Washiriki wa mpango wa mama shujaaa wa chakula unaodhaminiwa na benki ya NMB hatimaye wameingia katika kijiji cha Maisha Plus. 

NMB inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake. 

Vilevile, NMB kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha itapata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.
 Mmoja wa wageni rasmi katika uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim  akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa shindano hilo kwenye kijiji cha Maisha Plus.
 Washiriki wa shindano la Maisha plus wakifuatilia uzunduzi huo huku wakiburudika kwa kinywaji cha dafu.
 Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman wakifurahia kinywaji cha dafu wakati wa uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Shindano la Maisha Plus Bw. Masoud A. Kipanya (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (kati) pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Oxfam Bi. Monica Gorman (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wakati wenzetu wanabuni vitu vya kisayansi na teknolojia sisi tuna......kwel bongo tambarareeeeeee sanaaa

    mdau Tokyo

    ReplyDelete
  2. Hakuna makosa katika maelezo ya picha zenu kweli? Sister naye mshiriki?

    ReplyDelete
  3. kwa kweli nimecheka sana! sasa hayo matunguri ni ya nini? kweli kabisa mambo ya vipapai, vibwengo na masoga soga ndio maendeleo ya M-Tz

    ReplyDelete
  4. msifikiri kila mtu anakaa mjini anahifadhi vyakula kama mboga kwa friji. vitu vingine hapo vyaifadhia vyakula vijijini kama mboga kavu nk kwa shemu kame kama dodoma etc. jambo usilolijua ni usiku wa kiza.

    ReplyDelete
  5. nchi uchawi uchawi tu mpaka sehemu za maana wanatangazia uchawi

    ndio maana sirudi bongo mpaka wachawi wafe wote mwe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...