Na VOA

Tanzania na mataifa jirani ya Afrika Mashariki yanatajwa kuwa yanaweza kuboresha pato la ndani la mwaka – GDP – kama yatachukua hatua za kuboresha ubora wa bandari ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyopewa kichwa cha ‘Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania’ iliyoandikwa na Jacques Morisset, mchumi mkuu wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Uganda na Burundi, Tanzania na majirani zake wanaweza kuongeza pato lao la ndani kwa kiwango kikubwa.
Ripoti hiyo inasema Tanzania inaweza kuongeza pato lake la ndani kwa kiasi cha dola bilioni 1.8  na nchi jirani zinaweza kupandisha pato la ndani kwa dola milioni 830 kwa mwaka, kiwango ambacho kinaelezewa ni hasara iliyotokea mwaka 2012.

Ripoti hiyo inasema kuwa bandari ya Dar es Salaam iko katika njia kuu ya biashara ya Tanzania kwa asilimia 90, na inashughulikia bidhaa zinazogharimu dola bilioni 15 kwa mwaka, sawa na asilimia 60 ya pato la ndani la Tanzania kwa mwaka 2012.

Bandari hiyo pia inaelezewa kuwa inatumiwa na majirani sita wa Tanzania, ambao nchi zao hazina bandari, nchi hizo ni Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mwaka 2012 pekee, ripoti inasema hasara ya jumla inayoelezewa ambayo imetokea katika bandari hiyo imefikia dola bilioni 1.8 kwa uchumi wa Tanzania na dola milioni 830 kwa nchi jirani. Hasara ambayo ni sawa na asilimia saba ya pato la ndani la mwaka la Tanzania, na kwa kiasi kikubwa imeathiri wanunuzi wa ndani, biashara na mashirika ya serikali.

Moja ya sababu ambazo inaelezewa zimechangia katika hasara hii ni utendaji mbaya wa bandari ya Dar es Salaam ambao umezigharimu nchi nyingine jirani nazo kupata hasara, na hivyo kulazimika kulipa fedha zaidi kwa bidhaa zinazoagiwa kutoka nje, ikiwemo bidhaa za msingi kama vile mafuta ghafi, simenti, mbolea na madawa.

Moja ya vigezo  vilivyoelezewa katika ripoti ambavyo vinachangia katika kusababisha  hasara ni pamoja na uchelewesho unaozikabili meli ambazo zinafika katika bandari ya Dar es Salaam.  Katikati ya mwaka 2012, meli zilisubiri kwa takriban siku 10 ili kuweza kuruhusiwa kutia nagan na siku 10 nyingine za ziada ili kuweza kushusha mizigo. 

Rushwa pia imetajwa kuwa ni kigezo kingine kinachochangia katika utendaji mbaya wa Bandar, kama chanzo cha utendaji mbaya na kusababisha hasara kubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2013

    Umaskini wetu ungekwish kabisa, kama tungejenga bandari ya maana na tukawa na utendaji mzuri, tukawa na barabara na reli za uhakika toka Dar mpaka tunduma, dar Kigoma/Rwanda na Dar Malawi!

    ReplyDelete
  2. Mikausho MikaliMay 22, 2013

    Hiki kitu kiko wazi siku nyingi.Nashangaa mpaka mzungu aje aseme ndo waziri anaibuka na kusema kwamba atakufa na watu wanaokwamisha utendaji wa bandari hii.
    Kingine ni lazima kuimarisha mashirika ya reli na kubadili reli ya kati na kuwa yenye upana wa sasa wa kimataifa .Maana yake ni kufumua reli iliyopo na kujenga mpya(kujenga reli ni nafuu kuliko barabara na itaokoa sana uharibifu wa barabara unaofanywa na maroli) itakayounganisha mapaka nchi z aRwanda ,Burundi, na Uganda

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2013

    Msemaji aliyesema kupanua: reli ikipaniliwa wazee wetu watakula wapi? Barabara ndio huwapa kula. Ukiwazibia wakikutambua utang'olewa kucha na meno

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...