November 2012
Mbunge wa Viti Maalum -CCM,Mh. Catherine Magige akiwa na baadhi ya wadau wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa Catherine Foundation kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mapema leo Asubuhi.Pamoja na Uzinduzi huo wa Catherine Foundation pia iliweza kutoa msaada wa baskeli kwa walemavu wa wilaya ya Arusha.
Meza kuu.
Mbunge wa Viti Maalum,Umoja wa Vijana CCM,Mh. Catherine Maggige akisomama taarifa ya Foundation yake ilivyoanza kazi mbele ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Mh. John Mongela na kuhudhuliwa na Wananchi mbali mbali wa jijini Arusha leo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Mh. John Mongela (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum,Umoja wa Vijana CCM,Mh. Catherine Maggige wakisukuma Baiskeli za walemavu wakati wa kukabidhi Baiskeli hizo kwa walemavu watatu kwa niaba ya walemavu 20 waliopewa Msaada huo.

Picha na  Ahmed Mahmoud, Arusha
 Wahitimu wa Stashahada ya Uongozi ya Uhandisi wa Chuo cha Bandari wakibadilishana mawazo wakati wa mahafali ya 13 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Stella Mutayaba, Kenny Mwaisabula na Kaseko Malongo. 
Kenny Mwaisabula akiwa na tabasamu wakati wa mahafali ya 13 ya Chuo cha Bandari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Baaadhi ya wahitimu wa Chuo cha Bandari wakiingia kwa maandamano wakati wa mahafali ya 13 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw. Syvester Manyara akionesha baadhi ya simu aina ya Samsung Galaxy S III mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),wakati wa Uzinduzi rasmi ofa maalum ya kipindi hiki cha Msimu wa sikukuu ijulikanayo kama “Samsung Season’s Offer!”. Uzinduzi huu umefanyika katika duka la Samsung lililoko Quality Centre, Dar Es Salaam.Kulia ni Mkufunzi wa Kampuni ya Samsung Electronics hapa nchini,Bw. Joel Laize  
Afisa habari wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Adrofina Ndyeikiza akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kimkoa yatafanyika katika uwanja wa Biafra, Manispaa ya Kinondoni. Kulia ni Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Dar es salaa kutoka TACAIDS Bw. Omary Chambo.
Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Dar es salaa kutoka TACAIDS Bw. Omary Chambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya maabukizi ya ugonjwa huo katika jiji la Dar es salaam na kutoa wito kwa wakazi wa jiji hilo kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali katika kupambana na Ugonjwa huo. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kuitambua kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya Malaria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na ugonjwa huo inayoitwa (Malaria Safe Companys) uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jijini dar es salaam jana.ambapo Wizara ya afya inashirikiana pamoja na taasisi za kimataifa na Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo.
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi akimpongeza Bw. Geofrey Meena baada ya kupokea cheti hicho kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Mzee CHrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama ya mkoani Rukwa kwa mchango wake katika kupambana na Malaria nchini.
 
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadau makampuni na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini mara baada ya uzinduzi huo.


Serikali ya Tanzania imekitaka kituo cha televisheni cha Kimataifa cha CNN kusahihisha taarifa potofu ilizotoa kuhusu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa upo kwenye ufukwe wa Pwani ya Tanzania jambo ambalo Serikali imesema siyo sahihi.

Akiongea na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene amesema Serikali ya Tanzania imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kuitaka CNN kuisahihisha mara moja.

“Tumesikitishwa sana na taarifa hiyo na tunashangaa kuona chombo kikubwa kama CNN wanaweza kutoa taarifa za uongo kwa kiasi hicho” amesema Bw. Mwambene.

Amesema ukweli ni kwamba unapozungumia eneo la Tanzania kilometa za mraba 947,300 (947,300 sq km)  ikiwa ni pamoja na  nusu ya eneo la ziwa kaskazini mwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji na kwamba mpaka upo katikati ya ziwa kama ilivyo kwa mpaka wa Malawi na Msumbiji.

Kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24 Novemba, 2012, CNN International yenye makao yake Makuu nchini Marekani  imekuwa ikiendesha  kipindi kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi na kuonyesha kwamba mpaka uko pembezoni mwa ufukwe wa Tanzania.

Bw. Mwambene amesema kuwa suala hilo hivi sasa linatarajiwa kupelekwa katika Baraza la Marais wastaafu wa Nchi za Umoja wa SADC kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9 mwaka huu.

Kauli mbiu za sherehe za uhuru mwaka huu ni uwajibikaji , uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI
Kutoka kushoto Mbuyu Ali,Shamsa Hamud na Grace Lyon kutoka Vodacom Foundation wakihakiki majina ya wanufaika wa mradi wa MWEI katika shehia ya Nungiwi Mjini Zanzibar tayari kupokea fedha za mikopo kuendeshea biashara ndogondogo. Zaidi ya wanawake 230 wa Nungwi na Kiwengwa mkoa wa Kaskazini Unguja wamepatiwa mikopo nafuu yenye thamani ya shilingi 27 Milioni kutoka mradi wa MWEI ulio chini ya Vodacom Foundation.
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika ya Zanzibar Asha Ali Abdula akifurahia jambo pamoja na Asha Haji mkazi wa Nungwi kabla ya kumkabidhi fedha za mkopo kutoka mradi wa kuwawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo kiuchumi (MWEI). Kulia ni Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon na Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Kiasi cha Sh27 Milioni zimetolewa kwa wanawake 233 wa Nungwi na Kiwengwa Mjini Zanzibar.

Serikali ya Zanzibar (SMZ) imeipongeza kampuni ya Vodacom kwa kubuni na kuanzisha mradi maalum wa kuwawezesha kiuchumi wanawake wa M-pesa Women Empowerment Initiatives (MWEI) unaowajengea wanawake uwezo wa kukabiliana na maisha kwa kuwapatia mikopo nafuu ya baishara.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika ya Zanzibar Bi Asha Ali Abdula wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo nafuu kwa wajasiriamali wanawake 230 wa Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A kupitia mradi wa MWEI ulio chini ya mfuko wa kusaidia jamii – Vodacom Foundation.

Zaidi ya wanawake 330 wa Nungwi na Kiwengwa wamepatiwa mikopo nafuu ya MWEI yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 27 Milioni ambapo wastani wa Sh 10,000 hadi laki mbili hutolewa kwa mwombaji.

Bi Asha ameutaja mradi huo kama mkombozi kwa wanawake ambao licha ya kuwa na jitihada mbalimbali za kujikwamua kiuchumi wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika kufanikisha juhudi hizo.

Amesema wanawake wengi wa Zanzibar wamekuwa na mwamko wa kujishughulisha na biashara ndogondogo ili kupata fedha za kusaidia matumizi katika familia ikiwemo chakula, ada na vifaa vya shule hivyo kampuni ya aina ya Vodacom yenye kufanya biashara za simu za mkononi kuona umuhimu wa kuwawawezesha kiuchumi wanawake ni jambo linalostahili pongezi.

“Nachukua nafasi hii kwa niaba ya serikali ya Zanzibar kuwapongeza Vodacom kwa mradi huu wa MWEI, hii ni fursa ya kipekee kwa wanawake wa Zanzibar kupata mikopo isiyo na riba wala dhamana ambayo hatuna budi kuipongeza kwa kuwa inaendana na azma ya serikali ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.”Alisema.

“Wanawake wenzangu wa Nungwi mikopo ya MWEI imeondoa vikwazo vya kupata mikopo…..mikopo hii haina dhamana na zaidi haina riba na hivyo inaendana hata na misngi ya dini hatuna sababu kushindwa kutumia vema fursa hii kujikwamua huku tukiwashukuru Vodacom.”Aliongeza Bi Asha.

Amesema kumkomboa mwanamke ni kuikomboa familia na jamii na kwamba chini ya uhamasishaji wa kauli mbiu ya Mwanamke akiwezeshwa anaweza ana Imani kubwa wanawake wa Nungwi watakuwa wa mfano wakitambua kuwa hata kikubwa kilianza na kidogo.

“Dhana ya uwezeshaji ni pana inahitaji taaluma ya biashara, mtaji na masoko…MWEI imetatua kikwazo cha mtaji kwa kutuwezesha mikopo nafuu na pia inatupatia elimu ya biashara kinachobaki ni kuwa na ubunifu wa mawazo bora ya biashara na kupata masoko ya bidhaa zenu”. Alisema Bi Asha.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim amewataka wanawake walionufaika na mikopo hiyo kutambua kuwa suala la mtu kujikwamua kiuchumi huanza na dhamira sahihi na ya dhati ya mhusika.

“Mafanikio yenu yapo mikononi mwenu kila mmoja anapaswa kutambua kuwa kujikwamua kiuchumi kunaanzia ndani ya nafsi yake akiheshimu kila fursa anayopata na kunzia hapo unajifungulia milango ya mafanikio.”Alisema Mwalim.

Ameongeza kuwa “Inchofanya Vodacom kupitia MWEI ni kuwatengenezea wanawake fursa na kuwajengea uwezo kwa kuthamini nafasi yao katika jamii na baada ya hapo ni jukumu la kila mmoja kuheshimu kile MWEI ilichomuwezesha ili kujikwamua na hilo linawezekana na ni imani yangu kwamba ipo siku Nungwi itatoa mwanamke mjasiriamali mwenye mafanikio zaidi ambae historia ya maisha yake imeanza na MWEI.”Aliongeza Mwalim.

Mradi wa MWEI ulioanzishwa mwaka 2010 hadi sasa umeshawanufaisha wanawake zaidi ya 6,000 nchi nzima. Kwa mwaka huu zaidi ya shilingi 450 Milioni zimetengwa kuwafikia wanawake zaidi.
no image

FAMILIA YA MAREHEMU DR JOHN KWEBA, INASIKITIKA KUTANGAZA MSIBA WA BABA YAO DR JOHN RUJANGI KWEBA (74), KILICHOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO, TAREHE 29 NOVEMBER 2012. 

MAREHEMU DR KWEBA ATAKUMBUKWA KWA UTUMISHI WAKE KAMA DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA KINAMAMA KWENYE HOSPITALI YA MUHIMBILI, KCMC  NA NCHINI ETHIOPIA.

MAREHEMU PIA, ALIWAHI KUWA MGANGA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA.

MIPANGO YA MAZISHI INAANDALIWA NYUMBANI KWAKE PASIANSI, MWANZA

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
During the East African Community (EAC) Summit 2012 in Nairobi, Kenya, President Jakaya Kikwete (front, right) met with the Acting Secretary of United States Department of Commerce Dr. Rebecca Blank, (front, left). Also pictured are United States Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt, (2nd, Left); Assistant Secretary of Commerce for Market Access and Compliance, Michael Camuñez; Economic Officer Patrick Collins from the U. S. Embassy in Dar es Salaam Tanzania, and Tanzania Minister of East African Cooperation, Samuel Sitta (2nd, right). The EAC Summit 2012 took place in Nairobi, Kenya on November 28 and 29.
President Kikwete and Acting Secretary of United States Department of Commerce Dr. Rebecca Blank discussed increasing engagement between the United States and East African Community during the EAC Summit 2012 which took place in Nairobi, Kenya on November 28 and 29.
President Jakaya Mrisho Kikwete and Acting Secretary of United States Department of Commerce Dr. Rebecca Blank discussed increasing engagement between the United States and East African Community during the EAC Summit 2012 which took place in Nairobi, Kenya on November 28 and 29.

MAREHEMU MAMA EDNA LIGATE SANDE
1945 - 2003

Leo ni miaka tisa (9) tangu ulipotwaliwa na mungu mama yetu tarehe 30 novemba, 2003. ni kama ndoto bado lakini tunamshukuru sana mungu kwa ajili yako mama yetu, yote ni mapenzi  yake.

Familia ya Mzee Adam Ligate Sande wa Forest Mbeya pamoja na watoto wako Osward, Liz, Jerry, Tabitha, Patricia na Mwapi tunakukumbuka mno kwa malezi mazuri na mafunzo uliyotupatia.

Tunakukumbuka Upendo wako wa dhati, Ucheshi wako, Ukarimu wako na mengine mengi ambayo ulituachia hasa upendo.

Unakumbukwa pia na wakwe na wajukuu zako majirani zako na ndugu kwa ujumla.

JOSHUA 1:9


MUNGU AZIDI KUKUPA PUMZIKO LA MILELE
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania,Mhe.Job Ndugai,(Mb) akiongoza kikao cha Kamati ya Masuala ya Jamii na Mazingira ya Mabunge ya Nchi za Africa,Carribbean,Pacific na Jumuiya ya Ulaya.Mkutano huo umemalizika leo nchini Suriname.picha na Saidi Yakubu.
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Klaus-Peter Brandes mara alipomtembelea ofisini kwake. Balozi huyo aliongozana na watendaji kutoka kampuni ya Koch Engineering & Construction ya nchini Ujerumani ambao wanania ya kuwekeza katika miradi ya nishati ikiwamo gesi asilia, umeme wa upepo, jua pamoja na kuwekeza katika viwanda vya uzalishaji mbolea.
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo akimuonesha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Klaus-Peter Brandes ramani ya bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam. Profesa Muhongo alimueleza mheshimiwa Balozi kuwa Serikali ina mpango wa kuzalisha umeme kwa njia ya gesi katika eneo la Somangafungu.
Ambassador Alfonso Lenhardt launching the "Get Back to Treatment" campaign with Iringa Regional Commissioner Dr. Christine Ishengoma in September. Launched in Iringa in September 2012 and sponsored by the American People, the goal of the campaign was to reach out to and find the missing People Living with HIV(PLHIV) who had stopped treatment and bring those patients back to treatment. 

 Every year on December 1, the global community commemorates World AIDS Day. It is a day to reflect on lives lost, and lives forever changed, as a result of AIDS. It is also an opportunity to pay tribute to more than 34 million people living with HIV worldwide. Today, we celebrate those lives saved and improved in Tanzania and recommit to the fight against AIDS. 

 CLICK HERE FOR FULL STORY
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International, Balozi Ellen Margarethe akipokea zawadi ya dafu kutoka kwa mkazi wa kijiji cha Jaribu, Wilayani Kisarawe mara baada ya kukagua na kupata repoti za maendeleo za miradi hiyo kijijini hapo, wanaoangalia ni Lydie Boka, ambae pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Plan international akifuatiwa na Stella Tungaraza , Mshauri wa masuala ya Kujikimu wa Plan (T), anaeangalia kwa mbali ni Regis Nyamakanga, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Plan Internation.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International, Balozi Ellen Margarethe, akicheza na wananchi wa Kijiji cha Jaribu, Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, alipowatembelea kwa ajili ya kuangalia na kujifunza utendaji wa miradi inayofadhiliwa na shirika hilo.
Mdau Raphael Mwabuponde ambaye alikukuwa ni Mkurugenzi wa Makampuni ya RM Accounting and Tax Services na MR Shipping and Export LTD,Columbus-Ohio nchini Marekani akitoa msaada wa bidhaa mbali mbali yakiwemo mavazi kwa Watoto waliopo kwenye Kijiji cha Soga,Kibaha Mkoani Pwani.
Mdau Raphael Mwabuponde (kushoto) akizungumza na Baadhi ya Wanafunzi wenye Ulemavu wa Shule ya Sekondari ya Yombo Vituka,Jijini Dar mara baada ya kuwapatia Msaada wa Magongo ya Kutembelea wakati alipoitembea Shule hiyo.
Mdau Raphael Mwabuponde pia alipita katika Shule hii ya Awali iliyopo Kimara Suka na kuwachangia Vitabu na vitanda vya kupumzikia watoto.
Mdau Raphael Mwabuponde akiwa na kina bibi wa Kijiji cha cha Soga,Kibaha Mkoani Pwani mara baada ya kuwapatia msaada wa mavazi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana amezindua rasmi majengo ya makazi ya Mchikichi yaliyopo Mchikichini jijini Dar es Salaam katika tukio lililowakutanisha wadau mbalimbali nchini wakiwamo wanasiasa, wafanyakazi wa NHC, wadau wa sekta ya uendelezaji miliki.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akizindua rasmi Ujenzi wa Nyumba za Makazi za NHC Mchikichini Jijini Dar es Salaam kwa kuweka jiwe la msingi katika katika mojawapo ya majengo ya majengo hayo ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , baada ya uwekaji wa jiwe la msingi alikagua ujenzi wa mradi huo wa nyumba.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akizungumza na MC maarufu nchini na Mtangazaji wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba, Ephraim Kibonde (picha ya juu) pamoja na mtangazaji wa TBC (picha ya chini) baada ya uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi za NHC Mchikichini Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , baada ya uwekaji wa jiwe la msingi alikagua ujenzi wa mradi huo wa nyumba.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akizungumza na MC maarufu nchini na Mtangazaji wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba, Ephraim Kibonde (picha ya juu) pamoja na mtangazaji wa TBC (picha ya chini) baada ya uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi za NHC Mchikichini Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , baada ya uwekaji wa jiwe la msingi alikagua ujenzi wa mradi huo wa nyumba.

Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za misiba ya wasanii watatu wa tasnia ya filamu na muziki nchini.

“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya vifo hivi vya wasanii hawa John Mganga, Mlopelo na Hussein Mkeity a.k.a Sharo Milionea ambao mchango wao unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo waliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.”

Baraza linatoa pole kwa familia za marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na wapendwa wetu.

Tunaomba mwenyezi Mungu azipumzishe mahala pema peponi roho za marehemu. Baraza liko pamoja na familia za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Imetolewa na
Ghonche materego
Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.
Mantra Tanzania Managing Director Asa Mwaipopo
By Staff Reporter, Songea.

MANTRA Tanzania has conducted a uranium awareness seminar in Songea to sensitize members of the Ruvuma Regional Consultative Council (RCC) on uranium development and the Mkuju River Project located in Namtumbo District, Ruvuma region.

The seminar that was officiated by the Ruvuma Regional Commissioner, Hon. Said Mwambungu attracted other stakeholders from Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC), National Environment Management Council (NEMC), Ministry of Energy and Minerals (MEM) and Mantra Tanzania.

Speaking during the event, the Mantra Tanzania Managing Director Asa Mwaipopo said the seminar is part of the company’s awareness drive that seeks to create awareness on uranium mining amongst to the public.

 Hivi ndivyo kura zilivyopigwa katika tukio hilo  lililojaa shamra shamra za aina yake na kuifanya Palestina kuibuka  kidedea na kupandishwa hadhi, kura 138 zilisema ndiyo, kula 9 zilisema hapana na kura 41 hazikufungamana na upande wowote. Tanzania kama ilivyokuwa kwa  nchi nyingine nyingi  ilipiga kura ya kuunga  mkono azimio hilo pamoja na kutoa sababu kwa nini imefikia  uamuzi huo. Ingawa  azimio hilo linaipandisha hadhi Palestina  na kuifungulia milango ya  kujiunga na taasisi nyingine za kimataifa, kama ikitaka kufanya hivyo,  bado inasafari  ndefu ya kufikia hatua ya kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa,  kutoka na kwamba ni lazima mchakato huo uanzie Baraza  Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  ambako Marekani imeleza bayana kwamba itapiga kura ya veto dhidi ya  ombi hilo
Rais wa Mamlaka ya  Palestina Mahmoud Abbas akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  muda mfupi kabla ya upigaji kura wa Azimio la kuipandisha Hadhi Palestina kuwa  kama nchi muangalizi asiye mwanachama wa Umoja wa Mataifa,  tukio hilo la kihistoria limefanyika siku ya  Alhamisi hapa Makao Makuu ya  Umoja wa Mataifa.  
Habari kamili BOFYA HAPA


Hatimaye watanzania wamepata mtandao mpya wa kijamii unaojulikana kama mambopoint ambapo watumiaji watakuwa na uwezo wa Ku-chat na marafiki, kualika marafiki, kuona mambo yote yanayoburudisha kwenye mitandao ya kijamii kama facebook.

Hii ina maana watumiaji wanaweza kushirikishana matukio kwa picha (photo sharings), video na maandishi sambamba na kutoa comments kwenye matukio ya watu wengine na marafiki wakati kule kwenda zaidi ya mambo ya kijamii na kuongeza manufaa ya kiuchumi likiwa jambo linaloutofautisha mtandao huo na mingine.

Masoud Mahundi ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Maaarifa Informatics Ltd, wabunifu na waendeshaji wa mtandao wa mambopoint, amesema kuwa mtandao huo unapatikana kupitia tovuti www.mambopoint.com

Mahundi aliongeza kuwa tayari huduma muhimu ya kutangaza kazi imekwisha anza na takriban nafasi 50 za kazi huingizwa kila siku, kutoka idara mbali mbali ndani na nje ya nchi hivyo kuufanya mtandao huo kuwa wa kijamii na kiuchumi.

“Kwa hivyo badala ya kijana kutumia shilingi 800 kununua gazeti, kutafuta kazi kwenye mitandao mingine na kuchati kwingine, sasa atapata vyote katika mtandao wa mambopoint” alisema.

Mambopoint.com ilianza kusukwa tangu mwaka jana, 2011 na wataalam wa IT na ICT wengi wakitokea chuo kikuu cha Dar es Salaam kiasi cha kuutofautisha mtandao huo na mingine kwa kuongeza huduma za kiuchumi na hivyo kuwa social-economic network pekee nchini na pengine duniani.




 Precision Air Commercial Director Mr. Patrick Ndekana (left) speaks to journalists (not in picture) in Dar es Salaam yesterday about his company’s support of 9m/- towards a four-days breast cancer awareness and screening campaign that kicks off in Mtwara and Lindi on Wednesday. Looking on is the Aga Khan Health Service’s Head of Nursing Services, Loveluck Mwasha.
Aga Khan Health Service (AKHST’s) Head of Nursing Services, Loveluck Mwasha (right) speaks to journalists (not in picture) in Dar es Salaam yesterday about a four-days breast cancer awareness and screening campaign that kicks off in Mtwara and Lindi on Wednesday, which has received a support of 9m/- from Precision Air Services PLC. Looking on is the Precision Air Commercial Director Mr. Patrick Ndekana.Habari zaidi Bofya hapa.