingine.

    ReplyDelete
  7. Hongera Mchina kwa kuwaamsha WTZ ambao bado wamelala. Nyerere alisema: "Uchumi mnao, lakini bado mnaikalia". Heko Mchina, fundisha kazi Wabongo!

    ReplyDelete
  8. Serikali iko bizzi kukamata raia zake wakiuza maandazi kwa ajili ya kulisha familia lakini wachina faini ni milioni moja? kwanini isiwe milioni 100 kusudi waheshimu nchi yetu? ivi serikalòi iko wapiu wajamaa

    ReplyDelete
  9. Asante mchina kwa kutuibia maana hata usingeiba wewe basi waTZ wenzetu wachache wangeiba tu na hata tusingejau kwamba hapo pamewahi kua na madini. Tunaibiwa na tutaibiwa hadi tutembelee vichwa.

    ReplyDelete
  10. Yaani hapo wachina wamewashtua madudu mtu kuwa kuna dili huko, chekishia yatakavyopavamia kama viwavi jeshi.

    ReplyDelete
  11. Yaani naisoma hii habari kwa masikitiko makubwa na uchungu.
    Huyo jamaa angetakiwa kua deported na asikanyage nchi hii mpaka baada ya miaka 10 na mitambo ingetaifishwa.
    Hata sielewi ni sheria ndio zinasema hivyo, kwa adhabu aliyopewa?!. Wanaposemaga kua "hakimu ametoa adhabu hiyo kali ili iwe fundisho kwa wengine" wanakua wametumia kipengele gani cha sheria?!

    ReplyDelete

  12. Hawajaanza leo hao!

    Wakati wanajenga TAZARA walikuwa wanachukua udongo na mchanga kwa matani wanapakia kwenye meli wanapeleka mchanga kwao, wakiulizwa? ni "mzuri" kila kitu kinakubali.

    Kumbuka, reli imepita kwenye maeneo mengi sana yenye madini.

    ReplyDelete
  13. Ilitakiwa sample ya mchanga na tope kwa madini yaliyopatikana ijulikane na ndio thamani ya madini itafahamika na kiwango cha Faini kujulikana.

    Kwa nini kesi hiyo ipelekwe kwa kasi kiasi hicho?

    Hivi Hakimu anao uwezo wa kutathimini thamani za madini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...