Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto), akiwa na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Bw. Heikki Holmas, muda mfupi kabla ya kusaini Mkataba wa Krona 700 (sawa na sh. bilioni 200 za Tanzania) uliotolewa na Serikali ya Norway kwa Watanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto), akitiliana saini na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Bw. Heikki Holmas kuhusu msaada wa Krona 700 (sawa na sh. Bilioni 200 za kitanzania) kutoka Serikali ya Norway kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya miradi ya umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto), akipeana mkono na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Bw. Heikki Holmas, baada ya kusaini mkataba wa Krona 700 (sawa na sh. Bilioni 200 za Tanzania) uliotolewa na Serikali ya Norway kwa Watanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kila siku nasikia msaada msaada. Halafu mnasaini mikataba, ebo sasa msaada gani tena? inabidi kusema kuwa ni mkopo na sio msaada. Kama mtu anakusaidia kwa nini uanze kutia sahihi?

    Machozi

    ReplyDelete
  2. krona 700 za kinorway sio shillingi bilioni 200, hesabu imekosewa hiyo

    ReplyDelete
  3. Hizo lazima watazitumia vibaya, kwasababu sisi hatuna mpango wa kupeleka umeme vijijini kwasasa, kwavile mjini penyewe hakuna umeme ndo tupeleke vijijini hicho kitakuwa kitu cha ajabu sana na hatutegemei kufanya maajabu hayo bali ni vituko tu hamna kitu.

    ReplyDelete
  4. Hakuna lolote hapo, hizo hela zitaliwa na wajanja, nchi inuka ufisadi

    ReplyDelete
  5. nenda TANESCO ulipe gharama za kuingiza umeme kukiwa kunahitjika nguzo ndo utajua hii misaada ni dili za watu zaidi kuliko huduma kwa jamii. Mimi nina miezi 2 tangu nilipie gharama za kuingiza umeme kila nikiuliza naambiwa TANESCO hakuna nguzo kwa sasa.

    ReplyDelete
  6. Maoni yangu kuhusu Sintofahamu za kila mara ktk Masuala ya Kifedha na Mikataba, nadhani tuwe na Utamaduni wa kualika Wakaguzi na Wasimamizi wa Matumizi kwa ulinganishi wa Matekelezo ya Miradi.

    -----------------------------------
    Huu ni utaratibu wa kuendesha Mradi wakati matumizi yakifanyika hatua moja hadi nyingine kunaitwa wakaguzi wa Viwango vya Ubora na Wakaguzi wa Kifedha kutathimini kama kilichofanyika kinalingana na thamani halisi ya fedha?,,,Sio Utaratibu ule wa Kipindi cha Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambapo fungu likitoka inasubiriwa Ripoti ya kukamilika kwa Mradi bila kufuatilia hatua kwa hatua mchakato wa Matekelezo ya Mradi
    -----------------------------------

    Nchi hizi zinaongoza kwa utaratibu huo:

    1.UJERUMANI,
    2.JAPAN,
    3.CANADA.

    Ni vigumu kusikia Miradi imepewa fedha na matumizi mabaya ya fedha yakafanyika kwenye Miradi ya nchi hizo 3 hapo juu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...