Mjasiriamali Elizabeth Chami (26), akioka keki kwenye jiko la kisasa alilozawadiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012, kwenye karakana yake iliyopo Tabata Mawenzi, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Elizabeth akikata lebal  ya kampuni yake tayari kubandika kwenye kasha la keki
 Mfanyakazi wa karakana hiyo, Happiness akiweka akioka keki kwenye jiko hilo la kisasa. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mfanyakazi wa Kiwanda cha kutangeneza Shampoo  cha L & V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam, Hashim Hussein akifungasha katoni za bidhaa hiyo. Kiwanda hicho kilisaidiwa chupa 15,000 baada ya mmiliki wa kiwanda hicho Valerian Luzangi (hayupo pichani) kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012, (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Luzangi akisaidia kupanga vizuri chupa zilizojazwa shampoo. Kushoto ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Stahabu Mwinyi.
 Mjasiriamali Valerian Luzangi (38), kulia, akipanga vizuri katoni za shampoo anazozalisha katika kiwanda chake cha L & V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Luzangi alisaidiwa chupa 15,000 baada ya kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012, Kushoto ni mfanyakazi wake, Hashim Hussein. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha wakiwa sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012, (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mjasiriamali Innocent Mberwa akionesha tikiti maji katika moja ya mashamba ya Kampuni yao ya  Tin Wax yaliyopo eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo wa maji wa umwagiliaji baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha wakiwa sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Baadhi ya vitunguu vinavyozalishwa katika shamba hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Safi sana, serikali yetu nayo ijifunze wanapotoa takwimu mfano wakulima kadhaa wamepewa pembejeo wawe wanaonyesha na mrejesho wa matokeo yake sio maneno tu huku hakuna chochote.

    ReplyDelete
  2. Ama kweli tumethibitisha ya kuwa Ajira sio lazima uwe Ofisini Kazi ni kazi la muhimu iwe halali ili mradi mmkono wende kinywani!

    Angalieni,

    -Kilimo cha matikiti uwezekano wa maisha upo,

    -Usindikaji wa bidhaa za urembo na usafi uwezekano upo,

    -Utayarishaji wa vyakula uwezekano upo!

    -Kilimo cha vitunguu uwezekano upo!

    Yaani ni wewe tu!

    Akili kichwani na jitihada!

    Ya ni utumie ulaghai?, ya nini mabavu?

    ReplyDelete
  3. Inatia Moyo!mwenye macho haambiwi tazama!fanya maamuzi sasa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...