Mapema akihutubia katika mkutano wa Saba wa Maspika wanawake duniani Spika Anne Makinda aliwaambia wajumbe kuwa wabunge wanawake Tanzania ni 36% jambo ambalo lilifanya Tanzania kusifiwa na kushauriwa kusonga mbele hadi 50%.
Rais wa Inter-Parliamentary Union (IPU), Bw. Abdelwahad Radi (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Anders Johnsson ni miongoni mwa viongozi mashuhuri waliohudhuria mkutano huo unaosisitiza wanawake kupewa nafasi zaidi katika vyombo vya maamuzi.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini India, Engineer John Kijazi, wakati wakuingi a katika ukumbi wa utamaduni wa Kihindi katika viwanja vya Bunge la India mjini New Delhi.
Wakiwa kwenye vazi maalumu waliloandaliwa, kutoka kulia ni Spika wa Bunge la India na mwenyeji wa mkutano wa Saba wa Maspika wanawake duniani Mhe. Meira Kumar, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na spika wa Bunge la Swaziland Mhe Gelane T. Zwane.
Picha ya pamoja ya baadhi ya maspika wanawake wa IPU ndani ya vazi maalumu waliloandaliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. umependeza sana maa bora uwe mdosi kabisa mkuu wetu mheshimiwa spika ha ha ha

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa vazi la SARI limekutowa, that's nice! Kwa kweli umependeza mithili una asili nalo. Nawapongeza pia waandaji wa vazi hilo katika mkutano huo.

    ReplyDelete
  3. umependeza sana na vazi letu la taifa au walalahoi mnasemaje tulikubali kuwa vazi la taifa?

    ReplyDelete
  4. Mdau wa tatu hapo juu, Hilo siyo vazi letu letu la Taifa, ni vazi la wenzetu huko Sub-continent na jirani zao nchini Sri-Lanka. Sasa kama umeliita vazi letu la Taifa kuna haja gani ya kutuuliza walala hoi? Hovyooo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...