Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Othman Chande yuko ziarani
nchini Marekani ziara ambayo imejumuisha Majaji Wakuu wengine kutoka
Afrika Kusini,Ghana,Namibia,Zanmbia,Malawi,Kenya,Uganda na
Msumbiji, Ziara hii ya aina yake imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje
ya Marekani na madhumuni yake makubwa ni kujionea jinsi mfumo wa Sheria
na Utoaji Haki katika mahakama vinafanya kazi pamoja na maeneo ya
Utawala Bora. Katika ziara hii Jaji Mkuu Chande ametembelea mahakama ya
Rufaa ya Marekani jijini Washington DC pamoja na Chuo Endelevu cha
Majaji Chicago na leo hii alionana na Mhe.Hilary Clinton, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani pamoja na Majaji wengine waalikwa na kuwa na
mazungumzo nae katika Wizara ya Nje ya Marekani Washington DC.
Mhe.Mohamed Othman Chande PIA alipata wasaa wa kutembelea Ubalozi wa Tanzania Washington DC.Katika picha Mhe. Chande akipokelewa na Bw. Suleiman Saleh,Afisa
Ubalozi wa Tanzania Washington DC na pia akisaini kitabu caha wageni
Ubalozini hapo. Mhe.Chande akiwa na Bw.Suleiman Saleh mara baada ya
kumaliza ziara yake Ubalozini.
Katika tovuti ya Ubalozi wetu uliopo Washington, kuna maelezo ya kuwa Watanzania waliopo Marekani wanaweza wakajiandikisha kwa njia ya TEKNOHAMA na hivyo kuweza kutumia nguvu kazi yao katika fani mbalimbali. Lakini kwa bahati mbaya sijaweza kufanikiwa kuiona hiyo link kweye tovoti hii.
ReplyDeleteKama wahusika wa ubalozi wataiona hii naomba watueleweshe katika hilo ni nini cha kufanya