Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa China Xi Jinping wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA.Viongozi hao waliweka mashada hayo ya maua katika makaburi hayo yaliyopo katika kijiji cha Majohe,Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakiweka maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA huko katika kijiji cha Majohe,Ukonga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wa Rais Xi Jinping wakishuhudia(picha na Freddy Maro).
Wadau naomba kuuliza swali. Kwanini rais wa taifa kubwa kama China anatumia ndege ya ki-Marekani?
ReplyDeletewe anony wa 10:59pm Jibu ni kwa sababu kila mtu akitengeneza ndege nani atanunua ndege kwa mwenzake...ni mambo ya kawaida tu ya kibiashara, huzalishi kila kitu unazalisha kile ambacho unakizalisha kwa ufanisi na gharama ndogo zaidi kuliko mwingine.
ReplyDeleteMtoa Maoni wa 2 umenena Kiuchumi sana.
ReplyDeleteNi kwa Kimombo 'Comparative advantage' na 'Comparative costs'
HAKUNA "we anony wa 10:59pm"
ReplyDelete