Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema  matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.


Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa  ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.



 Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).



Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.



Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongereni sana kwa kufafanua jambo hili. Kuchakachua si jambo geni.

    Ingefaa NECTA iweke tarehe maalumu ya February ambayo itakuwa ndiyo tarehe na siku maalumu ya kutoa matokeo ya Kidato cha Nne. Tarehe maalumu kwa kutoa matokeo ya Kidato cha Sita n.k. Kusema tu yanatoka February. Mwezi ni mrefu kwa hamasa inavyokuwa!

    ReplyDelete
  2. NAWAPONGEZA JOPO LA MICHUZI BLOG, NA HII IWE FUNDISHO KWA BLOG UCHWARA ZINAZOJIFANYA NI MANAIBU MAKATIBU WA NECTA/ WIZARA NA KUSAMBAZA HABARI ZA UONGO IKIWEMO KUWEKA TOP TEN YA WALIOFAULU. AIBU KWAO KWANI WANARUDISHA MAENDELEO NYUMA

    ReplyDelete
  3. mi naishauri necta ituweke wanafunzi katika hali itayotufanya tujijue tulipotoka na tunapokwenda tena kwa wakati yaani iwe inatoa tarehe maalum ya kutoa matokeo

    ReplyDelete
  4. Vizuri wamesema wenyewe maana kila mtu alikuwa na tetesi zake

    ReplyDelete
  5. matokeoo yanatoka lini tena brotherr


































































    ReplyDelete
  6. kikubwa wekeni tarehe maalumu ya kutangaza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...