Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.
 
Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.
 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.
 
Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.
 
Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Shehe mambo yooote tisa, kumi hayo mapato ya Azam complex huko Chamanzi,,,! Nafikiri kuna somo limepatikana hapo, na waandaaji wa ratiba ya mashindano wamelielewa. Ila kwa timu zetu zinazotegemea mapato ya viingilio, kwa kweli hakuna mwanga wa uimara na uendelevu wao hapo mbeleni.

    ReplyDelete
  2. Embu tufanye scenario zifuatazo kwa kuzingatia viwango vya viingilio:
    - 59, 000 x 30, 000 = 1, 770, 000,000
    - 59, 000 x 20, 000 = 1, 180, 000,000
    - 59, 000 x 15, 000 = 885, 000, 000
    - 59, 000 x 10, 000 = 590, 000,000
    - 59, 000 x 7, 000 = 413, 000, 000
    - 59, 000 x 5, 000. = 295, 000, 000

    Hapa mtaona kwamba, tukifanya average (mliosoma hesabu na uhasibu ndo mahali penu hapa), basi walau kiingilio cha 10,000 ndo muafaka ya kuchukuliwa kama waliingia watu wote, mtaona kuwa mapato yalitakiwa yawe, walau 500, 000, 000.

    ReplyDelete
  3. HIVI HAYA MAHESABU MBONA TUNAFANYANA HATUNA AKILI?

    Hivi kweli 4,118.6 + (6,864.3 x 2) + (2,288.1 x 3)+ 1,372.8 + 915.2 ni sawasawa na 390 Milioni?

    Sio 26,999.5 ? AU MJOMBA WEWE NDIYE ULIYEKOSEA?

    HATUNA MAENDELEO KATIKA KILA SEKTA KWA KUWA TUNAFANYANA WAJINGA SISI KWA SISI!

    BORA HATA HAYO MAHESABU MSINGE YAKOKOTOA NA KUTUANIKIA HAPA JAMVINI KWA KUWA WATU TUNAZO AKILI!

    ReplyDelete
  4. Acheni Masihara!

    Hela nyingine ziko wapi TFF wakati Uwanja ulitapika namna ile?

    ReplyDelete
  5. Msifiiri kuwepo kwetu nje ya Maofisi hatuna akili!

    Wengine tumeyasoma Mahesabu mpaka kupitiliza, na tulikuwa Vipanga sana kwa NAMBA sasa leo ndio sisi mnatufanya Mzee Jangala kwenye Mahesabu sio?

    ReplyDelete
  6. Haya Mahesabu mbona yamekaa Kisanii sanii?

    Ule Uwanja unajulikana vizuri tu na mahudhurio yalionekana siku ile!

    ReplyDelete
  7. Miongoni mwa mwambo ya kuyafanyia kazi ni hili Suala la Maendeleo ya Michezo nchini sambamba na Makusanyo ya Mapato ktk Michezo.

    Inaonekana ni wazi pana 'Vijogoo' wananufaika binafsi kwa Makusanyo ya Mapato Michezoni wakati hayo Mapato yalitakiwa kunufaisha Tasnia ya Michezo nchini badala ya kuwapa uwezo binafsi wa kumiliki magari ya Kifahari na kuhudumia nyumba ndogo zao, huku na matokeo yake tunakuwa nyuma kimichezo Tanzania kila kukicha!

    ReplyDelete
  8. Duuu bonge la panga!

    Pana Mdau mmoja aliandika Maoni humu ya kuwa ktk Saccos chache zilizobaki nchini kimaisha ni;

    1.Siasa
    2.Dini
    3.Michezo

    Akasema kama utaanza na Saccos No.1 (Siasa) ukashindwa ni bora uhamie Saccos No.2 (Dini) napo ukishindwa nenda Saccos No.3 (Michezo) ni lazima kimaisha utafanikiwa!

    Sekta ya Michezo kulingana na Mapato yaliyochakachuliwa hapo kama tunavyoona mahesabu hayo (huku tukiangalia Uwanja ulivyokuwa siku ile) nimeamini ni SACCOS kubwa sana zaidi ya No.1 na No.2 hapo juu Nchini Tanzania!

    ReplyDelete
  9. What on the Earth TFF walikuwa wanafikiria, Unaweka mechi ya simba na yanga dar es salaam, siku moja na team ya Azam na Toto, na wanategemea watu waende wakaangalie Azam na Toto? Kweli TFF wamekaa kula hela tu na sio kufikiri jinsi gani ya kupata mapato.

    ReplyDelete
  10. Ankali ukokotoaji wa Mahesabu ya Mpato ya Michezo kama hapa, unatoa ushawishi wa hali ya juu kwa watu kutaka Kugombea nafasi za juu ktk Tasnia ya Michezo wakiamini pana Ulaji !

    Kuna sababu mtu akakaa kwenye Fani yake huku akiwa na Kipato kisicho ongezeka?

    Si ndio Dakitari akatundika ukutani Makoti ya Udakitari ,Glovu na Kipima joto shingoni akahamia kwenye Michezo?

    Ya nini kuteseka na Mandamano na Migomo ya Udakitari wakati azma kuu ya harakati hizo za migomo na maandamano ni kudai au kukuza Mapato?

    ReplyDelete
  11. Mwanawane haya mahesabu ndio yanakaribisha Ushindani wa hali ya juu katika Mchakato kuelekea Chaguzi za TFF na Vilabu vya Michezo nchini!

    ReplyDelete
  12. Nyingine ziko wapi???

    Eti nini mapato 390 Milioni tu?

    Ni afadhali msingetoa Takwimu hizi za kisanii kabisa tofauti na ukilinganisha jinsi Uwanja ulivyojaa siku ya Mchezo!

    ReplyDelete
  13. Heeeee!

    Michuzi mweleze 'Mkubwa' ya kuwa hapa ktk Michezo kuna wizi zaidi kuliko ukweli!

    ReplyDelete
  14. Ha ha ha ha ha !!!

    Wajameni haya ndio mafwao yenyewe ya mupira?

    Ya nini niote vigimbi vya miguu, sugu za viganja na niwe kijeba bureee wakati mimi kijana kwa kazi ngumu ya kilimo huku Mlimba Kijijini?

    Sikubali natupa jembe chini wataniwekea darini nyumbani Kijijini na mimi naenda Dar Es Salaam kugombea Uongozi TFF!

    ReplyDelete
  15. Ohhh!,

    Mtu mzima hasaidiwi kupenga kamasi!

    Michuzi wewe mwenyewe umepiga keybord za computer yako kuchapa mahesabu ya mandondocha uliyopewa na hawa jamaa.

    La muhimi mfikishie taarifa hizi 'Kingozi' juu ya wizi mkubwa unaojiri ktk mapato ya Michezo nchini!

    ReplyDelete
  16. Duh kulaleeek,

    Kwa mahesabu haya hata na mimi hapa Liwale napaki mkokoteni wangu na kuuweka juu ya mawe nataka Uongozi wa Michezo!

    Namshauri na Mjomba wangu Ndunje Ditundu kule Newala aukabidhi Mkoba wa ungariba kwa babu aendeleze hiyo kazi ya kutahiri watoto tukagombee Uongozi wa Michezo Dar!

    ReplyDelete
  17. Ela nyingine zilikua za bandia ndio mana TFF hawakuzihesabia...sasa msichokitaka nini..Kula urefu wa Kamba yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...