Hapa ni kwenye eneo la juu kabisa kuliko yote kwenye jiji la Mwanza ambapo unaweza kuona kila kona ya jiji hilo, ambapo hata minara ya mawasiliano ndiko ilikosimikwa. Kuna tofauti kubwa sana ya maisha ya eneo hili na maisha ya katikati ya jiji ingawa ni umbali wa mita kati ya 200 hadi 300 tu.
HiI ni moja ya njia ambayo wakazi hao wa milimani ndani ya jiji la Mwanza wanazitumia kupita huku zikiwa zimejazana mawe ambayo kwa mujibu wawenyeji mawe hayo yanahatarisha sana usalama wa watu wanoishi chini ya milima kwasababu mvua zinaponyesha nyingi huwa yanaporomoka.
 Kama haujaangalia vizuri unaweza kudhani ni jengo moja refu la ghorofa lakini si hivyo ila ujenzi wa milimani jijini Mwanza, hapa ni kwenye eneo la Kata ya Isamilo ipo ubavuni mwa jiji hilo upande wa kaskazini. Mbali ya kuwa ni mlimani lakini si milima hivi hivi ila ni milima yenye mawe makubwa na madogo ambapo hata ujenzi wake ni wachangamoto nyingi sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...