Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria kukifungua rasmi Kiwanda cha maji ya Kunywa cha Super Shine Kinachomilikiwa na Kampuni ya Safari yenye Makao Makuu yake Nchini India.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayesimamia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee akiwa na akiambatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kukagua baadhi ya sehemu ya KiwandaKipya cha Maji ya kunywa kiliopo maeneo ya Viwanda Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia baadhi ya mashine za Kiwanda cha maji ya kunywa kiliopo maeneo huru ya Viwanda yaliopo Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia moja ya sampuli ya chupa ya maji yenye ujazo wa nusu lita ambayo tayari imeshakamilika utayarishaji wake katika kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo Maeneo huru Amani.
wasanii wa Kikundi cha sanaa Zanzibar wakitoa burdani safi katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo amani maeneo huru ya viwanda.
Balozi Seif akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wakishangiria moja ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na kikundi cha sanaa kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo maeneo huru ya Viwanda Amani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa hapo maeneo huru amani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Safari inayomiliki kiwanda cha maji ya kunywa cha Super Shine kiliopo amani maeneo huru na Bibi Mala Kalwan mara baada ya uzinduzi wa kiwanda hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na wale wa Kampuni ya Safari inayomiliki Kiwanda cha maji ya kunywa hapo amani eneo huru la Viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2013

    Biashara ya maji ya chupa ni faida tupu Zanzibar.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2013

    Anamiliki maji ya kunywa? Lo!

    ReplyDelete
  3. Mi najiuliza ikiwa wananchi hawana maji je wenye viwanda wanapata wapi maji ya kuuza? hapo tujiulize wenye viwanda wanauwezo gani kuliko serikali?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...