Viwanja vinauzwa,vimepimwa na vina hati,vipo eneo la Viwanda Mwanambaya Mkuranga barabarani na vimezingatia hifadhi ya barabara,vimepakana na kiwanda cha Cement,kiwanda cha Gypsum na Yad ya Scania used,Heka 4 bei yake ni sh mil.700,zipo heka 28 nyuma ya hicho mil 700,zipo heka 4 zinapakana na ukuta wa kiwanda cha Cement Mil.600.

Zipo heka 6 hazijapimwa zipo barabarani  eneo hilo hilo mil 500. Mwandenga  zipo heka 67 Mil. 700,Zipo nyumba eneo la Gerezani  kariakoo Mil. 700 kwa Mil.900,Round about ya Kariakoo bilioni 1 na 200 milioni.Kariakoo stendi ya Kawe ni bilioni 1 na 200 mil. Ipo beach gezaulole Kigamboni Mil.600,pia vipo viwannja vya Mil.10 na vilivyopimwa kwa mil 25 Gezaulole-Kigamboni.

Kwa mawasiliano piga namba 0652020343

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hivi zile bei elekezi za viwanja bado hazijaanza kutoka?

    ReplyDelete
  2. duh.. !! hata newyork vipo vya rahisi zaidi ya hapo.

    ReplyDelete
  3. Kwa muondoko huu, Nani mzalendo asiye fisadi atamudu kumiliki ardhi??? Ya Zimbabwe ya ardhi yatakuja Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Mbona Watanzania vichwa vigumu sana kuelewa mambo?Hivi Mwalimu Nyerere tumemtupa wapi?Angekuwa hivyo wakati wa Uongozi wake,nchi hii ingekalika kweli?Masikini wangekuwa na sauti yoyote katika maamuzi ya nchi yao?Ardhi ni "Godgiven natural resource",ni zawadi kutoka kwa mwenyezi Mungu,muumba wa vyote kwa viumbe wake wote!Kila binadamu ana haki ya asili,ya kuzaliwa,kumiliki eneo kwa ajili ya maisha yake.Kama vile vile ambavyo huwezi kuuza "Hewa(Oxygen)",au "Maji(watersource)","Mwanga/Jua(light)",na rasilimali adimu na adhimu za aina hiyo,ambazo ni Mungu pekee aliye na uwezo wa kuzifanya ziwepo na zisiwepo,na kuhatarisha uhai wa viumbe wengine!Hivi karibuni tu,lilitoka Tamko la Serikali kupitia kwa Waziri wake,kwamba,Serikali muda si mrefu itatoa "Bei Elekezi"kwa ardhi yote nchini,ili kuziba mianya ya aina hiyo yenye kila dalili ya "Ushetani" wa kuabudu Pesa na Utajiri wa haraka haraka bila kuutolea jasho,isipokuwa kuwahi tu eneo la tukio!Kupitia Blog hii iliyotukuka,napeleka Ujumbe kwa Waziri Mhusika na Ardhi nchini,kwa maana hiyo,napeleka kilio changu serikalini,na kutarajia kwamba Rais wetu atausoma ujumbe huu,kwamba,"Asitishe mara moja"zoezi lolote hapa nchini,popote pale,la "Kuuza Ardhi" kwa mtindo huu wa "kidalali",hadi hapo Serikali itakapo toa Tamko Rasmi kuhusu biashara hiyo.Huu ni "Wizi na si Vinginevyo"!Mwenye Uwezo wa kununua Kiwanja kwa bei hiyo ys shs.milioni 700 na zaidi,Takukuru wafanye kazi yao,ili kubaini fedha hizo zimetokana na vyanzo gani,lakini,zisiwe Kodi za Walalahoi!Jamani,muda unakwenda kasi,mambo haya yasiachiwe yaote mizizi hapa nchini!waiting to see govt'ments' response! du!hapana,sasa nchi imefika pabaya!Mwisho wake,tutaanza kuuziwa hata Makaburi ya kuzika ndugu zetu!Serikali iko wapi,mmelala fofofo!....(to....y)

    ReplyDelete
  5. ...viwanja karibu na kiwanda cha cement na gypsum hilo ni eneo la makazi au la viwanda...?

    ReplyDelete
  6. Duhhhhh!!!!! Hivi hawa watu wanayajua maisha ya watanzania wa kawaida kweli? au hizi bei ni kwa ajili ya mafisadi tu??

    ReplyDelete
  7. Yeye anaeuza katumia vigezo gani kufikia hizo bei za bilion moja, na kodi yake vipi nani analipa!?

    ReplyDelete
  8. Hivi kweli tutamiliki mali kweli kwa bei kama hizi? Hii si kutaka wasionacho/masikini watumie mtaji wao kuweza na wao kumiliki vitu vya bei kama hizi??

    ReplyDelete
  9. wandegereko waende wapi? moshi? au Mtwara, kama gesi inakataliwa wananchi vilevile wangekataa nchi kuuzwa kama hivi. Huu ni wizi. Mtanzania gani mwenye uwezo wa kununua kiwanja bei kama. Anaeuza viwanja hivyo, ni serikali au Knightsupport. Tumekwisha watanzania.

    ReplyDelete
  10. Nichagueni kuwa rais....nina ahidi kuondoa ufisadi tanganyika na zanzibar


    Nagombea 2015...kauli mbiu ni. ..bongo si new york...ukisikia hiyo pigA kura kwangu

    ReplyDelete
  11. Kwa bei hizo nanunua nyumba Mayfair London na wala siyo kiwanja. Hii inaonyesha ni jinsi gani tunaishi ktk nchi ambayo hakuna regulation ya kitu chochote, kuanzia hospitals, shule hadi sasa ardhi. Kwanini watu wauze ardhi kwa bei hizo. ktk nchi masikini kama hii wanamuulizia nani kama hawataki kujenga system ya capitalism ktk nchi masikini. I think wee need to discuss about moral issues here!

    ReplyDelete
  12. Poleni ndugu mnaozisikia leo bei za hivi viwanja.
    Hii ndiyo Tanzania.
    Hapo bado hujampa huyo dalali 10% yake. Uzalendo bado Tanzania hicho ndicho kinatuuua hata wakipanga bei haitasaidia nataka utachukua hutaki nenda kwa mpanga bei akakupe chakwake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...