Mnara wa Askari jijini Dar es salaam enzi hizi na hizi sasa.
Hii  ni kumbukumbu ya askari jeshi waliopigana katika vita ya kwanza ya dunia inayosimama kuangalia bandari ya jiji hilo. 
Ilizinduliwa mwaka 1927. Sanamu hiyo ya askari wa British Carrier Corps iliundwa Uingereza na mchonga sanamu Mwingrereza aitwaye James Alexander Stevenson ambaye katika sanamu hii katumia jina lake la kufikirika la “Myrander”. 
Kabla ya kupelekwa Dar es salaam sanamu hii ya Askairi ilioneshwa kwa muda jijini London katka Royal Academy. Kabla ya kuwekwa sanamu ya askari, mahali hapa palikuwa na sanamu ya Meja Herman von Wissman, gavana wa wakati huo wa German East Africa, iliyozinduliwa mwaka 1911. Waingereza walipoingia Dar es salaam mwaka 1916, waliibomoa sanamu ya gavana wa Kijerumani pamoja na zingine za Karl Peter na Otto vo Bismarck zilizokuwa hapo. Sanamu ya askari ya Dar es salaam ni moja kati ya tatu zilizozinduliwa wakati mmoja kati ya tatu zilizoweka katika mwaka huo wa 1927 sehemu za koloni ya Uingereza ya Afrika Mashariki (British East Africa). Zingine mbili zilikuwa Mombada na Nairobi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2013

    Awesome. Very educative.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2013

    Asante kwa kutupatia historia hii.

    Uendelee kutuelimisha.

    ReplyDelete
  3. Al MusomaMay 01, 2013

    Kumbe kanzu fupi hazijaanza juzi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2013

    Ohhh ala kumbe ndio hivyo siyo?

    Sasa yote hayo na kuibomoa Sanamu ya wenzao ya nini?

    Ndio maana Mwingereza na Mjerumani ni kama Mzaramo na Mnyamwezi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2013

    Baada ya Talaka mara zote Mtalikiwa hukumbuka alipokuwa kwenye Ndoa!

    Kwa matatizo kama kushuka kwa Kiawango cha Elimu tunamkumbuka Mwingereza!

    Kwa uzembe ktk sehemu za Kazi tunamkubmuka Mjerumani na Kiboko Mkononi!

    Lakini kubwa ya yote kwa anayotufanyia Mwingereza na kutupangia (MPANGO WA NDOA ZA JINSIA MOJA KUWA SHARITI LA KUPEWA MISAADA YA MAENDELEO) ni bora wangerudisha Sanamu ya Meja wa Kijerumani Hermann Von Wismann!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2013

    Eti, kumbe hawa wenye kanzu, kofia na mabaibui ndio wenye mji hapo.

    Sasa ni nani baadae amewasukuma hadi hawaonekani tena, ni haohao Waingereza au?

    Tafakuri!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...