Hivi ndivyo Ulivyosomeka Ubao wa Matokeo katika Uwanja huu wa Taifa jijini Dar es Salaam,ambapo matokeo haya yalikuwa hivi mpaka mwisho wa mchezo uliomalizika hivi punge kwenye uwanja wa Taifa.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Taifa Stars,Mrisho Ngassa akijiandaa kuachia shuti kali lililoipatia  Stars bao la kuongoza wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda bao 1-0.
 Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Taifa stars imeshinda kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa mnamo dakika ya 45 ya mchezo. 
 Kocha wa Taifa Stars,Kim Poulsen akipeana mkoni na Kocha wa Zambia ambaye alionekana kutofurahishwa na Matokeo ya kufungwa kwa Timu yake,mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar jioni hii.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
Kocha wa Zambia hataki kumsikiliza mtu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hureeeeeeeeeeee hongera stars kumbe nilikua na wasiwasi na akina katongoz bure,ila sijui mchezo ulikuaje kiujumla? lakini ushindi ni ushindi.tupo pamoja.

    ReplyDelete
  2. What a sore loser!

    ReplyDelete
  3. Mchezo ulikuwa mzuri sana.Tulishuhudia burudani ya aina yake.Nilikuwemo uwanjani.Ni Nadra sana kuwaona stars wakicheza kwa kujiamini sana na kumiliki mipira,kuanza mashambulizi nyuma.Ulikuwa mchezo ambao kila timu ilitumia mbinu za kisasa za mpira.Tunahitaji wafungaji wawili wenye 'miili'pale mbele katikati.

    Huyo kocha wa Chipolopolo alikasrikia sana kwamba dakika ya 80 hivi timu yake ilinyimwa penati ya wazi baada ya Chris Katongo kufanyiwa faulo ndani ya 18 ...akarusha chupa uwanjani na kuingia tena uwanjani kuiokota.

    Nawatakieni wote sikukuu njema za mwisho wa mwaka.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...