Marehemu Jesca Emmanuel

Mhe. Tuvako Manongi, Balozi  wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  kwa majonzi makubwa, anasikitika  kutangaza kifo cha  Jesca Emmanuel  (12), Mtoto wa  Afisa mwenzetu  Bw.  Emmanuel Swere Alfred  na Bi Doto, kilichotokea ghafla siku ya Jumapili 18/11/2012 katika Hospitali ya Mt. Sinai, Queens, New York. Taratibu na mipango ya  kuusafirisha Mwili wa Marehemu Mtoto Jesca kwenda kijijini  Bumbombi- Shirati Tanzania kwa mazishi  zinaendelea kwa usimamizi wa Ubalozi na Familia ya Marehemu.

Taarifa zaidi  zitatolewa na Ubalozi  kuhusu  siku, tarehe na  mahali tutakapomuaga   mpendwa wetu  Jesca Emmanuel.

Raha ya Milele Umpe Eee Bwana, na Mwanga wa Milele Umuangazie apumzike kwa amani. Amina
  
UBALOZI WA TANZANIA  UMOJA WA MATAIFA
 NEW YORK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Jamani it is just so sad to see the little ones going so soon! Mtoto mzuri... looking so sweet but she's no more! It is heartbreaking to the parents, family and friends. Mungu awatie nguvu na awaondolee majonzi yatokanayo na msiba huu mzito. May God grant this beautiful angel everlasting peace. Pumzika kwa amani mtoto mzuri!

    ReplyDelete
  2. Dah! Poleni wazazi ndugu na marafiki, inasikitisha sana, juzi tu mtoto Daniela tuomeona ameenda, but dont worry, she is at Peace in ALLAh's beautiful heaven, he was looking for a beautiful flower to place somewhere in his heaven and he chose this little angel... inauma sana but ALLAh atawajaalia Subira InshaALLAh, sote ni wa ALLAh na kwake ndio marejeo yetu, RIP beautiful Angel ..Amin

    ReplyDelete
  3. Poleni wafiwa. So sad. Siwajui wazazi wala marehemu mwenyewe lakini this untimely death imenigusa sana. It is a loss to the family and the nation maisha yapokatika mapema hivi. My heart and prayers go to the bereaved family. Kama mzazi, I can feel your pain.

    ReplyDelete
  4. Mulashani RCNovember 20, 2012

    R.I.P sweet daughter, May Our Almighty God shines all your way! Wazazi, ndugu jamaa na marafiki jipe moyo mkuu maana tumaini letu ni ktk Bwana aliye hai! Mapenzi yake yatimizwe.... ni mshumaa umezimika ghafla ktk umri huu wa matumaini! Inauma sana.

    ReplyDelete
  5. Sifahamiani na hii familia wala ya Daniella lakini misiba hii imeniumiza sana, imeniuma mno, Poleni sana wazazi, kama mzazi naelewa ni wakati mgumu kiasi gani mnaopitia, Mungu pekee ndiye mfariji wenu,kama msemaji aliyetangulia hapo juu ni siku chache tumesikia juu ya malaika mwingine Daniella,na leo malaika mwingine tena, tunaumia ila hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

    ReplyDelete
  6. Sifahamiani na hii familia wala ya Daniella lakini misiba hii imeniumiza sana, imeniuma mno, Poleni sana wazazi, kama mzazi naelewa ni wakati mgumu kiasi gani mnaopitia, Mungu pekee ndiye mfariji wenu,kama msemaji aliyetangulia hapo juu ni siku chache tumesikia juu ya malaika mwingine Daniella,na leo malaika mwingine tena, tunaumia ila hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wafiwa, kwakweli kwa wazazi hakuna kitu kinasikitisha kama kuondokewa na mtoto... The angles.
    Masikini, alikuwa anaumwa nini, mbona ghafla hivi???

    Pole saana, may you find comfort in God's hand

    ReplyDelete
  8. Pole sana kwa famila.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...