Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekuwa ikiwapangia vituo vya kazi wahitimu wa Kada za Afya tangu mwaka 2005/2006.    Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na Matapeli wanaowarubuni na kuwaibia fedha baadhi ya waombaji wa kazi kwa lengo la kuwapangia vituo vya kazi vya Uuguzi na Wahudumu wa Afya.

Wizara inapenda kuwaarifu wananchi hususan wahitimu wa Kada mbalimbli za Afya kuwa:-

1. Kwa mwaka 2012/2013 Wizara bado haijapata Kibali cha kuwapangia Vituo vya kazi.  Kibali hicho kitakapotolewa wananchi watatangaziwa utaratibu wa jinsi ya kuomba kupitia Runinga, Magazeti, Radio na Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz).

2. Wizara itabadili mfumo wake wa utoaji wa barua za kupangiwa vituo vya kazi ambapo kuanzia sasa waombaji hawatapewa barua za kupangiwa vituo vya kazi bali majina ya waombaji na vituo walivyopangiwa yatatolewa kupitia Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz) na wahusika watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo walivyopangiwa baada ya kuona majina yao kupitia mtandao.

3. Upangaji wa vituo vya kazi hauwagharimu fedha yoyote.  Hivyo, waombaji wote msitoe fedha yoyote kwa ajili ya ahadi kuwa utapata ajira na mnatakiwa kuwa makini na matapeli hao.


Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
03 DESEMBA, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Du kama ni hivi basi tulipofikia sasa si pazuri tena na nadhani huko tunakokwenda kwa spidi hii mambo ndio yatakua mabaya zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...