Leo Ankal anaamka na 'Treat her like a Lady' ya The Temptations. Ankal anashukuru kwa kuungwa mkono kwa safu hii kwa wapenzi wa muziki wa zamani na wa sasa kwa kuwa kila upande unaburudika na kujifunza mengi. Ieleweke enzi hizo ngoma zilikuwa zinapigwa 'kavukavu' na hamna kutegemea kompyuta na ala zinazojipiga zenyewe.

Kama itakumbukwa kwa jiji la Dar es salaam kulikuwa na viota vingi vya disko, ikiwemo YMCA iliyokuwa inatamba kwa Disko Toto kila Jumapili jioni chini ya DJ Kalikali na DJ Neagre Jay, RSVB ya Mbowe hotel na DJ Jerry Kotto na Seydou, Valentino Discotheque iliyokuwa Continental hotel Mtaa wa Nkrumah, Space 1900 iliyokuwa chini ya DJ Paul MacGhee pale Vision hotel (zamani Maggot), Rungwe Oceanic ya Kunduchi chini ya DJ Young Kim, Motel Agip chini ya DJ Bonny Luv, Keys hotel mtaa wa Uhuru alikuwapo DJ Eddy Sally  na kadhalika. Wenye data ya madisko ya mikoani kama vile Arusha 'Cave', Iringa, Mbeya na Mwanza kazi kwenu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Asante Ankal.
    Arusha nakumbuka Mawingu Disko kule njiro we bwana wee

    ReplyDelete
  2. Ankal nae anakumbukwa enzi zile anapiga picha YMCA, picha yako unachukua weekend inayofwata hahahahahaha

    ReplyDelete
  3. Umewasahau DJ Ebonite Woo Jack, DJ Richie Dillon, DJ Luke Joe, DJ John Peter Pantalakis, DJ Joe Johnson Holela n.k

    ReplyDelete
  4. Umewasahau kina DJ Ebonite Woo Jack (Richard Mazula), DJ Richie Dillon, DJ John Peter Pantalakis, DJ Joe Johnson Holela, DJ Deo Composer, DJ Danny Star (Mzambia), DJ Luke Joe

    ReplyDelete
  5. Mwanza ilikuwa mambo ya Alshers chini ya DJ Richie Dillon, palikuwa hapatoshi

    ReplyDelete
  6. Moshi town kulikuwa na Dj Issa kibaya kwenye kiota cha Liberty Hotel.

    ReplyDelete
  7. nyie acheni tu kifo kibaya jamani. inanikumbusha marehemu mmoja baada ya mwingine. tumshuru mola kwa kuendelea kutupa uhai. hii ardhi kweli inameza watu!!!!!

    Lakinu tusisahau ujumbe ya huu mwimbo hasa kwenye kudhamini wake zetu. Kwa mfano:

    "....When I was young, my mama used to say,
    Boy, A woman's like a flower, with love on her you shower...Ever since that day, her words never went away...I always will remember to treat my baby tender..."

    ReplyDelete
  8. Pia usisahau mwananyamala B Villa Motel kulikua mashindano ya disco kila weekend.

    ReplyDelete
  9. Duuuu nakumbuka mbali sana!

    Dj.Ebonite Woo Jack, pana Dj. mmoja amefariki Marekani miaka ya karibuni alikuwa ni mzaliwa wa Iringa ila alianza kazi zake Dar na baadaye kuhamia Philadelphia Marekani,,,naomba nikumbushwe ni nani yule?

    ReplyDelete
  10. Duuuu nakumbuka mbali sana!

    Dj.Ebonite Woo Jack, pana Dj. mmoja amefariki Marekani miaka ya karibuni alikuwa ni mzaliwa wa Iringa ila alianza kazi zake Dar na baadaye kuhamia Philadelphia Marekani,,,naomba nikumbushwe ni nani yule?

    ReplyDelete
  11. Msimsahau Dj. Young Millionaire alikufa kwa ajali ya Gari maeneo iliyopo makutano ya Holiday Inn Hotel na njia ya Haidery Plaza.

    ReplyDelete
  12. Choggy Sly


    Msimsahau Dj. Nguli huyo !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...