Afisa Habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkoma akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka wahanga wa Mauaji ya Kimbari ya Holocaust kwa vijana wanafunzi wa shule za sekondari na baadhi ya vyuo.
Amesema katika siku hii ya kimataifa, tuwakumbuke watu wote wasio na hatia ambao walipoteza maisha wakati mauaji ya kimbari ya Holocaust.
Ameongeza kuwa vilevile tuhamasishe na wale ambao walikuwa na ujasiri wa kujali watu wa kawaida ambao walichukua hatua zisizo za kawaida kulinda heshima ya binadamu. Mfano wao unaweza kutusaidia sisi kujenga dunia bora zaidi leo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uokoaji wakati wa Mauaji ya Kimbari: Ujasiri wa Kujali”.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkoma (hayupo pichani) alipokuwa akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka wahanga wa Mauaji ya Kimbari ya Holocaust iliyofanyika jijini Dar leo katika ukumbi wa British Council.
Wanafunzi wa shule za Sekondari, vyuo na wafanyakazi wa UN wakifuatilia Filamu 'The Rescuers' inayosimulia kwa undani kuhusiana na stori zinazowahusu wanadiplomasia 13 waliofanya vitendo vya kishujaa na kijasiri ambao waliowaokoa maelfu ya Wayahudi wakati wa vita vya pili vya Dunia. Filamu hiyo imetengenezwa na mtayarishaji wa filamu maarufu na mshindi wa tuzo EMMY Michael King.
Mjumbe wa Chama cha Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Bernadetha Mshana akisoma shairi lenye ujumbe wa kupiga vita mauaji na kuhamasisha vijana kudumisha amani.
Burudani ya ngoma za asili.
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akiendesha mjadala na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari kutoka katika vilabu vya UN kuhusiana na siku ya kimataifa ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya Holocaust baada ya kutazama filamu iliyokuwa ikielezea mauaji hayo inayoitwa “ The Rescuers” iliyotengenezwa na mtengenezaji filamu maarufu Michael King.
Dakika moja ya ukimya: kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Holocaust.
Baadhi ya vijana wa UN Clubs wakimsikiliza kwa makini Bi. Stella Vuzo.
Pichani Juu na Chini Wanafunzi wakitoa maoni yao baada ya kutazama filamu hiyo wakati wa Mjadala ulioendesha na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi Stella Vuzo (hayupo pichani).
Bi. Usia Nkoma akitoa neno la shukrani kwa washiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mnakumbuka holocaust, what about watumwa? au kwasababu watumwa ni mipingo hivyo siyo tija?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...