Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii aliyeko Mikumi Morogoro. 
 ZAIDI ya wanyama 200 wa aina tofauti 12, katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi,kila mwaka hufa kwa kugongwa na magari katika barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Zambia inayopita katikati ya hifadhi hiyo kwa kipande cha kilometa 50. 

Na kutokana na magari kupita hifadhini bila kulipia na kusababisha mauaji ya wanyama, serikali imekuwa ikipoteza mapato ya zaidi ya Sh billion 6 kwa mwaka, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Damiani Saru amesema.

Akiongea na waandishi wa habari 10 wa mkoa wa Kilimanjaro, walio kwenye ziara za kutembelea hifadhi za taifa Bw Saru alisema kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi hiyo kina urefu wa kilomita 50, ambapo kuna mabango mbalimbali yakiwataka madereva kwenda kwa mwendo mdogo lakini bado wameendelea kuendesha kwa mwendo wa kasi unaoathiri  wanyama hao. 

 Alisema kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita wanyama zaidi ya wanyama 40 walikufa na baadhi ya magari yalikamatwa na kutozwa faini kulingana na aina ya mnyama. 

 “Faini inayotozwa si suluisho kwani si mara zote wanagogwa wakati askari wa wanyamapori wakiwepo mara nyingine inatokea wakati hawapo na wahusika kukimbia na kubaki kuokota mizoga…tumefanya utafiki kwa mwaka tungekusanya Sh billion 6 iwapo magari yote yanayopita yangelipa” alisema.

Aliainisha wanyama wanaogongwa mara kwa mara kuwa ni swala pala ambao huruka kwa wastani wa 15 hadi 20, samba, chui, twiga, tembo, nyani, nguruwe na digidigi na zaidi hutokea nyakati za usiku. 

Bw Saru aliongeza kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), limewasilisha andiko kwa serikali kuelea umuhimu wa kuondolewa kwa barabara hiyo na inavyoendelea kuwepo ina athari gani kwa mustakabali wa wanyama na wanaednelea kusubiri majibu. 

 Mhifadhi huyo alisema awali waliweka kizuia kwa magari mwanzo na mwisho wa hifadhi na kila gari kutakiwa kulipia, ili kuepusha utalii wa bure, ujangili na kugonga wanyama, lakini Walaka wa Barabara nchini (Tanroads) walipinga suala hilo kwa kuna barabara ni mali yao. “Ifike mahali tiuone wanyama wanakwishwa, kulea mnyama mmoja hadi akifie umri flani inacchukua muda mrefu, wakiendelea kuteketezwa kwa kugongwa na ujagili hifadhini ni wazi kuwa watakwisha” alisema Saru. 

 Naye, Mhifadhi Utalii, Tutindaga Mdoe, alisema uwepo wa barabara hiyo umeruhusu utalii wa bure, ambapo wageni ambao walitaka kutembelea hifadhi huacha kwa kuwa wanaweza kupita barabarani na kupiga picha. Hata hivyo, alisema hifadhi imechukua hatua na kuwakamata wanaofanya hivyo, lakini kwa wanaosafiri kwa mabasi wamekuwa wakijionea wanyama bure jambo ambalo linapunguza idadi ya watalii wa nje na ndani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kotoza Road Toll siyo suluhishi na wanyama wataendelea kuuawa tu!
    Suluhishi kamili ni kupitisha barabara hiyo sehemu nyingine.
    It will be costly but it is worth it!

    ReplyDelete
  2. The Mikumi National Park Authorities need to come up with something creative,wakishirikiana na Idara ya Traffic Police!Kwa mfano,kwa kuweka Road Reflectors katika kipande chote hicho cha barabara toka Hifadhi inapoanzia hadi inapoishia , kila upande wa barabara,with speed warning signals,kwamba,dereva hatakiwi kuendesha spidi zaidi ya kilometa 40 kwa saa!Atakaye zidisha spidi hiyo atatozwa faini kubwa sana!Utajuaje dereva ameendesha spidi kubwa hivyo?Umbali wa barabara ndani ya hifadhi unajulikana,say,50 kilometres.Kwa mwendo au spidi ya, say,40 kilometres kwa saa,dereva atachukua muda wa saa Moja na Robo,kutoka Mlango wa kuingilia hadi Mlango wa kutokea.Gari litakapo ingia katika hifadhi,Security Guard wa Park,atachukua namba ya gari,na kumpigia Guard mwenzake Mlango wa kutokea,kwamba,gari namba fulani,uitarajie hapo baada ya muda fulani.Iwapo gari hilo litawahi kufika Mlango wa kutokea kabla ya muda huo,basi moja kwa moja atakuwa amevunja sheria za hifadhi na hivyo kutozwa faini!Akiwa mkosaji mzoefu,basi afikishwe mahakamani!Pendekezo hili ni rahisi kulisema,lakini,hatari zake,ni kutukuwepo kwa uaminifu miongoni mwa Security Guard wa National Park,ambao,tahadhari za kutosha zisipochukuliwa,wanaweza kugeuza huo kuwa mradi wao wa kujipatia kipato cha ziada "kwa kupokea rushwa!".Hili likifanyiwa kazi,itapunguza sana vifo vya wanyama katika Mbuga ya Mikumi!

    ReplyDelete
  3. We unategemea nini kwenye nchi ambayo haina ustaarabu?? Watu wakishafunga vioo wanaona kila kilichoko nje ni takataka isipokuwa wao waliomo ndani ya vyombo vyao vya moto! Ndio maana kuna uhadui mkubwa (uliojificha) kati ya watembea kwa miguu na yeyote aliye kwenye gari, mpaka watu wamehalalisha kuwa ukimgonga mtu wewe kimbia wasije wakakuua. Sasa kama mtu anagongwa na dereva anakimbia utafikiri amekanyaka jiwe tu, ije kuwa kwa wanyama??

    Hii ndio tofauti yetu na binadamu waliostaarabika dunia nchi nyingine (hata Kenya na Uganda wameweka sheria kali za kudhibiti ufedhuli na mambo kama haya). Hata kupiga honi bila sababu unaweza kunyanganywa credit za leseni yako kwenye nchi zilizostaarabika!

    Hapa dreva akimuona binadamu anavuka barabara kwa mbali anapiga honi utafikiri ameona nyoka njiani, wakati muda wa kupiga honi angepunguza tu mwendo, mtu akapita. Kwa bahati mabaya nchi yetu haijawa na motor-way za madereva kupima uwezo wao kwa spidi!! Dreva akiwa kwenye njia anajiona yeye tu ndo mwenye haki ya kutumia hiyo njia! Ndugu zangu, ni dreva wa treni tu ndo amepewa haki miliki ya njia yake, hata ukigongwa pale unashatkiwa kuwa umeigonga treni.

    Na kwa bahati mbaya hapa kwetu barabara hazijaweka vizuizi kuwalinda watembea kwa miguu, hivyo madereva wanatakiwa wawe makini sana. Nafikiri ndo maana Wafaransa waliojenga Ubungo - Kimara baadhi ya sehemu waliweka mitaro mikubwa kuwa dreva akitaka manjonjo atumbukie humo bila kwenda upande wa watembea kwa miguu.

    hata watembea kwa miguu, inabidi muwe makini sana sana sana! Na hii tabia ya vituo vya msaada, inasumbua saaana! Wahusika mko wapi??

    Hivyo ustaarabu usiwe tu kuwalinda wanyama huko Mikumi, angalieni njia zote!!

    ReplyDelete
  4. Unachosema hapo #1 juu ni sahihi kabisa.Lakini bado madereva wanatakiwa kupewa elimu zaidi.Sina Imani kama madereva wa Tanzania wana akili timamu.EBU angalia hii;Ukiwambia watumie saa moja kutoka pointi A kwenda B watatumia kweli saa moja,lakini 3/4 ya huo umbali ni mbio sana(Overspeeding) halafu 1/4 ya umbali wanapunguza mwendo au kusimama kabisa ili kubalance muda!.Kwa hiyo wakifika point B mkaguzi anaona kweli wametumia saa moja.Upo hapo?Ni vichekesho.Lakini Mbona kule Ngorongoro-Naabi-Seronera-Ikoma/Ndabaka wanaweza?,Overspeed uone moto wake,na wanapatrol barabara zote Defender za 'kufa mtu'.Faini zaon ni kubwa sana,na utazilipa(Hakuna Rushwa!)

    David V

    ReplyDelete
  5. Tuangalie namna bora ya kuishi pamoja bila ya kudhuriana kwa kutumia tekinolojia ya kisasa na siyo simu ya kupigiana. Satelaiti ziko kwa ajili hiyo na njia kadhaa za data capture. Hata hivyo nao wanyama nao wamekuwa wakitujeruhi, je data zao mnazo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...