Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) akizungumza na wakili wake Peter Kibatala muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa ombi lake la dhamana leo asubuhi kwenye Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ambapo dhamana hiyo imepatikana kwa mashart ya mashahidi wawili wafanyakazi wa Serikali kwa bondio ya fedha Tsh20 Millioni kila mmoja na masharti mengine tumeorodhesha kwenye habari hapo chini.
Msanii Lulu (katikati) akisubiri kusikiliza maombiyake ya dhamana kusomwa na Jaji anaesikiliza kesi hiyo Zainabu Mruke leo jijini Dar es Salaam.
Lulu akiwasili kwenye kizimba cha Mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo.
Wakili wa Lulu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kupatiwa dhamana.
Ndugu jamaa na marafiki wa msanii huyo na baadhi ya watu wengine wakiwa kwenye Chumba cha mahakama kuu jijini Dar es Salaam wakisubiri kusikiliza maombi ya dhamana.
Msanii Muhusin Awadi (Dk.Cheni) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutolewa kwa dhamana ya msanii huyo.

 HATIMAYE Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu mchana wa leo amepata dhamana na kuachiliwa kutokana na kesi inayo mkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu marehemu Steven Kanumba  mwaka jana.

Akisoma mashart ya dhamana Jaji anaesikiliza Kesi hiyo Zainabu Mruke, alitaja mashart kadhaa ambayo mtuhumiwa atatakiwa kuyatekeleza kabla ya kupewa dhamana hiyo. 

Mruke alisema mtuhumiwa atatakiwa kuwasilisha hatizake za kusafiria zote mahakamani hapo, atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali ambao kila mmoja atatakiwa kuweka udhamini wa Tsh20Millioni kama bondi na sio keshi.

Aidha Jaji Mruke aliongeza kuwa mtuhumiwa hataruhusiwa kusafiri nnje ya jiji la Dar es Salaam isipokuwa kwa ruhusa maalum ya mahakama.

Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala alisema amefurahishwa na dhamana aliyopatiwa mtejawake na wataendelea na kazi ya kumtetea hadi mwisho wa kesi hiyo.

Wasanii wenzake waliojitokeza na kuonekana mahakamani hapo ni pamoja na Muhusin Awadh (Dk.Cheni) na Steve Nyerere. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo Dk.Cheni alisema yeye binafsi amefurahishwa na dhamana hiyo na yuko tayari kufanyanae kazi.

“Lulu nilimchukua kwao akiwa na miaka mine na kuanza kufanyanae kazi hadi sasa akiwa na umri wa miaka 18 amekua msanii mkubwa nan i Director mzuri pia kwahiyo nitaendelea kufanyanae kazi”Alisema Dk.Cheni.

Alipoulizwa kuhusu kutimiza Mashart ya dhamana Dk.Cheni alisema kila kitu kilikuwa kimetimia ispokuwa passport tu ndio hawakutarajia kama ingehitajika lakini tayari alishapigiwa simu mtu ailete kutoka nyumbani kwao Tabata na kukamilisha mashart ya dhamana hiyo. 

April saba mwakajana msanii huyo alifikwa na kadhia hiyo ya tuhuma za kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa Filamu nchini marehemu Steven Kanumba kutokana na mgogoro uliotokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kuelezwa kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. How are they going to compensate this young lady for all her precious time she wasted behind bars. Almost two years of her schooling is missing, and have no case against her so far. They keep saying that they are still doing investigation. If you are still doing investigation that means you have no probable cause. If you don't have probable cause, why do you have to put someone behind bars?

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu hayo maoni yako yangefaa sana yafike tume ya katiba mpya.

    Kwa sheria ilivyo sasa ukituhumiwa uumeuwa, yaani wewe huna dhamana mpaka uchunguzi ukamilike na kesi ianze kusikilizwa; huna hata nafasi ya kujiridhisha na ushahidi unaonaletwa mbele yako, ni mpaka polisi waseme uchunguzi umekalika...sote tunajua polisi wetu huwa inawachukua muda gani kukamilisha uchunguzi.

    ReplyDelete
  3. Anonymous of Tue Jan 29, 02:49:00 am 2013: Two years of her schooling - what schooling are you talking about? I beleive Kanumba died last April and it hasn't even been a year since his death and her behind bars.

    I suggest to her and her people to start to immediately to shed that name "Elizabeth Michael - Lulu" and start using Elizabeth Kimemeta. The name "Lulu" would forever be linked to Kanumba's death. Besides, its a character that she played in a movie - Sylvester Stallone is never associated with "Rambo" or "Rocky"; Arnold Swarzeneger (sp) never associated with "Commando" etc., all being famous characters they played in movies. Sadly Tanzanian actors are forever living with character names they played - Ray, Johari, etc. Upuuzi mtupu!!!

    ReplyDelete
  4. Lulu has not been acquitted, she still has to answer the charges against her, thank god that the charge has changed from murder to manslaughter. The nice thing is that this time she will be attending court for the charge from her parents' home instead of coming from lockup. Inshaallah she will completely be free soon.

    ReplyDelete
  5. Anony wa Tue Jan 29, 02:49:00 am 2013, unadhani watu wanaachiwa tu bila kufanya uchunguzi na sheria kufuatwa. Inaonesha hujui sheria za nchi wala jinsi kesi zinavyoendeshwa. Kwa hiyo ulitaka wamuachie huru siku ile ile waliyomkamata? Siyo lazina uchangie kila issue.

    ReplyDelete
  6. MUNGU NI MWEMA

    ReplyDelete
  7. Mdau wa kwanza mie ningekushauri ungekaa kimya kwanza uone mambo yanavyokwenda kumbuka kuwa hapa kunafamilia mbili zimedhurika jitahidi kuwa na hekima by not taking any sides.

    ReplyDelete
  8. She is too young!

    ReplyDelete
  9. Atakuwa salama huko mtaani?kwa maana ya lile kundi 'jingine'

    David V

    ReplyDelete
  10. nimefurahi sana.kwa mtu yeyote hapa linaweza kutokea kama anaishi na mume ajiulize mara ngapi walisukumana. au ulivyokua shule secondar hujawahi kusukuma mtu?bado alikua anampenda kanumba hakutaka afe.ni bahati mbaya tu.

    ReplyDelete
  11. Namuunga mkono mdau hapo juu,,kuna famikia mbili hapa,,kilichotokea siku ya kifo cha Kanumba ni Lulu na Kanumba ndo wanajua,too bad one of thm hayupo kusema ya upande wake,yeah kila mtu anamuonea huruma Lulu nw bt mama yake Kanumba je?simuhukumu yeyote hapa ila muache kutake sides na mumshauri huyo Lulu atulie,m sure wote wanaomuonea huruma wangejitokeza kumkanya kipindi anafanya mambo ya ajabu leo asingefikwa na yote hayo,Lulu mdg wangu umeyaina yote sasa kaa chini mrudie muumba wako na utulie,ningekushauri urudi shule tu.

    ReplyDelete
  12. Kanenepa kweli-Jela za bongo kama mtoni nini siku hizi-Mboga tatu duuu!

    Manslaughter minimum sentence yake si chini ya miaka 4 kama aliyokula Doctor wa Michael Jackson, bado tumuonee huruma maana hiyo Man slaughter inaweza mpeleka jela tena.

    ReplyDelete
  13. Huyo jamaa wa kwanza bwana, Elizabeth was not a student while all that happened was taking place. She dropped school zamani.Na kilichotokea hapo ni utakelezaji wa sheria tu ya dhamana,na km unafikiria kupoteza mda mie nadhani muda umepotezwa kwa kubishana umri na ama alistahiri dhamana au laa.

    Wala kesi yake ya msingi haijaanza kusikilizwa, sasa sijui ungekuwa wewe kwa mawazo yako ungesuggest hiyo fidia atoe nani. Na kwa taarifa yako mpk leo anaachiwa wala mwaka haujatimia tangu ashikiliwe ss sijui unazungumzia miaka miwili ipi!!!!!

    ReplyDelete
  14. WATU MNAJITIA KUJUA ENGLISH WAKATI HATA MATUMIZI YA HIS & HER HAMJUI
    KWENYE FEMALE MNAWEKA HIS, KWENYE MALE MNAWEKA HER????
    DUH, MUNGU WABARIKI WATANGANYIKA.
    ####PROUDLY JALUO!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. She looks healthy anyway, What do they feed them in there?
    Wacheni sheria ichukue mkondo wake na mwache Kiswahili mrefu ninyi WaTZ! Maneno matupu tu. Mwatakana muijue sheria na mwangalie vipi inakuwa enforced!
    Mkipeana kitu kidogo ni basi!

    ReplyDelete
  16. Msajili hayupo! Mtu anarudishwa lupango! A dysfunctional judicial system. Justice delayed is justice denied!

    ReplyDelete
  17. wewe hapo juu kanumba died 9 months ago...sasa hiyo miaka miwili sijui umeisoma kwenye kitabu gani! plus Lulu hakuwa school wala mtoto wa school

    ReplyDelete
  18. iam happy for lulu if she getout

    ReplyDelete
  19. @Anonymous of Tue Jan 29, 09:00:00 am 2013. Even if it was one day still it is a lot. It looks like state has no case against her. Nine months is too long still. The longer it gets, we get more contaminated evidences.

    I still believe they are wasting her time for no apparent reason. If that is how our judicial system works, then it is about time to change it. I rest my case.

    @Anonymous of Tue Jan 29, 02:49:00 am 2013. Yea, you know sheria za nchi. You better learn how to differentiate between L and R Mr. "Actuarrrry".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...