Balozi Gillian A. Milovanovic

Takriban muongo mmoja uliopita, jumuiya ya kimataifa ilifikia makubaliano ya kudhibiti biashara haramu ya almasi inayochochea machafuko, vita na ugaidi kwa kuweka utaratibu wa utambuzi wa vyanzo vya almasi ghafi ujulikanao kama Kimberley Process (KP) certification scheme. 

Utaratibu huu uliweka pia vigezo vinavyotakiwa kufuatwa katika uzalishaji na biashara ya almasi ghafi. Hivi leo, ni lazima nchi zote 77 wanachama waKimberley Process, wadau wengine katika biashara hii na jumuiya huru ya kiraia zihakikishe kuwa mpango huu unafanyiwa marekebisho ili uendane na mabadiliko yanayoendelea katika soko la dunia.

Waanzilishi Kimberley Process walikubaliana kwa kauli moja kwamba ni lazima kudhibiti na kukomesha kabisa almasi na mapato yatokanayo na biashara yake kugharimia vitendo vya ukatili na mauaji yanayofanya na vikundi vya uasi. 

Wakitambua kuwa biashara ya almasi inategemewa pia na mamilioni ya watu katika kukimu Maisha yao, waanzilishi wa mpango huu walilenga pia katika kuimarisha soko na mahitaji ya almasi halali kwa kulinda heshima na hadhi ya madini haya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...